title : SERIKALI KUTENGA KILA MWEZI MILIONI 55 KWA JIJI LA TANGA KUHAKIKISHA WANAFUNZI WA SHULE ZA MSINGI WANAPATA ELIMU BORA-WAZIRI UMMY
kiungo : SERIKALI KUTENGA KILA MWEZI MILIONI 55 KWA JIJI LA TANGA KUHAKIKISHA WANAFUNZI WA SHULE ZA MSINGI WANAPATA ELIMU BORA-WAZIRI UMMY
SERIKALI KUTENGA KILA MWEZI MILIONI 55 KWA JIJI LA TANGA KUHAKIKISHA WANAFUNZI WA SHULE ZA MSINGI WANAPATA ELIMU BORA-WAZIRI UMMY
WAZIRI wa Afya,Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto,Ummy Mwalimu amesema serikali kila mwezi imekuwa ikitenga fedha kiasi cha sh.milioni 55 kwenye Jiji la Tanga kwa ajili ya shule za msingi ili kuhakikisha wanafunzi wanasoma bila kuwepo kwa vikwazo na hivyo kupata elimu bora.
Aliyasema hayo wakati ufunguzi na kukabidhi vyumba vya madarasa 11 kwenye shule ya Msingi Bombo kwa halmashauri ya Jiji hilo ambavyo ujenzi wake ulichukua zaidi ya mwaka mmoja na kulazimika wanafunzi kuwepo nje ya madarasa yaliyogharimu kiasi cha zaidi ya Milioni 279 zilizotokana na mapato ya ndani.
Ndani ya kipindi hicho wanafunzi hao walilazimika kuhamia kwenye shule ya Msingi Mkwakwani jambo ambalo lilisababisha msongamano mkubwa ambao uliathiri kwa kiasi kikubwa taaluma.
Waziri Ummy ambaye pia ni Mbunge wa Viti Maalumu (CCM) Mkoa wa Tanga alisema licha ya hivyo lakini pia serikali imekuwa ikitenga fedha kiasi cha sh.milioni 108 kwa ajili ya shule za Sekondari kwenye Jiji hilo ili kuhakikisha wanaweza kukabiliana na changamoto ambazo zinawakabili kupitia sekta hiyo.
“Ndugu zangu ninafuraha sana leo baada ya kufungua madarasa haya ambayo yamejengwa kwa kiwango kizuri na yatawawezesha wanafunzi kusoma bila kuwepo kwa vikwazo lakini pia kupitia sera ya Rais elimu bure serikali inaleta milioni 55 kila mwezi kusaidia elimu kwa watoto wetu kwenye shule za msingi pia nahaidi kushirikiana nanyi”Alisema.
Hivyo makala SERIKALI KUTENGA KILA MWEZI MILIONI 55 KWA JIJI LA TANGA KUHAKIKISHA WANAFUNZI WA SHULE ZA MSINGI WANAPATA ELIMU BORA-WAZIRI UMMY
yaani makala yote SERIKALI KUTENGA KILA MWEZI MILIONI 55 KWA JIJI LA TANGA KUHAKIKISHA WANAFUNZI WA SHULE ZA MSINGI WANAPATA ELIMU BORA-WAZIRI UMMY Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala SERIKALI KUTENGA KILA MWEZI MILIONI 55 KWA JIJI LA TANGA KUHAKIKISHA WANAFUNZI WA SHULE ZA MSINGI WANAPATA ELIMU BORA-WAZIRI UMMY mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2018/05/serikali-kutenga-kila-mwezi-milioni-55.html
0 Response to "SERIKALI KUTENGA KILA MWEZI MILIONI 55 KWA JIJI LA TANGA KUHAKIKISHA WANAFUNZI WA SHULE ZA MSINGI WANAPATA ELIMU BORA-WAZIRI UMMY"
Post a Comment