title : MAPATO YA UTALII YAONGEZEKA HAPA NCHINI
kiungo : MAPATO YA UTALII YAONGEZEKA HAPA NCHINI
MAPATO YA UTALII YAONGEZEKA HAPA NCHINI
Imeelezwa kuwa Ukuaji wa sekta ya utalii hapa nchini, umedhihirika mapato yatokanayo na utalii kuongezaka kutoka Dola bilioni 1.7 mwaka 2012 hadi kufikia Dola bilioni 2.2 mwaka 2017.
Ongezeko la mapato hayo ni kutokana na kuongezeka kwa idadi ya watalii kutoka 1,077,058 mwaka 2012 hadi kufikia watalii 1,327,143 mwaka 2017. Ambapo Sekta ya utalii inachangia takriban asilimia 25 ya mapato ya fedha za kigeni (foreign exchange earnings).
Hayo yamebainishwa na Waziri wa Maliasili na Utalii Dkta Hamis Kigwangala wakati akifungua kongamano la kupitia rasimu ya sera ya Taifa ya utalii ya mwaka1999 linalofanyika jijini hapa na kuwashirikisha wadau wa sekta ya utalii nchini kutoka sekta binafsi na za umma.
Kigwangala amesema kuwa maboresho hayo yaende sambamba na mwendelezo wa mchakato wa kazi nzima ya kupitia Sera ya Taifa ya Utalii ya mwaka 1999 ambayo ni muhimu kwa mstakabali wa sekta ya utalii hapa nchini ambayo Kama ilivyoelezwa hapo awali, mojawapo ya dhumuni la msingi la hatua hiyo linalenga kuwa na Sera inayoendana na mabadiliko ya kiuchumi, mazingira, tecknolojia, kijamii na kisiasa yanayotokea ndani na nje ya nchi yetu ambayo yanagusa maendeleo ya sekta ya utalii nchini.
Amesema kuwa warsha imejumuisha Wadau mbalimbali wa Sekta ya Umma na Binafsi ambao kwa namna moja au nyingine huguswa au hushiriki katika maendeleo ya sekta ya utalii nchini. Aidha, kama mnavyofahamu, utalii ni sekta mtambuka na ili kufanikisha ukuaji wake unahitajika ushirikiano thabiti baina ya wadau wote. Ushirikiano huu utaweza kuleta matokeo chanya iwapo kuna Sera madhubuti ambayo mchakato wake wa maandalizi umeshirikisha wadau kikamilifu.
Hivyo makala MAPATO YA UTALII YAONGEZEKA HAPA NCHINI
yaani makala yote MAPATO YA UTALII YAONGEZEKA HAPA NCHINI Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala MAPATO YA UTALII YAONGEZEKA HAPA NCHINI mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2018/05/mapato-ya-utalii-yaongezeka-hapa-nchini.html
0 Response to "MAPATO YA UTALII YAONGEZEKA HAPA NCHINI"
Post a Comment