title : WAZAZI WAHIMIZWA KUWAINGIZA WATOTO WAO KWENYE MPANGO WA TOTO AFYA KADI KWA UHAKIKA WA MATIBABU
kiungo : WAZAZI WAHIMIZWA KUWAINGIZA WATOTO WAO KWENYE MPANGO WA TOTO AFYA KADI KWA UHAKIKA WA MATIBABU
WAZAZI WAHIMIZWA KUWAINGIZA WATOTO WAO KWENYE MPANGO WA TOTO AFYA KADI KWA UHAKIKA WA MATIBABU
Na Editha Karlo wa blog ya jamii, Karagwe.
WAZAZI na walezi Mkoani Kagera katika kuelekea msimu wa sikukuu wametakiwa kuhakikisha wanawapatia watoto wao zawadi ya kuwaingiza kwenye mpango wa Toto afya kadi ili waweze kuwa na uhakika wa matibabu pale wanapougua.
Mkuu wa Wilaya ya Karagwe Godfrey Mheruka aliyasema hayo wakati wa uzinduzi wa zoezi la utoaji wa Kadi za toto afya pamoja na upimaji wa afya bure kwa wananchi wa magonjwa yasiyoambukiza zoezi lililofanyika katika stand ya magari ya Omurushaka Wilayani Karagwe.
Mheruka alisema kuwa mzazi au mlezi kumpatia mtoto zawadi ya kadi ya toto afya ni muhimu badala ya kumpatia zawadi ya nguo ambazo atazivaa na zitaisha."Ndugu zangu wazazi wenzangu baada ya kumaliza kipindi hiki cha mfungo wa mwezi mtukufu wa Ramadhani zawadi nzuri ya kuwapatia watoto wetu ni kuwaingiza katika mpango huu wa toto afya kadi kwani utamuwezesha mtoto kuwa na uhakika wa matibabu anapougua kwa kipindi cha mwaka mmoja"alisema Mkuu wa Wilaya
Mkuu huyo wa Wilaya alisema kuwa wataendelea kuhimiza wananchi waweze kuingiza watoto wao katika mpango huo.Meneja wa Mfuko wa bima ya Taifa ya afya(NHIF)Elias Odhiambo alisema kuwa wiki hii NHIF wanafanya zoezi la upimaji wa afya wananchi bure na kutoa toto afya kadi katika maeneo ya Omurushaka na Kayanga Wilayani Karagwe.
Alisema kuwa magonjwa wanayopima wananchi ni uwiano wa uzito na refu(BMI)Kisukari,shinikizo la damu(BP)pamoja na kutoa ushauri.Odhiambo amewataka wananchi wa Wilaya ya Karagwe kutumia fursa hiyo kujua hali za afya zao sambamba na kupata elimu ya kujikinga na maradhi lakini pia kujiunga na mfuko huo."Nawaomba wananchi wote wafike maeneo ambayo tumeweka vituo kwaajili ya tutoa huduma ili waweze kupata huduma kwani huduma hizi tunatoa bure"alisema
Alisema huduma ya toto afya kadi inahusisha watoto wenye umri chini ya miaka 8,ambapoatatakiwa kujaza fomu zinazopatikana nchi nzima chini ya uangalizi wa mzazi au mlezi.Alisema mwanachama wa toto afya kadi atapata huduma zote ambazo mwanachama wa NHIF ambazo anapata na ambazo zimeorodheshwa katika huduma.Baadhi ya wananchi waliofika katika uzinduzi huo wameupongeza mfuko wa bima ya afya kwa jitihada zake za kuwafikia na kuwahudumia wananchi katika maeneo yao.
"Mfuko huu umetusaidia kutuletea hii huduma ya upimaji wa afya kwani inatusaidia kujua afya zetu lakini pia tunapata fursa ya kuujua vizuri mfuko na huduma zake ambazo ndo mkombozi wa maisha ya kila mwananchi,tunaomba huduma kama hizi ziwe endelevu"alisema Edson Kamugisha.
Meneja wa mfuko wa bima ya afya Taifa(NHIF)Mkoa wa Kagera Elias Odhiambo akiongea jambona wananchi(hawapo pichani) wakati wa uzinduzi wa zoezi la upimaji wa afya bure kwa magonjwa yasiyoambukiza na utoaji wa toto afya kadi katika stand ya magari ya Omurushaka Wilayani Karagwe.
Mkuu wa Wilaya ya Karagwe Godfrey Mheruka akimkabithi kadi ya toto afya kadi mmoja wa watoto waliopatiwa kadi katika zoezi la uzinduzi wa kupima afya bure na utoaji wa toto afya kadi kwenye stand ya magari ya omurushaka Wilayani Karagwe
Ofisa matekelezo kutoka mfuko wa bima ya Taifa Mkoa wa Kagera Adam Kanza akiongea na wananchi katika stand ya magari ya Omurushaka juu ya umuhimu wa kuwakatia watoto wao toto afya kadi
Baadhi ya Wananchi wakifuatilia yaliyokuwa yakijiri uwanjani hapo.
Hivyo makala WAZAZI WAHIMIZWA KUWAINGIZA WATOTO WAO KWENYE MPANGO WA TOTO AFYA KADI KWA UHAKIKA WA MATIBABU
yaani makala yote WAZAZI WAHIMIZWA KUWAINGIZA WATOTO WAO KWENYE MPANGO WA TOTO AFYA KADI KWA UHAKIKA WA MATIBABU Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala WAZAZI WAHIMIZWA KUWAINGIZA WATOTO WAO KWENYE MPANGO WA TOTO AFYA KADI KWA UHAKIKA WA MATIBABU mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2018/05/wazazi-wahimizwa-kuwaingiza-watoto-wao.html
0 Response to "WAZAZI WAHIMIZWA KUWAINGIZA WATOTO WAO KWENYE MPANGO WA TOTO AFYA KADI KWA UHAKIKA WA MATIBABU"
Post a Comment