title : MUHIMBILI KUFUNGA MASHINE YA KUDHIBITI TAKA HATARISHI
kiungo : MUHIMBILI KUFUNGA MASHINE YA KUDHIBITI TAKA HATARISHI
MUHIMBILI KUFUNGA MASHINE YA KUDHIBITI TAKA HATARISHI
Hospitali ya Taifa Muhimbili inatarajia kufunga mashine ya kisasa ya utasishaji taka ambayo itapunguza uchomaji wa taka za plastiki ambazo zina madhara kwa binadamu Mashine hiyo yenye thamani ya Dola Laki moja imetolewa na Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Maendeleo (UNDP) hivyo Hospitali ya Taifa Muhimbili itakua hospitali ya kwanza ya Umma kuwa na mashine hiyo.
Akizungumza mara baada ya kupokea ugeni kutoka UNDP ambao umekuja kwa lengo la kukagua utekelezwaji wa mradi wa mazingira , Mkuu wa Idara ya Mazingira MNH Muhandisi Veilla Matee amesema mashine hiyo itafungwa wiki hii na wiki ijayo itaanza kufanya kazi na kutoa fursa kwa kampuni mbalimbali kuja kununua malighafi ambayo hutumika kutengeneza vifaa vya plastiki. ‘’ Tumepokea mashine ya utasishaji kutoka UNDP na mara baada ya kufungwa mashine hiyo tutatoa mafunzo maalum ya kuwajengea uwezo watendaji wetu ili waweze kufanya kazi kwa ufanisi, mbali na kupewa mashine hiyo ya kisasa pia UNDP wametupatia vitendea kazi mbalimbali vya kuhifadhi taka ambavyo vitatusaidia sana katika mradi huu ’’amefafanua Injinia Matee.
Hospitalia ya Taifa Muhimbili kwa siku huzalisha taka hatarishi kilo 800 kutokana na idadi kubwa ya wagonjwa inayowahudumia . Mradi huo wa mazingira unasimamiwa na Idara ya Mazingira kwa kushirikiana na Kitengo cha Uhakiki na Ubora Muhimbili.
Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) Prof. Lawrence Museru akizungumza na ujumbe kutoka Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Maendeleo (UNDP) ambao umekuja kuangalia utekelezwaji wa mradi wa mazingira . UNDP wametoa msaada wa mashine ya kisasa ya utasishaji ambayo itasaidia kupunguza uchomaji wa taka za plastiki.
Taka 02: Mkuu wa Idara ya Mazingira Muhandisi Veilla Matee akiwasilisha mada kuhusu uzalishaji wa taka Muhimbili kwa wadau mbalimbali wa mazingira ambao wameambatana na ujumbe kutoka UNDP .
Mkuu wa Idara ya Mazingira Muhandisi Veilla Matee akiwasilisha mada kuhusu uzalishaji wa taka Muhimbili kwa wadau mbalimbali wa mazingira ambao wameambatana na ujumbe kutoka UNDP .
Wadau hao wakimsilikiza Muhandisi Matee alipokua akifafanua jambo wakati wa tukio hilo.
Mshauri wa masuala ya Mazingira kutoka UNDP Zambia Bi. Winnie Musonda akiuliza swali mara baada ya kuwasilishwa kwa mada hiyo mapema leo katika Hospitali ya Taifa Muhimbili.
Hivyo makala MUHIMBILI KUFUNGA MASHINE YA KUDHIBITI TAKA HATARISHI
yaani makala yote MUHIMBILI KUFUNGA MASHINE YA KUDHIBITI TAKA HATARISHI Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala MUHIMBILI KUFUNGA MASHINE YA KUDHIBITI TAKA HATARISHI mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2018/05/muhimbili-kufunga-mashine-ya-kudhibiti.html
0 Response to "MUHIMBILI KUFUNGA MASHINE YA KUDHIBITI TAKA HATARISHI"
Post a Comment