title : WIZARA YA AFYA YAWAONYA WANATOA HUDUMA ZA KIMAABARA BILA VIBALI
kiungo : WIZARA YA AFYA YAWAONYA WANATOA HUDUMA ZA KIMAABARA BILA VIBALI
WIZARA YA AFYA YAWAONYA WANATOA HUDUMA ZA KIMAABARA BILA VIBALI
Na Agness Francis, Globu ya Jamii
WIZARA ya Afya,Maendeleo ya Jami, Jinsia, Wazee na Watoto imewataka watoa huduma za kimaabara kwa wananchi kuhakikisha wanakuwa na vibali kwani kinyume na hapo hatua za kisheria zitachukuliwa dhidi yao kwa mujibu wa wa sheria.
Akizungumza jijini Dar es Salaam leo , Mkurugenzi Msaidizi Huduma ya uchunguzi na magonjwa Dk. Charles Massambu amesisitiza sheria itachukua mkondo wake kwa wale wanaohudumia wananchi shughuli za kimaabara bila lakini hawana vibali au kusajiliwa.
"Hakuna mtoa huduma atakaetoa huduma za maabara bila kusajiliwa.Tukibaini tutachukua hatua za kisheria," amesema Dk. Massambu.
Aidha Massambu ameeleza baraza linatambua uwezo na utaalamu katika kuelimisha jamii ya watanzania kuhusu majukumu katika kuwahudumia.Pia kutokana na changamoto za majibu ya vipimo kutofautiana kutoka sehemu moja hadi nyingine Wizara imechukua hatua ya uhakiki wa ubora wa vipimo.
"Tanzania kuna maabara 33 ambazo ni nyota moja mpaka nne,nyingine nane zilizo na hadhi ya kimataifa ambapo vipimo vyake huwa ni sawa na vya nchi nyingine za nje.
Mkurugenzi msaidizi wa huduma za uchunguzi wa Magonjwa Dkt Charles G Massambu akizungumza na waandishi wa habari leo katika ofisi zao Jijini Dar es Salaam akiwataka watoa huduma ya maabara wasio na vibali kutoka baraza la wataalamu la maabara kujisajili au kuacha kufanya kazi hiyo.
Msajili wa Baraza la wataalamu wa maabara akizungumza na waandishi wa habari leo katika ofisi zao Jijini Dar es Salaam akielezea kuhusu umuhimu wa kusajili huduma hizo.(Picha na Emmanuel Massaka,Globu ya jamii)
KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA
KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA
Hivyo makala WIZARA YA AFYA YAWAONYA WANATOA HUDUMA ZA KIMAABARA BILA VIBALI
yaani makala yote WIZARA YA AFYA YAWAONYA WANATOA HUDUMA ZA KIMAABARA BILA VIBALI Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala WIZARA YA AFYA YAWAONYA WANATOA HUDUMA ZA KIMAABARA BILA VIBALI mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2018/05/wizara-ya-afya-yawaonya-wanatoa-huduma.html
0 Response to "WIZARA YA AFYA YAWAONYA WANATOA HUDUMA ZA KIMAABARA BILA VIBALI"
Post a Comment