BALOZI SEIF AKABIDHI MASHINE YA BOTI KWA VIJANA WA KIKUNDI CHA HAMASA

BALOZI SEIF AKABIDHI MASHINE YA BOTI KWA VIJANA WA KIKUNDI CHA HAMASA - Hallo rafiki WORLD MAELEZO LATEST, Katika makala kusoma wakati huu na kichwa BALOZI SEIF AKABIDHI MASHINE YA BOTI KWA VIJANA WA KIKUNDI CHA HAMASA, tumeandaa vizuri kwa makala hii kusoma na kupakua maelezo humo. pengine kujaza posts makala afya, makala biashara, makala general, makala hobby, makala karibuni info, makala michezo, makala siasa, makala utamaduni, sisi kuandika anaweza kuelewa. Naam, furaha ya kusoma.

title : BALOZI SEIF AKABIDHI MASHINE YA BOTI KWA VIJANA WA KIKUNDI CHA HAMASA
kiungo : BALOZI SEIF AKABIDHI MASHINE YA BOTI KWA VIJANA WA KIKUNDI CHA HAMASA

soma pia


BALOZI SEIF AKABIDHI MASHINE YA BOTI KWA VIJANA WA KIKUNDI CHA HAMASA

Mwakilishi wa Jimbo la Mahonda Balozi Seif Ali Iddi alisema kwamba Viongozi wa Jimbo hilo wataendelea kuwaunga mkono  Wananchi wao hasa Vijana na Akina Mama walioamua kujituma katika muelekeo wa kujitafutia Maendeleo ili kujenga hatma njema ya maisha yao.

Alisema misaada ya kuyawezesha Makundi hayo katika kuyapatia vifaa, mtaji sambamba na  maarifa itakuwa ikiendelea kila wakati kulingana na mahitaji halisi ya Wananchi ikilenga zaidi katika Vikundi vya Ushirika.

Balozi Seif Ali Iddi alisema hayo wakati akikabidhi msaada wa  Mashine iliyoitanguliwa  na  Boti ya kuvulia Samaki  aliyoitoa kwa Kushirikiana na Mbunge wa Jimbo hilo Mh. Bahati Abeid Nassir kwa ajili ya Vijana wa  Kikundi cha Hamasa cha Jimbo la Mahonda chenye Mastakimu yake Kijiji cha Fujoni hafla iliyofanyika Nyumbani kwake Kama Kaskazini kidogo ya Mji wa Zanzibar.

Alisema hakuna Tajiri au Kikundi cha Jamii kilichopata utajiri wa kushtukia  bila ya kufanya kazi za ziada katika kujitafutia riziki ambazo Wanakikundi hao watalazimika kufanya jitihada zitakazowawezesha kujikwamua kutoka  katika mazingira magumu ya maisha.

Balozi Seif  aliwatahadharisha Wanachama wa Kikundi hicho cha Hamasa kwamba msaada huo wa Boti na Mshine yake  usije geuka kuwa chanzo cha  kuleta mifarakano baina yao.

Aliwataka Wanakikundi hao wapatao 50 walio jinsia mbili tofauti  wafanye kazi kwa juhudi zao zote ili vifaa vya msaada waliopatiwa  viwezeshe kuzaa vyengine kwa lengo la kutanua mradi wao unaopaswa kuwa wa kudumu.
  Mwakilishi wa Jimbo la Mahonda Balozi Seif Ali Iddi Kushoto akimkabidhi Mashine ya Boti Katibu wa Kikundi cha Hamasisha cha Jimbo la Mahonda Bibi  Mwanapatima Othman Salum kwa ajili ya shughuli za Uvuvi za Kikundi hicho. Kati kati yao ni Mkuu wa Nidhamu wa Kikundi cha Hamasa Bwana Kichamu Haji Abdullah.
 Mke wa Mwakilishi wa Jimbo la Mahonda Mama Asha Sul;eiman Iddi akitoa nasaha kwa Wanachama wa Kikundi cha Hamasa mara baada ya kukabidhiwa Mashine ya Boti hapo nyumbani kwae Kama.
 Mkuu wa Nidhamu wa Kikundi cha Hamasa Bwana Kichamu Haji Abdullah kwa niaba ya wana kikundi wenzake akitoa shukrani kwa Mwakilishi na Mbunge wa Jimbo la Mahonda  kwa uamuzi wao wa kuwapatia  Boti pamoja na Mashine yake kwa ajili ya shughuli za Uvuvi.
 Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi akijumuika pamoja na Viongozi na Wafanyakazi wa Ofisi yake katika futari ya pamoja iliyofanyika kwenye Makaazi yake Kama.
 Baadhi na Viongozi na Wafanyakazi wa Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar wakijipatia vyakula kwenye futari ya pamoja iliyoandaliwa na Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif. 
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mh. Mohamed Aboud Mohamed akitoa neon la shukrani mara baada ya futari ya pamoja iliyofanyika nyumbani kwa Balozi Seif. Picha na – OMPR – ZNZ.


KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA


Hivyo makala BALOZI SEIF AKABIDHI MASHINE YA BOTI KWA VIJANA WA KIKUNDI CHA HAMASA

yaani makala yote BALOZI SEIF AKABIDHI MASHINE YA BOTI KWA VIJANA WA KIKUNDI CHA HAMASA Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.

Wewe ni sasa kusoma makala BALOZI SEIF AKABIDHI MASHINE YA BOTI KWA VIJANA WA KIKUNDI CHA HAMASA mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2018/06/balozi-seif-akabidhi-mashine-ya-boti.html

Subscribe to receive free email updates:

0 Response to "BALOZI SEIF AKABIDHI MASHINE YA BOTI KWA VIJANA WA KIKUNDI CHA HAMASA"

Post a Comment