title : Makala aweka wazi mahusiano yake na Odama
kiungo : Makala aweka wazi mahusiano yake na Odama
Makala aweka wazi mahusiano yake na Odama
Mtayarishaji na muigizaji wa filamu hapa nchini Laurent Matiholo maarufu kama “Makala” amefunguka na kuweka wazi juu ya ukaribu wake wa kimahusiano na msanii mwenzake Jeniffer Kyaka maarufu kama ”Odama”.
Makala ambaye alijipatia umaarufu mkubwa sana tasnia hii ya filamu,baada ya kupokelewa vema na mashabiki katika kazi zake zilizomtambulisha vema kwenye ulimwengu huo zikiwemo filamu ya Kiss Me, Hot Love, Shella, Surprise na nyingine kibao alizocheza katika kiwango cha hali ya juu na kujipatia umaarufu mkubwa na ndani na nje ya nchi akiwa chini ya Mtunzi na Mtayarishaji nguli Mussa Banzi.
Makala amesema hayo baada ya kuwepo kwa taarifa kwenye baadhi ya mitandao ya kijamii, zikimuhusisha kuwa na ukaribu ambayo ukifananishwa na kuwa na mahusiano ya kimapenzi na msanii mwenzake kitu ambacho akina ukweli wowote.

“Unajua Bongo kumekuwa na mambo mengi sana na watu hata hawajui tumetoka wapi na Odama wanaanza kusambaza uzushi wa mimi kutoka kimahusiano nae, taarifa hizo wanazosambaza hawana uhakika nazo na laiti Wangejua navyomchukulia huyo dada kama nimezaliwa naye tumbo mmoja wala waingethubutu kunipakazia najisikia vibaya,"amesema Makala.
Amesema kuwa katika mafanikio yake Odama amekuwa na mchango mkubwa sana kama dada yake na amempiga tafu sana na anatamani siku moja aje kufikia alipokuwa yeye kwa sasa.
Makala ni mmiliki wa kampuni ya Usambazaji inayofahamika kama Wa Ukweli na kwa sasa anatamba na filamu ya Big SURPRISE inayokimbiza kwenye tasnia ya filamu akicheza na wakali wenzake wakiwemo Gabo,Odama,Mzee Jengua na wengine kibao,yupo njiani kuachia kazi mpya nyingine.
Hivyo makala Makala aweka wazi mahusiano yake na Odama
yaani makala yote Makala aweka wazi mahusiano yake na Odama Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala Makala aweka wazi mahusiano yake na Odama mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2018/05/makala-aweka-wazi-mahusiano-yake-na.html
0 Response to "Makala aweka wazi mahusiano yake na Odama"
Post a Comment