TANZANIA YASHIKA NAFASI YA PILI KOMBE LA DUNIA LA WATOTO NCHINI URUSI

TANZANIA YASHIKA NAFASI YA PILI KOMBE LA DUNIA LA WATOTO NCHINI URUSI - Hallo rafiki WORLD MAELEZO LATEST, Katika makala kusoma wakati huu na kichwa TANZANIA YASHIKA NAFASI YA PILI KOMBE LA DUNIA LA WATOTO NCHINI URUSI, tumeandaa vizuri kwa makala hii kusoma na kupakua maelezo humo. pengine kujaza posts makala afya, makala biashara, makala general, makala hobby, makala karibuni info, makala michezo, makala siasa, makala utamaduni, sisi kuandika anaweza kuelewa. Naam, furaha ya kusoma.

title : TANZANIA YASHIKA NAFASI YA PILI KOMBE LA DUNIA LA WATOTO NCHINI URUSI
kiungo : TANZANIA YASHIKA NAFASI YA PILI KOMBE LA DUNIA LA WATOTO NCHINI URUSI

soma pia


TANZANIA YASHIKA NAFASI YA PILI KOMBE LA DUNIA LA WATOTO NCHINI URUSI

Mashindano ya Kombe la dunia la watoto wa mitaani chini ya shirika la Steet Child United na udhaamini wa makampuni na taasisi tofauti, zaidi kampuni ya mawasiliano ya simu ya nchini Urusi, Megafon yamefikia tamati leo kwa kuchezwa mechi za mshindi wa tatu na fainali kwa watoto wa kike na wakiume, ambapo timu ya Tanzania (wasichana) iliweza kuwa mshindi wa pili baada ya kukubali kipigo cha bao 1-0 kutoka Brazil, baada ya kutokea mawasiliano mabaya kati ya mlinzi wa Tanzania na mlinda mlango wake katika hatua za mwisho za mchezo huo.

Mchezo huo ambao ulikuwa ni wa aina yake, huku Brazil wakimiliki mchezo sana na kufanikiwa kumficha kiungo mkuu wa Tanzania, Nahodha Asteria Robert na hapo Tanzania ikawa ishadhibitiwa. Kipindi cha pili Tanzania kidogo walicheza vizuri lakini hawakurudisha goli hilo.
Kipindi cha kwanza Tanzania walicheza kwa presha sana na hawakutulia na mpira na hali hio ikawapotezea kujiamini. Lakini mwisho wa siku asiekubali kushidwa sio mshindani. Tanzania ikashika nafasi ya pili katika mashindano hayo kwa wanawake. 


Mechi hiyo ya fainali ilihudhuriwa na watu wengi mashuhuri, wakiwemo viongozi wa Ubalozi wa Tanzania nchini Urusi pamoja na mchezaji wa zamani wa Arsenal na bingwa wa kombe la dunia kwa kikosi cha Brazil na kiungo maarufu na mwenye uwezo wa viwango vya dunia, Gilberto Da Silva. 
Timu zote baada ya mechi zilipata nafasi ya kumuuliza swali moja Gilberto Da Silva. Tanzania iliuliza swali kupitia Nahodha wake, Asteria Robert kwa Kiswahili na mkalimani Mohamed Masour Nassor akatafsiri moja kwa moja kwa lugha ya Kireno ya mchezaji huyo. Swali hilo lilikua hivi,"Je ni vipi Unawasaidia watoto wa mitaani kufikia ndoto zao na wale watoto ambao wanataka kuwa wachezaji wa viwango vya dunia kama wewe? Mwisho ikafuata sherehe ya ufungaji wa mashindano hayo. 

Muda wa zawadi ulipofika, Tanzania ilizawadiwa Kombe na medali za shaba kwa kila mchezaji na viongozi wa timu kutoka chama cha mpira cha Urusi na zawadi zengine kutoka kwa chuo cha Patrice Lumumba. Tanzania pia ilitoa kiungo bora wa mashindano ambae ni nahodha, Asteria Robert ambae kwa kweli alistahili sana. Kwa upande wa bingwa wa wanaume ni Timu  ya Uzbekistan baada ya kuilaza kwa mikwaju ya penati timu ya Pakistan.
 Kwa upande wa zawadi zengine, Mlinda Mlango bora alitoka Uingereza kwa wanawake, kwa wanaume alitoka Indonezia, Mfungaji bora kwa wanawake alitoka Brazil, mlinzi bora kwa wanawake alitoka Ufilipino, mlinzi bora kwa wanaume alitoka Uzbekistan, mchezaji bora kwa wanaume alitoka Pakistan, mchezaji bora kwa wanawake alitoka Brazil na wengine. 
Tanzania kwa ujumla imeweka rikodi nzuri pia kwa kuwa  mshindi wa pili mwaka huu kwa wanawake. Mwaka 2014 Tanzania ilikua bingwa wa mashindano haya kwa wanaume huko mjini Rio di Jeneiro, Brazil na mwaka 2010 Tanzania iliishia nusu fainali huko Afrika ya Kusini kwa upande wa wanaume. Nafikiri mwaka 2022 nchini Qatar, Tanzania kwa wanawake itafanya vizuri zaidi. Nchi zilizoshiriki ni 21 na timu zikiwa ni 24.  imeandikwa na Mohamed Mansour Nassor, SOYUZ Alumni Association of Tanzania


Hivyo makala TANZANIA YASHIKA NAFASI YA PILI KOMBE LA DUNIA LA WATOTO NCHINI URUSI

yaani makala yote TANZANIA YASHIKA NAFASI YA PILI KOMBE LA DUNIA LA WATOTO NCHINI URUSI Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.

Wewe ni sasa kusoma makala TANZANIA YASHIKA NAFASI YA PILI KOMBE LA DUNIA LA WATOTO NCHINI URUSI mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2018/05/tanzania-yashika-nafasi-ya-pili-kombe.html

Subscribe to receive free email updates:

0 Response to "TANZANIA YASHIKA NAFASI YA PILI KOMBE LA DUNIA LA WATOTO NCHINI URUSI"

Post a Comment