WAFANYABIASHARA WADOGO WADOGO 17,601 MOROGORO KUPATIWA VITAMBULISHO VYA TRA

WAFANYABIASHARA WADOGO WADOGO 17,601 MOROGORO KUPATIWA VITAMBULISHO VYA TRA - Hallo rafiki WORLD MAELEZO LATEST, Katika makala kusoma wakati huu na kichwa WAFANYABIASHARA WADOGO WADOGO 17,601 MOROGORO KUPATIWA VITAMBULISHO VYA TRA, tumeandaa vizuri kwa makala hii kusoma na kupakua maelezo humo. pengine kujaza posts makala afya, makala biashara, makala general, makala hobby, makala karibuni info, makala michezo, makala siasa, makala utamaduni, sisi kuandika anaweza kuelewa. Naam, furaha ya kusoma.

title : WAFANYABIASHARA WADOGO WADOGO 17,601 MOROGORO KUPATIWA VITAMBULISHO VYA TRA
kiungo : WAFANYABIASHARA WADOGO WADOGO 17,601 MOROGORO KUPATIWA VITAMBULISHO VYA TRA

soma pia


WAFANYABIASHARA WADOGO WADOGO 17,601 MOROGORO KUPATIWA VITAMBULISHO VYA TRA


Na Rachel Mkundai, Morogoro
Jumla ya wafanyabiashara wadogo wadogo 17,601 waliokuwa katika sekta isiyo rasmi mkoani Morogoro wametambuliwa na hivyo watapatiwa vitambulisho maalumu na Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) ili waweze kufanya biashara zao bila kusumbuliwa.  
Hayo yameelezwa na Kamishna wa kodi za ndani wa TRA Bw. Elijah Mwandumbya alipokuwa akitoa maelezo mafupi kuhusu zoezi la kuwatambua, kuwasajili na kuwapatia vitambulisho maalumu wafanyabiashara wadogo wadogo walio katika sekta isiyo rasmi wakati wa hafla ya uzinduzi iliyofanyika katika viwanja vya Masika mjini Morogoro.
Mwandumbya amesema zoezi la utambuzi linafanyika kwa kupitia vikundi vya wafanyabiashara ambapo katika mkoa wa Morogoro vikundi 1851 vyenye jumla ya wanachama 17,601 wametambuliwa na watapatiwa vitambulisho maalumu vyenye jina na mahali wanapofanyia biashara zao ambavyo watadumu nabyo kwa miaka mitatu.
Ameongeza kuwa kati ya hivyo 1,851, vikundi 473 vimeshapatiwa mafunzo ya umuhimu wa kutambuliwa, kusajiliwa na kupatiwa vitambulisho vya TRA, na kati ya hivyo vikundi 143 vyenye jumla ya wanachama 2,324 wameshasajiliwa ili waweze kufanya biashara zao bila usumbufu.
“Lengo ni kuhakikisha kuwa tunawatambua wafanyabiashara wadogo wadogo kwa idadi yao kwa ajili ya serikali kupanga mipango mizuri ya kuboresha biashara zao ziweze kuendelea na vile vile serikali iweze kuweka mipango mizuri ya kuwapatia huduma mbalimbali”, alisema Bw. Mwandumbya.
Akizindua zoezi hilo mkuu wa mkoa wa Morogoro Dkt Kebwe Steven Kebwe, amesema ulipaji wa kodi ni jambo zuri sana na mkoa wa Morogoro ni miongoni mwa mikoa inayofaidi matunda ya ulipaji kodi kwa kuwa na stendi nzuri ya kisasa ya mabasi ya abiria, stendi ya Msamvu.
“Nitoe rai kwa wafanyabiashara wa mkoa wa Morogoro kutumia fursa hii ya kujisajili na kupatiwa vitambulisho vya TRA ili mkoa uweze  kuwapatia huduma muhimu kama vile maeneo ya kufanyia biashara ikiwemo ndani ya stendi ya Msamvu”, ametoa rai.


