MAJAJI WAPYA 14 WAPATA MAFUNZO YA TEHAMA

MAJAJI WAPYA 14 WAPATA MAFUNZO YA TEHAMA - Hallo rafiki WORLD MAELEZO LATEST, Katika makala kusoma wakati huu na kichwa MAJAJI WAPYA 14 WAPATA MAFUNZO YA TEHAMA, tumeandaa vizuri kwa makala hii kusoma na kupakua maelezo humo. pengine kujaza posts makala afya, makala biashara, makala general, makala hobby, makala karibuni info, makala michezo, makala siasa, makala utamaduni, sisi kuandika anaweza kuelewa. Naam, furaha ya kusoma.

title : MAJAJI WAPYA 14 WAPATA MAFUNZO YA TEHAMA
kiungo : MAJAJI WAPYA 14 WAPATA MAFUNZO YA TEHAMA

soma pia


MAJAJI WAPYA 14 WAPATA MAFUNZO YA TEHAMA

Na Karama Kenyunko, blogu ya jamii 

JAJI Mkuu wa Mahakama ya Tanzania Ibrahimu Juma, amefungua mafunzo elekezi kwa majaji wapya 14 wa Mahakama Kuu nchini yenye lengo la  kuwataka kufanya kazi kwa makini kwa kuwa jamii inamatarajio makubwa kutoka kwao.

Mafunzo hayo ya wiki tatu yamezinduliwa leo katika kituo cha mahakama cha mafunzo ya uongozi kilichopo katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu. Mafunzo hayo yanahusu masuala ya Teknolojia ya Habari na Mawasiliano(Tehama) hasa katika eneo la makosa ya kimtandao.

Akizungumza wakati wa uzinduzi wa mafunzo hao Jaji Mkuu, amewataka majaji hao kutambua kuwa kadri wananchi wanavyotambua haki zao, mlundikano wa kesi unaweza kuongezeka lakini hiyo isiwe kigezo cha wao kushindwa kukidhi matarajio ya wananchi ya kusikiliza mashauri yao na kuyatolea maamuzi kwa wakati.

" Kwa sasa ninyi ni mali ya jamii na jamii inawaangalia na kuwa na matazamio ya kutatua kesi ambazo ziko mbele yenu kwa hiyo muwe mameneja wazuri ", amesema.Pia amewataka majaji hao kujiangalia na kuutumia muda wao vizuri na kuongeza "Kwanza tuna upungufu mkubwa wa majaji, na unapofanikiwa kupata majaji 12 unataka majaji wenye afya na wataofanya kazi sehemu yeyote katika Jamuhuri yetu sehemu yoyote watakayopangiwa, watafanya bila malalamiko kwamba 
wanaugua.

"Sasa kuna magonjwa nyemelezi ambayo yanatokana na maisha, sasa tunawaambia wajiepushe na magonjwa hayo ili wawe na muda mwingi zaidi wa kufanya kazi za kimahakama badala ya kuwa na muda mwingi wa kwenda India au kuwa kwenye hospitali."

Akizungumza kuhusu mlundikano wa kesi, Jaji Mkuu amewataka majaji hao kujitahidi kuamua kesi ambazo zinaweweza kutolewa uamuzi mapema na kumalizika na kwamba jaji mmoja anaweza kuwa na kesi 500 lakini akashauri isiwe sababu ya kurundikana kwa kesi hizo.Ameongeza kuwa kwa sasa ukiiangalia jamii imebadilika na hivyo hawawezi kuacha hukumu zibaki kwenye makaratasi tu, bali hukumu hizo zitolewe mara moja na zipatikane kwenye mitandao.

Majaji wanaohudhuria mafunzo hayo ni, George Masaju, Gerson Mdemu, Ilvin Mgeta, Elinaza Luvanda, Joseph Mlyambina, Immaculate Banzi, Mustapher Siyani, Paul Ngwembe, Agnes Mgeyekwa, Stephen Magoiga, Thadeo Mwenempazi, Butamo Philip, Aziza Suwezi na Khamis Ramadhani.


Hivyo makala MAJAJI WAPYA 14 WAPATA MAFUNZO YA TEHAMA

yaani makala yote MAJAJI WAPYA 14 WAPATA MAFUNZO YA TEHAMA Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.

Wewe ni sasa kusoma makala MAJAJI WAPYA 14 WAPATA MAFUNZO YA TEHAMA mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2018/05/majaji-wapya-14-wapata-mafunzo-ya-tehama.html

Subscribe to receive free email updates:

Related Posts :

0 Response to "MAJAJI WAPYA 14 WAPATA MAFUNZO YA TEHAMA"

Post a Comment