title : ASKARI JWTZ AUAWA AFRIKA YA KATI, WENGINE WATANO HALI ZAO SI NZURI
kiungo : ASKARI JWTZ AUAWA AFRIKA YA KATI, WENGINE WATANO HALI ZAO SI NZURI
ASKARI JWTZ AUAWA AFRIKA YA KATI, WENGINE WATANO HALI ZAO SI NZURI
Na Ripota Wetu, Globu ya jamii
JESHI la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) limesema kuwa askari wake mmoja ameuawa na wengine watano hali zao si nzuri baada ya kushambuliwa na kikundi cha waasi kinachojulikana kwa jina la Siriri kilichopo Jamhuri ya Afrika ya Kati.
Taarifa ya kifo cha mwanajeshi huyo imetolewa leo jijini Dar es Salaam na Mkurugenzi wa Habari na Uhusiano wa JWTZ Kanali Ramadhan Dogoli ambapo akifafanua kuhusu kifo hicho amesema Juni kuwa 3 mwaka huu kikundi chetu cha wanajeshi , maofisa na askari ambao idadi yao ilikuwa 90 kikiwa katika uwajibakaji kilishambuliwa na kikundi hicho cha waasi.
Amefafanua sehemu ya kikosi hicho cha kulinda amani kilichopo Jamhuri ya Afrika ya Kati(TANZBATT-1 CAR)baada ya kuanza kushambuliwa na waasi hao kwa kushtukizwa kiliamua kujibu mapigo.
"Kikundi chetu kilijihami kwa kujibu mapigo kijasiri na kufanikiwa kuwashinda nguvu washambuliaji na kwa bahati mbaya katika mapambano hayo askari wetu mmoja alipoteza maisa na wengine 18 walipata majeraha katika sehemu mbalimbali za miili yao,"amesema.
Ameongeza kati ya hao waliojrehiwa askari watano hali zao si nzuri sana na kuongeza kuwa "askari wetu waliojeruhiwa wanaendelea na matibabu katika Hospitali ya kanda ya Umoja wa Mataifa iliyopo Bangui katika Mji mkuu wa nchi hiyo".
Kanali Dogoli amesema mipango ya kuurejesha nyumbani mwili wa askari aliyepoteza maisha inafanywa na Umoja wa Mataifa na ikikamilika mwili huo utawasili nchini kwa taratibu za maziko
Hivyo makala ASKARI JWTZ AUAWA AFRIKA YA KATI, WENGINE WATANO HALI ZAO SI NZURI
yaani makala yote ASKARI JWTZ AUAWA AFRIKA YA KATI, WENGINE WATANO HALI ZAO SI NZURI Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala ASKARI JWTZ AUAWA AFRIKA YA KATI, WENGINE WATANO HALI ZAO SI NZURI mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2018/06/askari-jwtz-auawa-afrika-ya-kati.html
0 Response to "ASKARI JWTZ AUAWA AFRIKA YA KATI, WENGINE WATANO HALI ZAO SI NZURI"
Post a Comment