title : Msajili Baraza la Uuguzi Tanzania Aanza Kazi Rasmi, apokewa kwa shangwe
kiungo : Msajili Baraza la Uuguzi Tanzania Aanza Kazi Rasmi, apokewa kwa shangwe
Msajili Baraza la Uuguzi Tanzania Aanza Kazi Rasmi, apokewa kwa shangwe
Msajili wa Baraza la Uuguzi na Ukunga Tanzania, Bi. Agnes Mtawa leo ameanza kazi rasmi baada ya kukabidhiwa ofisi tangu alipoteuliwa kushika nafasi hiyo mwezi uliopita. Bi. Agnes Mtawa anachukua nafasi ya Bi. Lena Mfalila aliyemaliza muda wake.
Awali Bi. Mtawa alikuwa Mkurugenzi wa Huduma za Uuguzi katika Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) ambapo mwezi uliopita Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mhe. Ummy Mwalimu alimteua kuwa Msajili wa Baraza la Uuguzi Tanzania.
Uteuzi huo ulianza rasmi tarehe 16-04-2018 na kwamba utadumu kwa muda wa miaka mitano kuanzia tarehe ya uteuzi.
Nafasi mbalimbali alizowahi kushika katika Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH), Bi. Mtawa ni; Mkuu wa Mafunzo na Uajiri kuanzia mwaka 2004 hadi 2006, Mkuu wa Mafunzo, Utafiti na Elimu kuanzia mwaka 1997 hadi 2004, amewahi kuwa Katibu Mkuu katika baraza la uuguzi na ukunga Tanzania kuanzia 2002 hadi 2011 na mwaka 2007 aliteuliwa Mkuurugenzi wa Uuguzi katika Hospitali ya Taifa Muhimbili hadi mwezi uliopita alipoteuliwa.
Msajili wa Baraza la Uuguzi na Ukunga Tanzania, Bi. Agnes Mtawa akikaribishwa leo ofisini na watumishi wa baraza hilo, huku Bi. Jane Mazigo aliyekuwa akikaimu nafasi hiyo akimpatia maua. Kulia ni Happy Masenga anayeshughulika na mafunzo katika baraza hilo.
Msajili wa Baraza la Uuguzi na Ukunga Tanzania, Bi. Agnes Mtawa akitazama zawadi ya maua aliyokabidhiwa na watumishi wa baraza hilo leo.
Msajili wa Baraza la Uuguzi na Ukunga Tanzania, Bi. Agnes Mtawa akikaribishwa kwa shangwe leo ofisini na watumishi wa baraza hilo.
Hivyo makala Msajili Baraza la Uuguzi Tanzania Aanza Kazi Rasmi, apokewa kwa shangwe
yaani makala yote Msajili Baraza la Uuguzi Tanzania Aanza Kazi Rasmi, apokewa kwa shangwe Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala Msajili Baraza la Uuguzi Tanzania Aanza Kazi Rasmi, apokewa kwa shangwe mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2018/05/msajili-baraza-la-uuguzi-tanzania-aanza.html
0 Response to "Msajili Baraza la Uuguzi Tanzania Aanza Kazi Rasmi, apokewa kwa shangwe"
Post a Comment