title : YANGA YAENDELEA KUSHIKA MKIA KUNDI "D" CAF, YATOKA SARE NA RAYON
kiungo : YANGA YAENDELEA KUSHIKA MKIA KUNDI "D" CAF, YATOKA SARE NA RAYON
YANGA YAENDELEA KUSHIKA MKIA KUNDI "D" CAF, YATOKA SARE NA RAYON
Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii.
Wawakilishi wa Tanzania katika Kombe la Shirikisho Barani Afrika Yanga wameshindwa kuondoka na ushindi dhidi ya Rayon ya Rwanda baada ya kulazimishwa suluhu ya kutokufungana.
Yanga waliokuwa katika dimbani la nyumbani la Uwanja wa Taifa walikubali matokeo hayo baada ya kushindwa kupata goli la ushindi ma matokeo kuishia 1-1.
Mchezo huo ulioanza majira ya saa 1 usiku Yanga waliweza kucheza vizuri katika kipindi cha kwanza wakionekana kutawala sehemu ya kiungo kilichokuwa kinaendeshwa na Thaban Kamosoku na Pius Buswita.
Kocha msaidizi wa Yanga Noel Mwandila amesema kuwa hajaridhishwa na matokeo ya leo dhidi ya Rayon Sports kwani walihitaji ushindi ili kuweza kujiweka katika nafasi nzuri ya kufuzu kwenda hatua inayofuata.
"Sijaridhishwa na matokeo ya leo, katika mchezo huu tulihitaji ushindi ili kuweza kujiweka kwenye nafasi nzuri ya kwenda hatua inayofuata ila wachezaji walikosa umakini na kushindwa kutumia nafasi walizozitumia,"amesema Mwandila.
Mwandila amesema kwa sasa mashindano haya yanasimama kwa muda mpaka mwezi wa saba kwahiyo watatumia kipindi hiki kwa ajili ya kukiunda kikosi na kukifanyia marekebisho kwenye nafasi zinazohitajika na zaidi watahakikisha wanafanya vizuri kwenye michezo inayofuata.
Baada ya mechi hii Yanga wanakuwa na alama 1 baada ya mchezo wa kwanza kufungwa huku Rayon wakiwa ma alama 2.
Hivyo makala YANGA YAENDELEA KUSHIKA MKIA KUNDI "D" CAF, YATOKA SARE NA RAYON
yaani makala yote YANGA YAENDELEA KUSHIKA MKIA KUNDI "D" CAF, YATOKA SARE NA RAYON Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala YANGA YAENDELEA KUSHIKA MKIA KUNDI "D" CAF, YATOKA SARE NA RAYON mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2018/05/yanga-yaendelea-kushika-mkia-kundi-d.html
0 Response to "YANGA YAENDELEA KUSHIKA MKIA KUNDI "D" CAF, YATOKA SARE NA RAYON"
Post a Comment