title : DED MBINGA ATUMBUA WATUMISHI 10 WA IDARA YA AFYA
kiungo : DED MBINGA ATUMBUA WATUMISHI 10 WA IDARA YA AFYA
DED MBINGA ATUMBUA WATUMISHI 10 WA IDARA YA AFYA
Na Mwandishi Wetu Mbinga
MKURUGENZI Mtendaji wa halmashauri ya wilaya ya Mbinga mkoani Ruvuma Gombo Samandito,amewasimamisha kazi watumishi kumi wa idara ya Afya akiwemo mganga mkuu wa halmashauri hiyo Dkt Hussen Sepoko.
Watumishi hao kwa pamoja wamesimamishwa kazi kutokana na matumizi mabaya ya fedha zaidi ya shilingi milioni 11, 270,000/= zilizotolewa na shirika lisilokuwa na kiserikali la Waterled kwa ajili ya kufanikisha mpango wa kutoa elimu ya Afya kwa wananchi kinyume na utaratibu.
Kwa mujibu wa Gombo, watumishi hao walijilipa fedha hizo na kuongopa kwamba wanakwenda kutoa elimu ya Afya ikiwemo masaula ya Ukimwi katika vijiji mbalimbali,hata hivyo katika hali isiokuwa ya kawaida hawakwenda vijijini licha ya kila mmoja kuchukua fedha na kuzitumia kinyume na taratibu.
Mbali na Dkt Sepoko,watumishi wengine ni Andrew Kapinga, Tulizo Nziku,Sara Komba,Mary Ngonyani, Evarist Towegela tabibu mwandamizi,Agnes Adidas,Bryson Mapunda na katibu wa Afya Georg Mhina ambaye alichukua kiasi cha zaidi ya shilingi milioni nne na kwenda kuzifanyia matumizi mengine kinyume na utaratibu na maelekezo ya fedha hizo.
“ ni kweli nimewasimamisha kazi watumishi kumi wa Idara ya Afya katika halmashauri yangu, hawa watumishi wakiongozwa na Dkt Sepoko walichukua fedha zilizotolewa na Waterled kwa kisingizio cha kwenda kutoa elimu ya Afya kwa wananchi lakini hawakufanya hivyo”alisisitiza Gombo.
Alisema,alipata taarifa kuwa watumishi hao kumi kila mmoja alichukua kiasi cha fedha kulingana na cheo chake na kushindwa kwenda vijijini kutekeleza wajibu wao, na hata alipomtuma mkaguzi wa ndani aliyefuatilia ubadhirifu huo katika vijiji vilivyotajwa kupitia hati za malipo alibaini kuwa , watumishi hao hawakwenda vijijini husika licha ya kuchukua fedha.
Gombo alibainisha kuwa, taarifa ya ukaguzi katika kipindi cha Januari hadi March inaonesha kuwa,idara ya Afya imekuwa na matumizi mabaya ya fedha za miradi jambo linalo sababisha Idara hiyo kushindwa kufanya vizuri kutokana na kuwepo kwa watumishi wasiokuwa waadilifu na wanao fanya kazi kwa maslahi binafsi.
Alisema, baada ya kuwasimamisha kazi hatua inayofuata ni ya kinidhamu,ambapo ataunda tume maalum ambayo itawaita na kuwahoji kabla ya kuchukua hatua nyingine zaidi za kiutumishi kutokana na makosa waliyofanya.
Alisema, ataendelea kuchukua hatua kali kwa watumishi wote wa halmashauri ambao wamekuwa wakishiriki katika vitendo vya wizi ili kurudisha nidhamu ya matumizi ya fedha za serikali zinazotolewa kwa ajili ya kuboresha huduma za kijamii na miradi mbalimbali ya maendeleo.
Hivyo makala DED MBINGA ATUMBUA WATUMISHI 10 WA IDARA YA AFYA
yaani makala yote DED MBINGA ATUMBUA WATUMISHI 10 WA IDARA YA AFYA Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala DED MBINGA ATUMBUA WATUMISHI 10 WA IDARA YA AFYA mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2018/05/ded-mbinga-atumbua-watumishi-10-wa.html
0 Response to "DED MBINGA ATUMBUA WATUMISHI 10 WA IDARA YA AFYA"
Post a Comment