NBS Kukusanya Takwimu Kwa Njia ya Satelaiti na Vishikwambi

NBS Kukusanya Takwimu Kwa Njia ya Satelaiti na Vishikwambi - Hallo rafiki WORLD MAELEZO LATEST, Katika makala kusoma wakati huu na kichwa NBS Kukusanya Takwimu Kwa Njia ya Satelaiti na Vishikwambi, tumeandaa vizuri kwa makala hii kusoma na kupakua maelezo humo. pengine kujaza posts makala afya, makala biashara, makala general, makala hobby, makala karibuni info, makala michezo, makala siasa, makala utamaduni, sisi kuandika anaweza kuelewa. Naam, furaha ya kusoma.

title : NBS Kukusanya Takwimu Kwa Njia ya Satelaiti na Vishikwambi
kiungo : NBS Kukusanya Takwimu Kwa Njia ya Satelaiti na Vishikwambi

soma pia


NBS Kukusanya Takwimu Kwa Njia ya Satelaiti na Vishikwambi

Na Beatrice Lyimo- MAELEZO, Dodoma
Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS) imeanzisha mfumo wa ukusanyaji wa taarifa kwa kutumia teknolojia mpya na ya kisasa ya kielektroniki kwa njia ya satelaiti  na Vishikwambi.
Akizungumza na waandishi wa habari leo mkoani Dodoma mrasimu ramani mwandamizi na msimamizi wa Sehemu ya mfumo wa Ukusanyaji na Usambazaji wa taarifa za Kijiografia (GIS) Benedict Mgambi amesema kuwa lengo la mfumo huo ni kuboresha ukusanyaji wa  taarifa na tafiti mbalimbali   kwa ajili ya maendeleo ya nchi.
Mgambi amesema kuwa teknolojia hii mpya imerahisisha kwa kiasi kikubwa ufanyaji kazi ikilinganishwa na taratibu zilizokuwa zikitumika awali.
“Awali tulikuwa tunatumia teknolojia ya duni ambapo mchakato wake ulihusisha watu wengi, gharama kubwa ila kwa sasa hivi kila kitu kinafanyika eneo husika la tafiti na kutumwa moja kwa moja makao makuu” amesema Mgambi
Aidha Mgambi amesema kuwa zoezi hilo limeshirikisha wadau mbalimbali ikiwemo, TAMISEMI, Wizara ya Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi ,Wizara ya Maliasili na utalii pamoja na TAMISEMI.
Kwa upande wake Mtaalamu wa Masuala ya Kijiografia (NBS) Martha Macha amesema kuwa mfumo huo umerahisisha utendaji kazi wao kwani unasaidia kutambua mipaka mbalimbali kati ya kitongoji kimoja na kingine.
“Vifaa hivi vinafanya kazi kubwa kwa muda mfupi na pia vinafanya kazi kwa ubora ule unaohitajika kwa kuona vielelezo mbalimbali vitakavyokuwezesha kufanya kazi kwa urahisi” amefafanu Bi. Macha.
Mpaka sasa vijii vitano vya Sasajila, Suli, Fufu, Champumba na Chiboli Wilaya ya Chamwino Mkoa wa Dodoma vimefanyiwa majaribio ya mfumo huo.
Mrasimu ramani Mwandamizi   kutoka Ofisi ya Taifa ya Takwimu Bw. Benedict Mgambi akieleza kwa waandishi wa habari  faida za kutumia mfumo wa ukusanyaji na usambazaji wa taarifa za kijiografia  wakati wa ziara yao iliyonga kujionea jinsi Ofisi ya hiyo inavyotekeleza majukumu yake katika ukusanyaji wa taarifa mbalimbali ikiwemo sense na tafiti zinazofanywa kwa kutumia mfumo huo wa kisasa.
Mtaalamu wa masuala ya Jiografia kutoka Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS) Matha Macha  akitoa maelezo kuhusu namna mfumo huo unavyofanya kazi.
Mrasimu ramani msaidizi kutoka Ofisi ya Taifa ya Takwimu Bw. Rahim  Mussa  akisisitiza kuhusu namna mfumo huo unavyochochea maendeleo.
Mrasimu ramani Mwandamizi   kutoka Ofisi ya Taifa ya Takwimu Bw. Benedict Mgambi  akiongoza ujumbe kutoka Ofisi ya Taifa ya Takwimu kutembelea  kijiji cha  Sasa Wilaya ya Chamwino ambapo  ujumbe huo umeambatana na waandishi wa habari kujionea mfumo wa ukusanyaji na usambazaji wa taarifa za kijiografia  wakati wa ziara yao iliyonga kujionea jinsi Ofisi ya hiyo inavyotekeleza majukumu yake katika ukusanyaji wa taarifa mbalimbali ikiwemo sense na tafiti zinazofanywa kwa kutumia mfumo huo wa kisasa.
Mwenyekiti   wa  kijiji cha  Sasa Wilaya ya Chamwino ambapo ni ujumbe wa NBS  na waandishi wa habari walitembelea  kujionea jinsi  mfumo wa ukusanyaji na usambazaji wa taarifa za kijiografia  wakati wa ziara yao iliyonga kujionea jinsi Ofisi ya hiyo inavyotekeleza majukumu yake katika ukusanyaji wa taarifa mbalimbali ikiwemo sense na tafiti zinazofanywa kwa kutumia mfumo huo wa kisasa. (Picha zote na Frank Mvungi- MAELEZO)


Hivyo makala NBS Kukusanya Takwimu Kwa Njia ya Satelaiti na Vishikwambi

yaani makala yote NBS Kukusanya Takwimu Kwa Njia ya Satelaiti na Vishikwambi Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.

Wewe ni sasa kusoma makala NBS Kukusanya Takwimu Kwa Njia ya Satelaiti na Vishikwambi mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2018/05/nbs-kukusanya-takwimu-kwa-njia-ya.html

Subscribe to receive free email updates:

0 Response to "NBS Kukusanya Takwimu Kwa Njia ya Satelaiti na Vishikwambi"

Post a Comment