title : UPELELEZI KESI KIGOGO WA TPA ANAYEDAIWA KUJILIMBIKIZA MALI ZA BILIONI 1.4/- BADO HAUJAKAMILIKA, APATA DHAMANA
kiungo : UPELELEZI KESI KIGOGO WA TPA ANAYEDAIWA KUJILIMBIKIZA MALI ZA BILIONI 1.4/- BADO HAUJAKAMILIKA, APATA DHAMANA
UPELELEZI KESI KIGOGO WA TPA ANAYEDAIWA KUJILIMBIKIZA MALI ZA BILIONI 1.4/- BADO HAUJAKAMILIKA, APATA DHAMANA
Na Karama Kenyunko,Globu ya jamii
MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi Kisutu ,imeelezwa upelelezi wa kesi ya kujilimbikizia mali zenye thamani ya Sh.bilioni 1.4 zisizolingana na kipato chake halali inayomkabili Meneja wa Fedha wa Mamlaka ya Bandari Tanzania,(TPA), Prosper Kimaro bado haujakamilika.
Taatifa hiyo imeelezwa leo mahakamani hapo na Wakili wa Serikali Vitalis Peter mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu Thomas Simba ambapo kesi hiyo ilipokuja kwa kutajwa.
Kutokana na taarifa hiyo, ksi hiyo imeahirishwa hadi Juni 5 mwaka huu na kuutaka upande wa mashtaka kukamilisha upelelezi. Mshtakiwa huyo anashtakiwa chini ya kifungu cha 27 (1)(4) cha sheria ya kuzuia na Kupambana na Rushwa namba 11 ya mwaka 2007.
Kimaro anadaiwa kumiliki nyumba zenye thamani ya Sh.1,178,370,334, na magari yenye thamani Sh 307,364,678.20, zisizolingana na kipato chake ambapo anadaiwa ametenda kosa hilo kati ya mwaka 2012 na 2016.
Alidai mshtakiwa akiwa maeneo ya Temeke na mtumishi wa umma wa TPA kama Meneja wa Fedha, amekutwa akimiliki mali zisizolingana na kipato chake halali cha zamani na cha sasa.
Mali hizo ni nyumba mbili zilizopo mtaa wa Uwazi Temeke zenye thamani ya Sh.milioni 124.2, kiwanja kilichopo Yombo Vituka chenye thamani ya Sh.milioni 12.9 . Nyumba mbili zilizopo Temeke zenye thamani ya Sh.milioni 63.5, nyumba tatu zilizopo Temeke zenye thamani ya Sh.milioni 159.
Nyumba nyingine tatu zenye thamani ya Sh.milioni 170.1, nyumba nyingine moja yenye thamani ya Sh.milioni 71.3.kiwanja kilichopo Temeke chenye thamani ya Sh.milioni 35.Pia kiwanja chenye thamani ya Sh.milioni 25 na amejenga nyumba tatu ambazo zinathamani ya Sh.milioni 159 pamoja na nyumba nyingine moja yenye thamani ya Sh.milioni 106.Nyumba zenye thamani ya Sh.milioni 214, nyumba nne eneo la Viziwaziwa Kibaha Mjini zenye thamani ya Sh.milioni 199.7 na nyumba nyingine iliyopo Kilimahewa Tandika yenye thamani ya Sh.milioni 70.
Imedaiwa mahakamani hapo kuwa pia anamiliki magari aina ya Toyota Land cruise lenye thamani ya Sh.milioni 180.1, Mitsubishi lenye thamani ya Sh.milioni 38.4, Massey Ferguson lenye thamani ya Sh.milioni 24 na Trailer lenye thamani ya Sh.milioni 4.5.
Mengine ni Toyota Harrier yenye thamani ya Sh.milioni 35.8, Trailer lenye thamani ya Sh.milioni 4.8, na Massey Ferguson lenye lenye thamani ya Sh.milioni 19.1.
Baada ya kusomewa mashtaka hayo, mshtakiwa huyo alikana shtaka na yupo nje kwa dhamana. Hiyo ni baada ya kukamilisha masharti ya kuwa na wadhamini wawili ambao kila mdhamini awasilishe hati ya mali isiyohamishika yenye thamani ya Sh.milioni 200.
Pia alimtaka mshtakiwa huyo asitoke nje ya mkoa wa Dar es Salaam bila ya kuwa na kibali cha mahakama na mshtakiwa awasilishe hati zake za kisafiria mahakamani.
Hivyo makala UPELELEZI KESI KIGOGO WA TPA ANAYEDAIWA KUJILIMBIKIZA MALI ZA BILIONI 1.4/- BADO HAUJAKAMILIKA, APATA DHAMANA
yaani makala yote UPELELEZI KESI KIGOGO WA TPA ANAYEDAIWA KUJILIMBIKIZA MALI ZA BILIONI 1.4/- BADO HAUJAKAMILIKA, APATA DHAMANA Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala UPELELEZI KESI KIGOGO WA TPA ANAYEDAIWA KUJILIMBIKIZA MALI ZA BILIONI 1.4/- BADO HAUJAKAMILIKA, APATA DHAMANA mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2018/05/upelelezi-kesi-kigogo-wa-tpa-anayedaiwa.html
0 Response to "UPELELEZI KESI KIGOGO WA TPA ANAYEDAIWA KUJILIMBIKIZA MALI ZA BILIONI 1.4/- BADO HAUJAKAMILIKA, APATA DHAMANA"
Post a Comment