title : TANAPA WAMKABIDHI MNYETI ZAHANATI YA GIJEDABUNG
kiungo : TANAPA WAMKABIDHI MNYETI ZAHANATI YA GIJEDABUNG
TANAPA WAMKABIDHI MNYETI ZAHANATI YA GIJEDABUNG
SHIRIKA la hifadhi za Taifa nchini ( TANAPA ) limemkabidhi Mkuu wa Mkoa wa Manyara, Alexander Mnyeti, zahanati itakayowasaidia wananchi wa Kiijiji cha Gijedabung kata ya Endakiso Wilbayani Babati, kupata huduma ya afya hivyo kuondokana na adha ya kutembea umbali mrefu wa kilomita 15 kufuata huduma hiyo eneo la Endakiso.
Akizungumza kwa niaba ya Mkurugenzi mkuu wa TANAPA, Allan Kijazi, Meneja wa ujirani mwema Ahmed Mbugi wakati akimkabidhi mkuu huyo wa Mkoa alisema ujenzi wa jengo la zahati hiyo hilo ni wakati wa makabidhiano ya zahanati hiyo ni ushirikiano kati ya hifadhi za Taifa Tanzania kupitia hifadhi ya Tarangire na wananchi wa kijiji cha Gijedabung.
Mbugi alisema Halmashauri ya wilaya ya Babati chini ya mkurugenzi wake Hamis Malinga ni miongoni mwa wilaya nne zinazopakana na Hifadhi ya Taifa ya Tarangire, ambapo wamekua wakishirikiana katika mambo mbalimbali yakiwemo ya uhifadhi wa maliasili na mazingira pamoja na maendeleo ya wananchi.
"Naomba nikujulishe kwamba mpango wa ujirani mwema katika shirika la hifadhi za Taifa Tanzania kuwa ulianzishwa mwaka 1988 katika hifadhi ya Taifa Serengeti kama mradi wa majaribio ukiwa na malengo makuu manne, moja kuweza na kuanzisha uhusiano mzuri kati ya hifadhi na jamii inayoizunguka, pili kuwezesha mpango wa kufikisha Faida za uhifadhi kwa jamii kwa urahisi zaidi, tatu kusaidia jamii kuweza kupata elimu ya uhifadhi kwanjia rahisi, nne kubuni mpango wa kitaalam wa ushirikishwaji wadau wote wa uhifadhi kwa pamoja," alisema Mbugi.
Mkuu wa Mkoa wa Manyara, Alexander Mnyeti akipanda mti kwenye eneo la zahanati ya Kijiji cha Gijedabung Wilayani Babati Mkoani Manyara, iliyojengwa kwa shirilingi milioni 83 ambpo shirika la hifadhi za Taifa (TANAPA) imechangia shilingi milioni 65 na nguvu za wananchi wa eneo hilo shilingi milioni 18.
Mbunge wa viti maalum wa Mkoa wa Manyara, Esta Mahawe akipongezwa na Mkuu wa Mkoa huo Alexander Mnyeti na viongozi wengine wa Wilaya ya Babati, baada ya mbunge huyo kumkabidhi mkuu huyo wa mkoa mashuka 10 yatakayotumika kwenye zahanati ya kijiji cha Gijedabung iliyozinduliwa na Mnyeti.
Meneja ujirani mwema wa shirika la hifadhi za Taifa (TANAPA) Ahmed Mbugi, akisoma kwa niaba ya Mkurugenzi Mkuu wa TANAPA, Allan Kijazi, taarifa ya ujenzi wa zahanati ya Kijiji cha Gijedabung kwa Mkuu wa Mkoa wa Manyara, Alexander Mnyeti, ambapo TANAPA ilitumia shilingi milioni 65 kujenga zahanati hiyo na nguvu za wananchi zikathaminishwa kwa shilingi milioni 18 hivyo jumla kutumika kiasi cha shilingi milioni 83 hadi kukamilika kwake.
Kikundi cha ngoma cha Kijiji cha Gijedabung Wilayani Babati Mkoani Manyara, wakicheza ngoma wakati shirika la hifadhi za Taifa (TANAPA) lilipokabidhi zahanati ya kijiji hicho kwa Mkuu wa Mkoa huo Alexander Mnyeti.
Mkuu wa Mkoa wa Manyara, Alexander Mnyeti akimkabidhi Mkuu wa hifadhi ya Taifa ya Tarangire, Herman Batiho cheti cha kutambua mchango wake wa kusimamia maendeleo baada ya TANAPA kumkabidhi zahanati waliyojenga kwenye Kijiji cha Gijedabung Wilayani Babati.
KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA
KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA
Hivyo makala TANAPA WAMKABIDHI MNYETI ZAHANATI YA GIJEDABUNG
yaani makala yote TANAPA WAMKABIDHI MNYETI ZAHANATI YA GIJEDABUNG Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala TANAPA WAMKABIDHI MNYETI ZAHANATI YA GIJEDABUNG mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2018/05/tanapa-wamkabidhi-mnyeti-zahanati-ya.html
0 Response to "TANAPA WAMKABIDHI MNYETI ZAHANATI YA GIJEDABUNG"
Post a Comment