title : MGODI WA MGONGO GOLD MINE WAWAOKOA WANAFUNZI 99 WANAOSOMEA CHINI YA MITI IRAMBA
kiungo : MGODI WA MGONGO GOLD MINE WAWAOKOA WANAFUNZI 99 WANAOSOMEA CHINI YA MITI IRAMBA
MGODI WA MGONGO GOLD MINE WAWAOKOA WANAFUNZI 99 WANAOSOMEA CHINI YA MITI IRAMBA
Na Jumbe Ismailly IRAMBA
WANAFUNZI 99 wa darasa la awali katika shule ya msingi Kibululu,kata ya Mgongo,tarafa ya Shelui,wilayani Iramba,Mkoani Singida wanasoma wakiwa wamekaa chini ya miti huku wakitumia magoti ya miguu yao kama meza wakati wakiandika kutokana na upungufu wa vyumba vya madarasa pamoja na madawati unaoikabili shule hiyo.
Kaimu Ofisa elimu Kata ya Mgongo,Lazaro Isaya Sakata alithibitisha kuwepo kwa upungufu huo wa vyumba vya madarasa pamoja na madawati kwenye hafla fupi ya kupokea tani tano za mifuko ya saruji zilizotolewa na Kampuni ya kuchimba madini ya Mgongo Gold Mine kwa ajili ya kusaidia ujenzi wa vyumba vya madarasa katika shule hiyo.
Alifafanua Ofisa huyo wa elimu kuwa wanafunzi wa awali katika shule ya msingi Kibululu wanasoma wakiwa wamekaa chini ya miti kwa sababu hakuna chumba cha darasa kinachoweza kuwamudu kuingia wote 99 na kuweza kumsikiliza mwalimu wao kikamilifu.
Kwa mujibu wa Sakata wanafunzi hao 99 wanatakiwa kuwa na vyumba vinne vya madarasa kutokana na kwamba uwiano wa mkondo mmoja ni wanafunzi 25,kitu ambacho kimekuwa kigumu na kulazimika kuwakusanya chini ya miti na kuendelea na masomo.
“Sasa namna ya kumudu kwamba niangalie kila mmoja anaumba vipi ile herufi au kile ninachokifundisha,inakuwa ni kazi kidogo mara kuna mvua mnatoka mnakimbia,mara jua kali inabidi msogee mahali Fulani na mara kuna upepo kwa wakati wote wanakuwa ni vurugu halafu mkiwa nje watoto hawajifunzi vizuri”alisisitiza Sakata.
Akikabidhi msaada huo wa tani tano za saruji,Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya Mgongo Gold Mine,Herieth Michael Sagati alitumia fursa hiyo kuyashawishi Makampuni yanayochimba madini katika Kijiji cha Kibululu kujitokeza na kuhakikisha wanawekeza kwenye sekta ya elimu.
Ni baadhi ya wanafunzi wa shule ya msingi Kibululu,kata ya Mgongo,wilayani Iramba wakionekana wakipanda juu ya gari dogo lililoleta saruji kwa ajili ya kujenga vyumba vya madarasa ambayo yameonekana kuwa ni changamoto kwa wanafunzi kusomea chini ili waweze kushusha mzigo huo.
Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya Mgongo Gold Mine,Herieth Sagati akiwa na wanafunzi wa shule ya msingi Kibululu,kata ya Mgongo katika picha ya pamoja mara baada ya gari lililobeba saruji kuwasili shuleni hapo.(Picha zote Na Jumbe Ismailly).
Hivyo makala MGODI WA MGONGO GOLD MINE WAWAOKOA WANAFUNZI 99 WANAOSOMEA CHINI YA MITI IRAMBA
yaani makala yote MGODI WA MGONGO GOLD MINE WAWAOKOA WANAFUNZI 99 WANAOSOMEA CHINI YA MITI IRAMBA Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala MGODI WA MGONGO GOLD MINE WAWAOKOA WANAFUNZI 99 WANAOSOMEA CHINI YA MITI IRAMBA mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2018/05/mgodi-wa-mgongo-gold-mine-wawaokoa.html
0 Response to "MGODI WA MGONGO GOLD MINE WAWAOKOA WANAFUNZI 99 WANAOSOMEA CHINI YA MITI IRAMBA"
Post a Comment