STARTIMES KUONESHA,KUTANGAZA KOMBE LA DUNIA KWA KISWAHILI

STARTIMES KUONESHA,KUTANGAZA KOMBE LA DUNIA KWA KISWAHILI - Hallo rafiki WORLD MAELEZO LATEST, Katika makala kusoma wakati huu na kichwa STARTIMES KUONESHA,KUTANGAZA KOMBE LA DUNIA KWA KISWAHILI, tumeandaa vizuri kwa makala hii kusoma na kupakua maelezo humo. pengine kujaza posts makala afya, makala biashara, makala general, makala hobby, makala karibuni info, makala michezo, makala siasa, makala utamaduni, sisi kuandika anaweza kuelewa. Naam, furaha ya kusoma.

title : STARTIMES KUONESHA,KUTANGAZA KOMBE LA DUNIA KWA KISWAHILI
kiungo : STARTIMES KUONESHA,KUTANGAZA KOMBE LA DUNIA KWA KISWAHILI

soma pia


STARTIMES KUONESHA,KUTANGAZA KOMBE LA DUNIA KWA KISWAHILI

*Kutumia lugha ya Kiswahili katika kuutangaza

Na Ripota Wetu, Globu ya jamii
KAMPUNI ya Star Media (T) Ltd yenye chapa ya StarTimes imetangaza rasmi kurusha matangazo ya Kombe la Dunia Urusi mwaka 2018 Mubashara kupitia king’amuzi chake. StarTimes imethibitisha kuonesha michuano hiyo leo katika hafla fupi iliyofanyika Terrace, Slipway Masaki jijini Dar es Salaam na kushirikisha waandishi wa Habari pamoja na wadau mbalimbali wa soka nchini.

Akizungumza katika uzinduzi huo, Meneja Masoko wa Kampuni hiyo David Malisa amesema “Mwaka huu katika Kombe la Dunia la 21, StarTimes ni mrushaji rasmi wa michuano hiyo itakayoanza Juni 14 hadi Julai 15 nchini Urusi. Mechi zote 64 zitakazochezwa Urusi katika Kombe la Dunia zitarushwa moja kwa moja.

" Amefafanua mbali na kurusha tu michuano hiyo maarufu zaidi Duniani, StarTimes watarusha matangazo ya michezo yote katika lugha ya Kiswahili na hiyo ni katika jitihada za kuienzi na kuikuza   lugha ya Kiswahili lugha ambayo ni maarufu zaidi katika ukanda huu wa Afrika Mashariki.

“StarTimes tutarusha matangazo ya Kombe la Dunia, mechi zote 64 katika lugha ya Kiswahili pamoja na uchambuzi utakaoambatana na mechi hizo, uchambuzi utakaofanywa na wachambuzi mahiri na tuliowazoea hapa nchini”, ameongeza David.

Sambamba na kuzindua Kombe la Dunia, StarTimes pia wametangaza ofa kwa wapenzi wa soka, ambapo wateja watakaonunua king’amuzi au Luninga zao za kidigitali kati sasa na Juni 30 watapatiwa kifurushi cha juu hadi Julai 31 mwaka huu bure.
Meneja masoko wa Kampuni ya Startimes, David Malisa akizungumza na waandishi wa habari pamoja na wageni waalikwa wakati wa uzinduzi wa kurusha matangazo ya Kombe la Dunia Urusi 2018 kwa kutumia lugha ya Kiswahili kwenye king'amuzi cha Startimes.
Mkuu wa Kitengo cha Maudhui ya Startimes, Zamarad Nzowa akizungumzia namna walivyojipanga wakishirikiana na wasanii mbalimbali wa hapa nchini kwenye msimu wa kombe la Dunia litakalochezwa nchini Urusi hasa kwenye vipindi mbalimbali  vitakavyokuwa vinarushwa kupitia kwenye king'amuzi cha Startimes.
Mkuu wa kitengo cha Mawasiliano wa Shirika la utangazaji nchini Tanzania (TBC), Edna Rajab akizungumza na waandishi wa habari pamoja na wageni mbalimbali waliofika katika uzinduzi wa kurusha matangazo ya Kombe la Dunia Urusi 2018 kwa kutumia lugha ya Kiswahili kwenye king'amuzi cha Startimes.
Balozi wa Startimes Tanzania kwenye msimu wa Kombe la Dunia na Msanii wa Bongo Movies, Wema Sepetu akizungumzia namna walivyojipanga na wasanii wenzake wakati wa kipindi chote cha Kombe la dunia wakishirikiana na Startimes Tanzania.
Mchambuzi wa Michezo, Jeff Leya akizungumzia fulsa aliyoipata mara baada kuingia mkataba na Startimes kuchambua mpira kwenye kombe la dunia kupitia king'amuzi cha Startimes.
Mkurugenziwa Startimes Tanzania, Wang Xiaobo akipiga mpira golini kuashiria kufunguliwa kwa uzinduzi wa kurusha matangazo ya Kombe la Dunia Urusi 2018 kwa kutumia lugha ya Kiswahili kwenye king'amuzi cha Startimes.
Baadhi ya waandishi wa habari pamoja na waalikwa
Viongozi wa Startimes wakiwa kwenye picha ya pamoja na wasanii wakati wa wa uzinduzi wa kurusha matangazo ya Kombe la Dunia Urusi 2018 kwa kutumia lugha ya Kiswahili kwenye king'amuzi cha Startimes kwenye ukumbi wa Hotel ya Slip Way jijini Dar es Salaam.


Hivyo makala STARTIMES KUONESHA,KUTANGAZA KOMBE LA DUNIA KWA KISWAHILI

yaani makala yote STARTIMES KUONESHA,KUTANGAZA KOMBE LA DUNIA KWA KISWAHILI Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.

Wewe ni sasa kusoma makala STARTIMES KUONESHA,KUTANGAZA KOMBE LA DUNIA KWA KISWAHILI mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2018/05/startimes-kuoneshakutangaza-kombe-la.html

Subscribe to receive free email updates:

0 Response to "STARTIMES KUONESHA,KUTANGAZA KOMBE LA DUNIA KWA KISWAHILI"

Post a Comment