title : DC MJEMA APOKEA MSAADA WA KWAAJILI YA WATU WALIO ATHIRIKA NA MAFURIKO.
kiungo : DC MJEMA APOKEA MSAADA WA KWAAJILI YA WATU WALIO ATHIRIKA NA MAFURIKO.
DC MJEMA APOKEA MSAADA WA KWAAJILI YA WATU WALIO ATHIRIKA NA MAFURIKO.
Mwambawahabari
Mkuu wa Wilaya ya Ilala Sophia Mjema leo amepokea Msada wa vyakula na bidhaa mbalimbali kutoka kwa Jumuiya Khoja Shia Ishanashari Kamat na IST kwaajili ya wana nchi na shule za umma zilizoathirika na Mafuriko katika wilaya ya Ilala.
Akizungumza wakati anapokea msaada huo Mh. Mjema amesema katika wilaya hiyo jumla ya nyumba 70 na shule moja zote ziliathirika na mvua katika kipindi cha mwezi April na mvua zinazoendelea kunyesha Jijini Dar es Salaam, na kwamba Kuna watu Misaada hiyo itawasaidia kwa kuwa vitu vyao vingi viliharibiwa na Maji.
"Tuna shukrani Sana ndugu zetu hawa wamekusanyana wamechanga jumla ya shilingi milioni kumi wamenunua hivi vifaa, wametuletea Masink ya vyoo mia moja, water guard, biscuits, Freestyle kwaajili ya akina mama, Taulo, vitabu, madaktari takribani vifaa hivi ni vya watu mitano. "Amesema Mjema.
"Misaada hii itapelekwa kwa familia zilizopata mafuriko zote kila mtu itamfikia"alisema Mjema.
Kwa upande wao waliotoamsaada huo akizungumza mara baada kukabidhi msaada huo Dewji amesema, shule yao ya Tanganyika inafundisha watoto wa miaka minne hadi 12,mara baada kutokea mafuriko hayo wanafunzi wa shule hiyo waliguswa.
"Wanafunzi wa shule yetu wameguswa wameungana na Serikali leo tumekabidhi msaada wetu kwa Mkuu wa Wilaya Sophia Mjema "alisema Dewji.
Hivyo makala DC MJEMA APOKEA MSAADA WA KWAAJILI YA WATU WALIO ATHIRIKA NA MAFURIKO.
yaani makala yote DC MJEMA APOKEA MSAADA WA KWAAJILI YA WATU WALIO ATHIRIKA NA MAFURIKO. Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala DC MJEMA APOKEA MSAADA WA KWAAJILI YA WATU WALIO ATHIRIKA NA MAFURIKO. mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2018/05/dc-mjema-apokea-msaada-wa-kwaajili-ya.html
0 Response to "DC MJEMA APOKEA MSAADA WA KWAAJILI YA WATU WALIO ATHIRIKA NA MAFURIKO."
Post a Comment