CCM YAIHAKIKISHIA JUMUIA YA KIMATAIFA MAZINGIRA WEZESHI NA RAFIKI YA UWEKEZESHAJI NCHINI

CCM YAIHAKIKISHIA JUMUIA YA KIMATAIFA MAZINGIRA WEZESHI NA RAFIKI YA UWEKEZESHAJI NCHINI - Hallo rafiki WORLD MAELEZO LATEST, Katika makala kusoma wakati huu na kichwa CCM YAIHAKIKISHIA JUMUIA YA KIMATAIFA MAZINGIRA WEZESHI NA RAFIKI YA UWEKEZESHAJI NCHINI, tumeandaa vizuri kwa makala hii kusoma na kupakua maelezo humo. pengine kujaza posts makala afya, makala biashara, makala general, makala hobby, makala karibuni info, makala michezo, makala siasa, makala utamaduni, sisi kuandika anaweza kuelewa. Naam, furaha ya kusoma.

title : CCM YAIHAKIKISHIA JUMUIA YA KIMATAIFA MAZINGIRA WEZESHI NA RAFIKI YA UWEKEZESHAJI NCHINI
kiungo : CCM YAIHAKIKISHIA JUMUIA YA KIMATAIFA MAZINGIRA WEZESHI NA RAFIKI YA UWEKEZESHAJI NCHINI

soma pia


CCM YAIHAKIKISHIA JUMUIA YA KIMATAIFA MAZINGIRA WEZESHI NA RAFIKI YA UWEKEZESHAJI NCHINI

Chama Cha Mapinduzi (CCM) kimeihakikishia Jumuia ya kimataifa mazingira mazuri, wezeshi na rafiki kwa uwekezaji nchini. Kauli ya CCM imetolewa leo na Ndg. Humphrey Polepole Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM.

Akiambatana na Maafisa wa Idara ya Siasa na Uhusiano wa Kimataifa (SUKI) Ndg. Polepole amefanya mazungunzo ya kirafiki na Mabalozi wawili Bi. Matli na Bwana Arthur Matli wa nchi ya Uswisi wanaowakilisha Tanzania pamoja na Afrika Mashariki na Zambia.
Katika mazungumzo hayo Ndg. Polepole amefafanua juu ya Mageuzi makubwa ambayo CCM inayafanya katika Chama na Serikali na ambayo yanalenga kuongeza tija, ufanisi na utumishi wa watu. Aidha amewajulisha Mabalozi hao kuwa Chama kimeielekeza Serikali kupitia mikataba ya Madini ili kuhakikisha haki ya Tanzania inapatikana na kwamba baada ya mapitio kumefanyika majadiliano na mashauriano na wawekezaji ambao wameridhia kwa moyo mmoja kuingia katika utaratibu mpya ambao unalinda haki ya watanzania na wawekezaji pia. 

"Chama Cha Mapinduzi kimeendelea kuielekeza Serikali kuendelea kuweka mazingira rafiki, wezeshi na mazuri kwa wawekezaji ambao wako tayari kuja kuwekeza hapa Tanzania na hasa katika eneo la viwanda. Serikali imetenga ardhi ya kutosha kwa uwekezaji mkubwa, imeweka utaratibu mzuri kupitia kituo cha uwekezaji (TIC) na hivyo yeyote mwenye nia ya kuwekeza anakaribishwa. Kama kuna mwekezaji ambaye amepata changamoto katika mchakato wa kuwekeza nchini au anapata ugumu wowote asisite kutoa taarifa na Serikali ya CCM itashughulikia changamoto hizo" amesema Ndg. Polepole.
Naye Balozi wa Uswisi nchini Tanzania amesema amefarijika sana kwa mazungumzo na yamemwongezea Imani zaidi kwasababu amepata kujua mambo mengi tofauti na habari ambazo anazisikia zikiwemo zinazopotoshwa. "Nakuhakikishia kwamba wakati wowote atakapopatikana mwekezaji nitamleta mara moja Tanzania, na ninapendekeza utaratibu huu wa mazungumzo uendelee" amesema Bi. Matli Balozi wa Uswisi Nchini Tanzania  

Huu ni mwendelezo wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) kuimarisha mahusiano ya ndani na nje katika eneo la siasa, diplomasia na uchumi.

Imetolewa na,

IDARA YA ITIKADI NA UENEZI
CHAMA CHA MAPINDUZI (CCM)
OND LUMUMBA


Hivyo makala CCM YAIHAKIKISHIA JUMUIA YA KIMATAIFA MAZINGIRA WEZESHI NA RAFIKI YA UWEKEZESHAJI NCHINI

yaani makala yote CCM YAIHAKIKISHIA JUMUIA YA KIMATAIFA MAZINGIRA WEZESHI NA RAFIKI YA UWEKEZESHAJI NCHINI Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.

Wewe ni sasa kusoma makala CCM YAIHAKIKISHIA JUMUIA YA KIMATAIFA MAZINGIRA WEZESHI NA RAFIKI YA UWEKEZESHAJI NCHINI mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2018/06/ccm-yaihakikishia-jumuia-ya-kimataifa.html

Subscribe to receive free email updates:

0 Response to "CCM YAIHAKIKISHIA JUMUIA YA KIMATAIFA MAZINGIRA WEZESHI NA RAFIKI YA UWEKEZESHAJI NCHINI"

Post a Comment