title : Kwa kocha Sir Alex Feguson Wiki chache zinazokuja ni muhimu sana: Kutokwa Damu kwenye/ndani ya Ubongo, Maswali na Majibu
kiungo : Kwa kocha Sir Alex Feguson Wiki chache zinazokuja ni muhimu sana: Kutokwa Damu kwenye/ndani ya Ubongo, Maswali na Majibu
Kwa kocha Sir Alex Feguson Wiki chache zinazokuja ni muhimu sana: Kutokwa Damu kwenye/ndani ya Ubongo, Maswali na Majibu
![]() |
Sir Alex Ferguson |
Ni sahihi familia ya Sir Feguson kutopenda kuzungumzia hali ya mgonjwa wao (Sir Alex) baada ya kukimbizwa hospitali na kufanyiwa upasuaji wa ubongo.
Lakini kwa mtu wa umri wake na historia ya tatizo la moyo alilonalo ikumbukwe mwaka 2003 Sir Alex aliwekewa betri ya moyo (Pacemaker). Sababu kubwa itakuwa kuvuja damu ndani ya ubongo ambayo husababisha adhari zisizoweza tibika( irreparable damage to those cells).
Kwa ugonjwa wa Sir Alex, madaktari walifanya maamuzi ya kufanya upasuaji kwa sababu walihisi uvujaji wa damu ndani ya ubongo ulikuwa unaharibu sehemu zingine za ubongo. Hii huwa inahatarisha uhai wa mgonjwa. Upasuaji huu husaidia kupunguza adhari za muda mrefu kwa Sir Alex ambazo anaweza kuzipata (kutoweza kuzungumza sawa sawa, kupooza upande mmoja n.k) kifupi alichopata ni kiarusi/stroke).
Sir Alex ugonjwa wake kwa vasilimia 100% ni mishipa kupasuka ndio maana maamuzi yalikuwa kupasua ingekuwa ni mishapa kuziba mara nyingi upasuaji huwa haufanywi.
Nini kilicho sababisha?
sababu ni nyingi kwa mfano:
1. Udhaifu wa mishipa ya damu ndani ya ubongo, 2. Ugonjwa ndani ya ubongo, 3. Hitilafu katika ugandaji wa damu (clotting disorders au damu kuwa nyepesi ) labda kwa dawa alizo kuwa anatumia k.m Asprin, clopidogrel nk. Kwa hiyo kila mgojwa anakuwa na sababu tofauti na mwingine.

Siku au wiki chache baada ya upasuaji huu ni muhimu sana kwa mgonjwa kuangaliwa kwa ukaribu kwa mfano damu inaweza toka tena (rebleed).
Kama mgonjwa hajapoteza maisha lakini kapooza au hasemi vizuri na hakujarekebishika kwa wiki au miezi kadha uwezekano wa mgonjwa kurudia shughuli zake za kawaida mara nyingi ni vigumu sana. Kubwa kama madaktari kuna sababu zote za kuendelea kupigania maisha ya mgonjwa husika.
Nini maana ya kutokwa damu kwenye/ndani ya Ubongo?
Maana yake ni kuvuja damu kwenye/ndani ya ubongo(A brain haemorrhage is bleeding in or around the brain). Inasababisha kuvimba kwa ubongo kwa sababu ya mkusanyiko wa damu (hematoma) hii itapelekea kupanda kwa presha ndani ya ubongo na kupunguza mzunguko wa damu ndani ya ubongo. Dalili zake zitakuwa sawa na mtu aliyepata kiarusi (Stroke) yaani upungufu wa nguvu/kupooza upande mmoja wa mwili. Mara zingine wagonjwa watasikia kichwa kuuma sana, kutoo weza kusema/kuzungumza vizuri na kutoona vizuri pia.
Nini kinasababisha kutokwa damu kwenye/ndani ya Ubongo?
Kuna sababu nyingi ya kutokwa damu kwenye/ndani ya Ubongo. Inaweza damu kutoka yenyewe (spontaneous) kwa kupasuka mishapa ya damu (ruptured aneurysm), inajulikana kama Kiarusi/stroke. Sababu zingine ni shinikizo la damu, ambalo husababisha mishipa kuwa dhaifu na kupasuka.
Upasuaji wa ubongo nini kinafanywa na je unasaidia?
Baadhi ya wagonjwa wa hili tatizo wanahitaji upasuaji kupunguza pressure ndani ya ubongo. Upasuaji huu unapunguza/unatoa damu iliyovuja ndani ya ubongo wakati huohuo madaktari wanarekebisha mishipa iliopasuka (repair). Kuna njia kadha za upasuaji ili kupunguza/kutoa damu ndani ya ubongo 1. Kupasua kichwa na kuitoa damu 2. Kutoboa tundu dogo na kuivuta damu iliyovuja ndani ya ubongo.
Nini matokeo ya upasuaji huu wa ubongo?
Matokeo ya upasuaji huu unategemea vitu vingi k.m. sehemu gani ya ubongo umetoka damu, kiasi gani cha damu kimetoka n.k. Wagonjwa wengi hawatakufa kwa tatizo hili lakini kupona kunaweza kuchukua muda mrefu wiki/miezi kadha mpaka miaka au kutopona kabisa (yaani kuweza kuzungumza sawa sawa, kutembea sawa sawa , au kutumia kikamilifu upande wa mwili uliopooza.
Kila la kheri Sir Alex Ferguson
Mohamed Janabi MD., PhD., FACC
Mpenzi wa mpira wa miguu (Soccer)
Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete, Dar es salaam
Hivyo makala Kwa kocha Sir Alex Feguson Wiki chache zinazokuja ni muhimu sana: Kutokwa Damu kwenye/ndani ya Ubongo, Maswali na Majibu
yaani makala yote Kwa kocha Sir Alex Feguson Wiki chache zinazokuja ni muhimu sana: Kutokwa Damu kwenye/ndani ya Ubongo, Maswali na Majibu Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala Kwa kocha Sir Alex Feguson Wiki chache zinazokuja ni muhimu sana: Kutokwa Damu kwenye/ndani ya Ubongo, Maswali na Majibu mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2018/05/kwa-kocha-sir-alex-feguson-wiki-chache.html
0 Response to "Kwa kocha Sir Alex Feguson Wiki chache zinazokuja ni muhimu sana: Kutokwa Damu kwenye/ndani ya Ubongo, Maswali na Majibu"
Post a Comment