Mkuu wa Mkoa Mwanza akagua maghala ya ununuzi wa pamba

Mkuu wa Mkoa Mwanza akagua maghala ya ununuzi wa pamba - Hallo rafiki WORLD MAELEZO LATEST, Katika makala kusoma wakati huu na kichwa Mkuu wa Mkoa Mwanza akagua maghala ya ununuzi wa pamba, tumeandaa vizuri kwa makala hii kusoma na kupakua maelezo humo. pengine kujaza posts makala afya, makala biashara, makala general, makala hobby, makala karibuni info, makala michezo, makala siasa, makala utamaduni, sisi kuandika anaweza kuelewa. Naam, furaha ya kusoma.

title : Mkuu wa Mkoa Mwanza akagua maghala ya ununuzi wa pamba
kiungo : Mkuu wa Mkoa Mwanza akagua maghala ya ununuzi wa pamba

soma pia


Mkuu wa Mkoa Mwanza akagua maghala ya ununuzi wa pamba

 Na George Binagi-GB Pazzo, BMG

Mkuu wa Mkoa Mwanza John Mongella amewataka viongozi na watendaji mbalimbali wakiwemo wa vyama vya msingi vya ushirika AMCOS kuwahamasisha wakulima kuongeza kasi ya uvunaji wa zao hilo ili kunufaika na msimu mpya wa ununuzi ambao tayari umeanza.

Mongella ametoa rai hiyo hii leo baada ya kufanya ziara wilayani Misungwi ili kujionea hali ya ununuzi wa pamba baada ya msimu mpya kuzinduliwa Mei Mosi mwaka huu na Waziri Mkuu Kassim Majaliwa katika Kijiji cha Bukama wilaya ya Igunga mkoani Tabora.

Akizungumza wakati wa ziara hiyo ya kutembelea maghala mbalimbali ya vyama vya msingi vya ushirika AMCOS wilayani Misungwi, Mongella amewataka wasimamizi wa zoezi hilo kuhakikisha mizani haichezewi kwa minajili ya kuwapunja wakulima.

Mkurugenzi wa Huduma za Usimamizi Bodi ya Pamba Tanzania, James Shimbe amesema tayari bodi hiyo imetoa leseni za ununuzi wa zao la pamba kwa vyama vya msingi vya ushirika AMCOS ambapo amewataka wanunuzi wote kuhakikisha wanachukua leseni hizo ili kukidhi vigezo vilivyowekwa.

Naye John Masalu ambaye ni Meneja Shughuli, Chama Kikuu cha Ushirika Nyanza amesema maandalizi yote yamekamilika hivyo ni wakati mwafaka wakulima kunufaika na zao la pamba kupitia AMCOS ambazo zinasimamia zoezi hilo.

Issa Malando ambaye ni mwandishi AMCOS ya Mwalu Mabuki amesema bei ya pamba hivi sasa ni shilingi 1,100 kwa kilo moja hivyo matarajio ni wakulima kuanza kuuza pamba kwa wingi licha ya kwamba baadhi yao bado wanaendelea kuvuna.

Awali akitoa taarifa kwa niaba ya Mkuu wa wilaya Misungwi, Katibu Tawala wilaya hiyo Peter Michale amesema zaidi ya vituo 100 vya ununuzi wa pamba vimejiandaa vyema kusimamia zoezi hilo ambapo tayari vituo 18 vimepokea zaidi ya shilingi milioni 50 kwa ajili ya malipo ya wakulima.


Hivyo makala Mkuu wa Mkoa Mwanza akagua maghala ya ununuzi wa pamba

yaani makala yote Mkuu wa Mkoa Mwanza akagua maghala ya ununuzi wa pamba Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.

Wewe ni sasa kusoma makala Mkuu wa Mkoa Mwanza akagua maghala ya ununuzi wa pamba mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2018/05/mkuu-wa-mkoa-mwanza-akagua-maghala-ya.html

Subscribe to receive free email updates:

0 Response to "Mkuu wa Mkoa Mwanza akagua maghala ya ununuzi wa pamba"

Post a Comment