Baadhi ya Wafanyabiashara ndogo ndogo Mkoani Morogoro wakishangilia kwa furaha mara baada ya kukabidhiwa vitambulisho maalum vinavyorasimisha rasmi shughuli zao za biashara mkoani hapo wakati wa uzinduzi wa utoaji vitambulisho kwa wafanyabiashara hao linalofanywa na Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA)   kwa kushirikiana na baadhi ya taasisi za Serikali, 21 Mei, 2018 mkoani hapo. (Imeandaliwa Robert Okanda Blogs)
Baadhi ya Wafanyabiashara ndogo ndogo Mkoani Morogoro wakiwa katika maandamano kuelekea viwanja vya Masika mkoani hapo wakiwa wamebeba bango lenye ujumbe wa usajili na utoaji vitambulisho kwa wafanyabiashara hao zoezi ambalo linafanywa na Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) kwa kushirikiana na baadhi ya taasisi za Serikali uliofanyika 21 Mei, 2018 mkoani hapo.
(Juu na chini) Baadhi ya Wafanyabiashara ndogo ndogo Mkoani Morogoro wakifuatilia kwa makini hotuba mbalimbali kutoka kwa mgeni rasmi pamoja na viongozi wa ngazi ya juu kutoka Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) wakati wa uzinduzi wa utoaji vitambulisho kwa wafanyabiashara hao 21 Mei, 2018 mkoani hapo.
Baadhi ya Wafanyabiashara ndogo ndogo Mkoani Morogoro wakipatiwa vitambulisho vyao vinavyorasimisha shughuli zao za biashara toka kwa mgeni rasmi Mkuu wa Mkoa wa Morogoro, Mhe. Dkt. Steven Kebwe (mwenye tai nyekundu) wakati wa uzinduzi wa utoaji vitambulisho kwa wafanyabiashara hao linalofanywa na Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA)   kwa kushirikiana na baadhi ya taasisi za Serikali, 21 Mei, 2018 mkoani hapo. 
Baadhi ya Wafanyabiashara ndogo ndogo Mkoani Morogoro wakipatiwa vitambulisho vyao vinavyorasimisha shughuli zao za biashara toka kwa mgeni rasmi Mkuu wa Mkoa wa Morogoro, Mhe. Dkt. Steven Kebwe (mwenye tai nyekundu) wakati wa uzinduzi wa utoaji vitambulisho kwa wafanyabiashara hao linalofanywa na Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA)   kwa kushirikiana na baadhi ya taasisi za Serikali, 21 Mei, 2018 mkoani hapo. 
Baadhi ya Wafanyabiashara ndogo ndogo Mkoani Morogoro wakipatiwa vitambulisho vyao vinavyorasimisha shughuli zao za biashara toka kwa mgeni rasmi Mkuu wa Mkoa wa Morogoro, Mhe. Dkt. Steven Kebwe (mwenye tai nyekundu) wakati wa uzinduzi wa utoaji vitambulisho kwa wafanyabiashara hao linalofanywa na Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA)   kwa kushirikiana na baadhi ya taasisi za Serikali, 21 Mei, 2018 mkoani hapo. 
Baadhi ya Wafanyabiashara ndogo ndogo Mkoani Morogoro wakipatiwa vitambulisho vyao vinavyorasimisha shughuli zao za biashara toka kwa mgeni rasmi Mkuu wa Mkoa wa Morogoro, Mhe. Dkt. Steven Kebwe (mwenye tai nyekundu) wakati wa uzinduzi wa utoaji vitambulisho kwa wafanyabiashara hao linalofanywa na Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA)   kwa kushirikiana na baadhi ya taasisi za Serikali, 21 Mei, 2018 mkoani hapo. (Picha na TRA)


Hivyo makala WAFANYABIASHARA WADOGO WADOGO 17,601 MOROGORO KUPATIWA VITAMBULISHO VYA TRA

yaani makala yote WAFANYABIASHARA WADOGO WADOGO 17,601 MOROGORO KUPATIWA VITAMBULISHO VYA TRA Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.

Wewe ni sasa kusoma makala WAFANYABIASHARA WADOGO WADOGO 17,601 MOROGORO KUPATIWA VITAMBULISHO VYA TRA mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2018/05/wafanyabiashara-wadogo-wadogo-17601.html

Subscribe to receive free email updates:

0 Response to "WAFANYABIASHARA WADOGO WADOGO 17,601 MOROGORO KUPATIWA VITAMBULISHO VYA TRA"

Post a Comment