Balozi Ambokile kuzindua mgahawa wa chakula cha Kitanzania Afrika Kusini

Balozi Ambokile kuzindua mgahawa wa chakula cha Kitanzania Afrika Kusini - Hallo rafiki WORLD MAELEZO LATEST, Katika makala kusoma wakati huu na kichwa Balozi Ambokile kuzindua mgahawa wa chakula cha Kitanzania Afrika Kusini, tumeandaa vizuri kwa makala hii kusoma na kupakua maelezo humo. pengine kujaza posts makala afya, makala biashara, makala general, makala hobby, makala karibuni info, makala michezo, makala siasa, makala utamaduni, sisi kuandika anaweza kuelewa. Naam, furaha ya kusoma.

title : Balozi Ambokile kuzindua mgahawa wa chakula cha Kitanzania Afrika Kusini
kiungo : Balozi Ambokile kuzindua mgahawa wa chakula cha Kitanzania Afrika Kusini

soma pia


Balozi Ambokile kuzindua mgahawa wa chakula cha Kitanzania Afrika Kusini


 NA CHRISTOPHER LISSA 
Mwamba wa habari
BALOZI wa Tanzania  nchini  Afrika Kusini, Sylvester Ambokile ,  anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika uzinduzi wa mgahawa wa kisasa  wa chakula cha Kitanzania uitwao  Grill House Take Away  jijini Johanesburg nchini humo.

 Mgahawa huo unalengo la kutangaza chakula asili cha kitanzania  kimataifa  pamoja na kuwapa huduma hiyo watanzania waishio nchini humo.
Akizungumza  na waandishi wa habari  jijini Dar es Salaam, jana kwa niaba ya Mmiliki wa Mgahawa huo ,  Christopher Robert, mwakilishi wa mkurugenzi huyo hapa nchini, Frank Koko alisema sherehe za ufunguzi rasmi zimepangwa  kufanyika  Juni 21 mwaka huu.
“Dhima yetu ni kukitangaza chakula asilia cha kitanzania kimataifa. Wapishi wote ni kutoka Tanzania na chakula kinasafirishwa kutoka Tanzania hadi nchini humo,”alisema Koko.
Alisema, kwa miaka mingi chakula cha kitanzania hakijapewa nafasi kubwa katika soko la hoteli na migahawa dunian  kiasi cha kuwafanya hata watanzania wakiwa nje ya nchi kulazimika kula chakula ambacho si asili yao.


“Tuliona kwamba hata hoteli za kitanzania zinapika zaidi  chakula cha  utamaduni wa nje, watu wanalazimika kula tu.Ukifika Johanesburg ni changamoto kubwa kupata chakula cha nyumbani.
Watanzania wanahangaika kupata chakula cha asili yao jambo ambalo lilitusukuma kuja na wazo hili la kuwa na sehemu ambayo mtanzania akitua Johanesburg atapata huduma zote kama za nyumbani,”alisema.
Aliongeza; “ Tunaomba watanzania watakaotembelea Johanesburg watemelee Grill House Take Away , Mtaa wa 51 Regent ili  waweze kutuunga mkono,”alisema Koko.

























Hivyo makala Balozi Ambokile kuzindua mgahawa wa chakula cha Kitanzania Afrika Kusini

yaani makala yote Balozi Ambokile kuzindua mgahawa wa chakula cha Kitanzania Afrika Kusini Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.

Wewe ni sasa kusoma makala Balozi Ambokile kuzindua mgahawa wa chakula cha Kitanzania Afrika Kusini mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2018/05/balozi-ambokile-kuzindua-mgahawa-wa.html

Subscribe to receive free email updates:

Related Posts :

0 Response to "Balozi Ambokile kuzindua mgahawa wa chakula cha Kitanzania Afrika Kusini"

Post a Comment