ALIYEJIFUNGUA WATOTO MAPACHA ,AENDELEA KUSOTA GEREZANI KARANGA

ALIYEJIFUNGUA WATOTO MAPACHA ,AENDELEA KUSOTA GEREZANI KARANGA - Hallo rafiki WORLD MAELEZO LATEST, Katika makala kusoma wakati huu na kichwa ALIYEJIFUNGUA WATOTO MAPACHA ,AENDELEA KUSOTA GEREZANI KARANGA, tumeandaa vizuri kwa makala hii kusoma na kupakua maelezo humo. pengine kujaza posts makala afya, makala biashara, makala general, makala hobby, makala karibuni info, makala michezo, makala siasa, makala utamaduni, sisi kuandika anaweza kuelewa. Naam, furaha ya kusoma.

title : ALIYEJIFUNGUA WATOTO MAPACHA ,AENDELEA KUSOTA GEREZANI KARANGA
kiungo : ALIYEJIFUNGUA WATOTO MAPACHA ,AENDELEA KUSOTA GEREZANI KARANGA

soma pia


ALIYEJIFUNGUA WATOTO MAPACHA ,AENDELEA KUSOTA GEREZANI KARANGA

Na Dixon Busagaga-MOSHI.

MWANAMKE aliyejifungua watoto Mapacha akiwa Mahabusu ,Marry Lukumay ameendelea kusota Gerezani na watoto wake baada ya kukosekana kwa wadhamini wenye sifa zinazokidhi masharti yaliyotolewa na Mahakama.

Miongoni mwa masharti ya dhamana yaliyotolewa na Mahakama ya Hakimu mkazi ,Moshi ni pamoja na kuwa na wadhamini wawili ambao ni wakazi wa mkoa wa Kilimanjaro watakaosaini Fungu la Dhamana la kiasi cha sh laki tano kila mmoja.Marry Lukumay mkazi wa Babati mkoani Manyara kwa mara nyingine alifikishwa mahakama ya hakimu Mkazi ,Moshi baada ya kukamatwa Oktoba 15 mwaka jana kwa madai ya kukutwa na Mirungi kilogramu 10.

Katika shauri hilo namba 182 la mwaka 2017 ,mwendesha mashtaka upande wa Jamhuri ,Lilian Kowelo aliiomba mahakama kupanga tarehe nyingine ya kutajwa kwa shauri hilo kutokana na upelelezi kutokamilika .Hakimu anayesikiliza shauri hilo ,Pamela Meena alikubaliana na ombi hilo na kupanga June 27 mwaka huu ,mtuhumiwa kufikishwa mahakamani hapo kwa ajili ya kutajwa kwa shauri hilo.

Akizungumza na mwanahabari wetu nje ya Mahakama ,Mwanamke huyo aliyewapa majina watoto wake ya Nora na Noreen wenye umri sasa wa miezi miwili sasa alisema alikamatwa mwaka jana katika eneo la Himo Oktoba mwaka jana.Alisema kuwa, Oktoba 24 Mwaka jana alifikishwa mahakamani kwa mara ya kwanza na kusomewa shitaka linalomkabili na kuelezwa kuwa dhamana yake ipo wazi huku akitakiwa kuwa na wadhamini wawili.

Mary anayeshikiliwa katika Gereza la Karanga mkoani Kilimanjaro alisema wakati anakamatwa tayari alikuwa na ujauzito wa miezi miwili na Aprily 8 mwaka huu alijifungua watoto hao Mapacha katika Hospitali ya Rufaa ya mkoa wa Kilimanjaro ,Mawenzi .


Hivyo makala ALIYEJIFUNGUA WATOTO MAPACHA ,AENDELEA KUSOTA GEREZANI KARANGA

yaani makala yote ALIYEJIFUNGUA WATOTO MAPACHA ,AENDELEA KUSOTA GEREZANI KARANGA Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.

Wewe ni sasa kusoma makala ALIYEJIFUNGUA WATOTO MAPACHA ,AENDELEA KUSOTA GEREZANI KARANGA mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2018/06/aliyejifungua-watoto-mapacha-aendelea.html

Subscribe to receive free email updates:

0 Response to "ALIYEJIFUNGUA WATOTO MAPACHA ,AENDELEA KUSOTA GEREZANI KARANGA"

Post a Comment