title : ZAWADI PEKEE YA KUWAPA WATOTO WENU KATIKA KIPINDI CHA SIKUKUU NI KUWAKATIA TOTO AFYA KADI
kiungo : ZAWADI PEKEE YA KUWAPA WATOTO WENU KATIKA KIPINDI CHA SIKUKUU NI KUWAKATIA TOTO AFYA KADI
ZAWADI PEKEE YA KUWAPA WATOTO WENU KATIKA KIPINDI CHA SIKUKUU NI KUWAKATIA TOTO AFYA KADI
WAZAZI na Walezi mkoani Tanga wametakiwa kuhakikisha wanawapa watoto wao zawadi kwenye kpindi cha mwezi mtukufu wa ramadhani kwa kuwaingiza kwenye mpango wa Toto Afya Kadi ili waweze kunufaika na matibabu wakati wanapougua.
Hayo yalisemwa na Afisa Matekelezo wa Mfuko wa Bima ya Afya Mkoani Tanga (NHIF) Macrina Clemens (Pichani Juu) ambapo alisema zawadi hiyo ni muhimu sana katika ukuaji wao badala ya kuwanunulia nguo ambazo wanavaa kwa wakati Fulani na baaadae kwisha.
Alisema mpango huo ni muhimu kwa watoto wao kutokana na kuwahakikishia kupata huduma za matibabu wakati wote wanapokumbana na magonjwa mbalimbali ambayo yanaweza kuathiri.
“Ndugu zangu wazazi na walezi kwenye kipindi hiki cha mwezi wa ramadhani zawadi mzuri ambayo mnaweza kuwapatia watoto wenu ni kuwaingiza kwenye mpango huu wa Toto Afya Kadi kwani malipo yake yana muwezesha mtoto kupata huduma za matibabu mwaka mzima kwa kiasi cha sh.50400”Alisema.
Hata hivyo alisema wataendelea kuhimiza wananchi kuweza kuwaingiza watoto wao kwenye mpango huo ili waweze kuwahakikishia watoto wao kupata huduma za matibabu bila vikwazo hasa wanapokuwa wakiumwa .(Habari kwa Hisani ya Blog ya Kijamii ya Tanga Raha)
Hivyo makala ZAWADI PEKEE YA KUWAPA WATOTO WENU KATIKA KIPINDI CHA SIKUKUU NI KUWAKATIA TOTO AFYA KADI
yaani makala yote ZAWADI PEKEE YA KUWAPA WATOTO WENU KATIKA KIPINDI CHA SIKUKUU NI KUWAKATIA TOTO AFYA KADI Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala ZAWADI PEKEE YA KUWAPA WATOTO WENU KATIKA KIPINDI CHA SIKUKUU NI KUWAKATIA TOTO AFYA KADI mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2018/05/zawadi-pekee-ya-kuwapa-watoto-wenu.html
0 Response to "ZAWADI PEKEE YA KUWAPA WATOTO WENU KATIKA KIPINDI CHA SIKUKUU NI KUWAKATIA TOTO AFYA KADI"
Post a Comment