title : STANBIC FC YAISULUBU TRAVEL PARTNER FC WAKISHEREKEA SHEREHE ZA MEI MOSI
kiungo : STANBIC FC YAISULUBU TRAVEL PARTNER FC WAKISHEREKEA SHEREHE ZA MEI MOSI
STANBIC FC YAISULUBU TRAVEL PARTNER FC WAKISHEREKEA SHEREHE ZA MEI MOSI
Na Leandra Gabriel, Blogu ya jamii
KATIKA Maadhimisho ya siku ya wafanyakazi duniani (Mei Mosi) benki ya Stanbic sambamba na wadau wao wakubwa Travel Partner wamesherekea kwa kucheza kandanda katika viwanja vya
Don Bosco Oysterbay jijini Dar es salaam.
Katika mtanange huu Stanbic Fc walimaliza kwa kutoka kifua mbele kwa mabao 9 na Travel Partner wakiambulia bao 1 pekee lililofungwa kipindi cha pili na James Malola.Akizungumza na Michuzi blog, Mkurugenzi Mkuu wa Travel Partner Erick Mashauri amesema wameamua kusheherekea Mei Mosi kwa namna hiyo ili kujenga mahusiano ya kikazi, kufurahi na kujenga mwili.
Licha ya kupoteza mchezo huo Mashauri ameeleza sababu za kushindwa kwao ni kutokana na uchanga wa timu na amehaidi watafanya mazoezi ili kuwapiku vinara hao.
Pia Mashauri amewaomba wafanyakazi wengine kutumia siku hiyo kusherekea kwa namna mbalimbali zinazolenga kujenga,
kushirikiana na kubadilishana mawazo katika kazi zao.Kiongozi wa Timu ya Stanbic William Kimaro ameeleza siri ya ushindi huo ni mazoezi ya kutosha na kufafanua mchezo huo umewafanya waendelee kudumisha uhusiano na kampuni hiyo.
Aidha James Malola aliyeipatia bao pekee Travel Partner amesema licha ya kupoteza mchezo bado wana nguvu katika mechi zinazofuata na kukiri mazoezi makali ya Stanbic Fc ndio yaliruhusu magoli 9 wavuni.
Mkurugenzi mkuu wa Travel partner, Erick Mashauri akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kumalizika kwa mechi hiyo.
Kikosi cha timu ya Stanbic Fc kilichocheza na na Travel partner katika kusherekea siku ya Mei mosi.
Mechi baina ya Stanbic Fc Dhidi ya Travel partner ikiendelea katika viwanja vya Oysterbay jijini Dar es salaam.(picha zote na Emmanuel Massaka,Globu ya jamii)
Kocha wa Travel partner Aziz Chonya akizungumza na wachezaji wake mara baada ya kipindi cha kwanza kumalizika.
Hivyo makala STANBIC FC YAISULUBU TRAVEL PARTNER FC WAKISHEREKEA SHEREHE ZA MEI MOSI
yaani makala yote STANBIC FC YAISULUBU TRAVEL PARTNER FC WAKISHEREKEA SHEREHE ZA MEI MOSI Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala STANBIC FC YAISULUBU TRAVEL PARTNER FC WAKISHEREKEA SHEREHE ZA MEI MOSI mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2018/05/stanbic-fc-yaisulubu-travel-partner-fc.html
0 Response to "STANBIC FC YAISULUBU TRAVEL PARTNER FC WAKISHEREKEA SHEREHE ZA MEI MOSI"
Post a Comment