title : SERIKALI YAKUTANA NA WADAU WA MAENDELEO KUJADILI MASUALA YA KIJINSIA
kiungo : SERIKALI YAKUTANA NA WADAU WA MAENDELEO KUJADILI MASUALA YA KIJINSIA
SERIKALI YAKUTANA NA WADAU WA MAENDELEO KUJADILI MASUALA YA KIJINSIA
Serikali imekutana na wadau wa Maendeleo Jijini Dar es Salaam kujadiliana kuhusu utekelezaji wa Sera na Mipango ya kitaifa inayohusu masuala ya jinsia ikiwemo Mpango wa Kitaifa wa Kutokomeza vitendo vya Ukatili dhidi ya Wanawake na Watoto (2017/18 – 2021/22); utekelezaji wa mikataba ya kikanda na kimataifa kuhusu kufikia usawa wa kijinsia na uwezeshaji wa Wanawake kiuchumi.
Akizungumza katika kikao kati ya Serikali na wadau hao Katibu Mkuu Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Sihaba Nkinga amesema Serikali imeamua kukutana na wadau ili kujadiliana na kupata maoni kuhusu utekelezaji wa Sera Mipango na mikakati ya Serikali katika masuala ya kijinsia ili kuweza kutekeleza kwa mafanikio masuala hayo.
Ameongeza kuwa Serikali inashirikiana na wadau wa Maendeleo kwa karibu ili kuwa na Mipango na mikakati ya pamoja ya kutekeleza masuala mbalimbali ya kijinsia ikiwemo kutokomeza vitendo vya Ukatili dhidi ya Wanawake na Watoto na uwezeshaji wa Wanawake kiuchumi.
"Ni jambo la busara kuwashirikisha wadau wa Maendeleo katika masuala ya kimaendeleo ili kupeleke mbele kurudumu la maendeleo" alisisitiza Bi. Sihaba.
Katibu Mkuu Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Sihaba Nkinga akizungumza na wadau wa Maendeleo Jijini Dar es Slaam wakati wa majadiliano kuhusu utekelezaji wa Sera na mipango ya kitaifa inayohusu masuala ya jinsia ikiwemo Mpango wa Kitaifa wa Kutokomeza Vitendo vya Ukatili dhidi ya Wanawake na Watoto (2017/18 – 2021/22); utekelezaji wa mikataba ya kimataifa kuhusu kufikia usawa wa kijinsia na uwezeshaji wa wanawake kiuchumi. Kulia ni Mwakilishi wa UN Women nchini Bi. Susan Steffen.
Mwakilishi wa UN Women nchini Bi Susan Steffen akielezea Mipango ya Umoja wa Mataifa katika kuwezesha masuala ya Kijinsia na uwezeshaji wa wanawake kiuchumi wakati wa kikao kati ya Serikali na wadau wa Maendeleo Jijini Dar es Slaam kujadiliana kuhusu utekelezaji wa Sera na mipango ya kitaifa inayohusu masuala ya jinsia ikiwemo Mpango wa Kitaifa wa Kutokomeza vitendo vya Ukatili dhidi ya Wanawake na Watoto (2017/18 – 2021/22) ; utekelezaji wa mikataba ya kikanda na kimataifa kuhusu kufikia usawa wa kijinsia na uwezeshaji wa wanawake kiuchumi. Kushoto ni Katibu Mkuu Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Bi. Sihaba Nkinga.
Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Sera na Mipango Bw. Atupele Mwambene akielezea kuhusu utekelezaji wa Mipango wa Kitaifa wa Kutokomeza Ukatili dhidi ya Wanawake na Watoto (2017/18 – 2021/22) (NPA) katika kikao kati ya Serikali na wadau kujadiliana kuhusu utekelezaji wa Sera na mipango ya kitaifa inayohusu masuala ya jinsia ikiwemo Mpango wa Kitaifa wa Kutokomeza vitendo vya Ukatili dhidi ya Wanawake na Watoto (2017/18 – 2021/22) ; utekelezaji wa mikataba ya kikanda na kimataifa kuhusu kufikia usawa wa kijinsia na uwezeshaji wa Wanawake kiuchumi.
Afisa Maendeleo ya Jamii kutoka Idara ya Maendeleo ya Jinsia Bi.Dorah Neema akielezea kuhusu masuala ya Kamisheni ya hali ya Wanawake (CWS) katika kikao kati ya Serikali na wadau kuhusu utekelezaji wa Sera na mipango ya kitaifa inayohusu masuala ya jinsia ikiwemo Mpango wa Kitaifa wa Kutokomeza vitendo vya Ukatili dhidi ya Wanawake na Watoto (2017/18 – 2021/22) , utekelezaji wa mikataba ya kimataifa kuhusu kufikia usawa wa kijinsia na uwezeshaji wa Wanawake kiuchumi.
KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA
KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA
Hivyo makala SERIKALI YAKUTANA NA WADAU WA MAENDELEO KUJADILI MASUALA YA KIJINSIA
yaani makala yote SERIKALI YAKUTANA NA WADAU WA MAENDELEO KUJADILI MASUALA YA KIJINSIA Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala SERIKALI YAKUTANA NA WADAU WA MAENDELEO KUJADILI MASUALA YA KIJINSIA mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2018/05/serikali-yakutana-na-wadau-wa-maendeleo.html
0 Response to "SERIKALI YAKUTANA NA WADAU WA MAENDELEO KUJADILI MASUALA YA KIJINSIA"
Post a Comment