title : NGORONGORO HEROES KUVAANA NA MALI MEI 12 MWAKA HUU
kiungo : NGORONGORO HEROES KUVAANA NA MALI MEI 12 MWAKA HUU
NGORONGORO HEROES KUVAANA NA MALI MEI 12 MWAKA HUU
Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii
TIMU ya Taifa ya chini ya miaka 20 Ngorongoro Heroes inashuka dimbani Mei 12 mwaka huu kuvaana na kikosi cha Timu ya Mali utakaofanyika Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.
Ngorongoro Heroes walifanikiwa kuwaondoa timu ya vijana ya Congo DR kwa mikwaju ya Penati baada ya kutoka sare ya 1-1 hapa jijini Dar es salaam na 0-0 nchini Congo kwenye mchezo wa kutafuta tiketi ya kucheza fainali za Vijana za Africa zitakazochezwa Niger mwezi Novemba
Akizungumza kuelekea mtanange huo Ofisa Habari wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Nchini.(TFF) Clifford Ndimbo amesema mchezo huo utakaoanza majira ya saa 10 alasir utakuwa ni kwa ajili ya kufuzu kwenda katika fainali za Vijana za Africa zitakazochezwa Niger mwezi Novemba.
Ndimbo amesema timu hiyo ambayo tayari ipo kambini kujiandaa na mchezo huo muhimu na tayari benchi la ufundi limeanza mikakati ya kuhakikisha wanatoka na ushindi ili kuweza kuvuka hatua inayofuata.
Viingilio vya michezo hiyo ni Sh.3000 kwa VIP na mzunguko ikiwa ni Sh.1000 Ngorongoro Heroes inatakiwa kuhakikisha wanatoka na ushindi nyumbani ili mchezo wa marudiano usiwe mgumu kwa upande wao.
TIMU ya Taifa ya chini ya miaka 20 Ngorongoro Heroes
Hivyo makala NGORONGORO HEROES KUVAANA NA MALI MEI 12 MWAKA HUU
yaani makala yote NGORONGORO HEROES KUVAANA NA MALI MEI 12 MWAKA HUU Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala NGORONGORO HEROES KUVAANA NA MALI MEI 12 MWAKA HUU mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2018/05/ngorongoro-heroes-kuvaana-na-mali-mei.html
0 Response to "NGORONGORO HEROES KUVAANA NA MALI MEI 12 MWAKA HUU"
Post a Comment