AZAM WAKATA TAMAA KUTWAA UBINGWA MSIMU HUU, WAAHIDI KULINDA HESHIMA

AZAM WAKATA TAMAA KUTWAA UBINGWA MSIMU HUU, WAAHIDI KULINDA HESHIMA - Hallo rafiki WORLD MAELEZO LATEST, Katika makala kusoma wakati huu na kichwa AZAM WAKATA TAMAA KUTWAA UBINGWA MSIMU HUU, WAAHIDI KULINDA HESHIMA, tumeandaa vizuri kwa makala hii kusoma na kupakua maelezo humo. pengine kujaza posts makala afya, makala biashara, makala general, makala hobby, makala karibuni info, makala michezo, makala siasa, makala utamaduni, sisi kuandika anaweza kuelewa. Naam, furaha ya kusoma.

title : AZAM WAKATA TAMAA KUTWAA UBINGWA MSIMU HUU, WAAHIDI KULINDA HESHIMA
kiungo : AZAM WAKATA TAMAA KUTWAA UBINGWA MSIMU HUU, WAAHIDI KULINDA HESHIMA

soma pia


AZAM WAKATA TAMAA KUTWAA UBINGWA MSIMU HUU, WAAHIDI KULINDA HESHIMA

Na Agness Francis, Blogu ya Jamii

KLABU Bingwa Afrika Mashariki na Kati Azam FC imepoteza matumaini yake ya kunyakuwa kombe la Ligi Kuu vodacom Tanzania bara msimu huu.

Kwa sasa Azam FC ana michezo 3 iliyobakia mpaka hivi sasa ambayo akishinda yote atanyakuwa pointi 9,miwili ikiwa ni ya Nyumbani na mmoja wa ugenini.

Wanalambalamba hao watawakaribisha wanalizombe Maji maji kutoka mkoani Ruvuma katika dimba la Uwanja wa Azam Complex Chamazi jijini Dar es Salaam utakaochezwa kesho saa 10 jioni.

Msemaji wa Azam FC Jafarry Maganga amesema leo jijini Dar es Salaam kuwa wanahitaji kulinda heshima yao hasa kwa kuzingatia mechi hiyo inachezwa kwenye uwanja wao wa  nyumbani huku akifafanua mchezo huo ni wa umuhimu kwao ili kuongeza alama za kuendelea  kubakia  katika nafasi waliyonayo sasa.

"Tutafanya vizuri kwa kushinda michezo yote iliyobaki ili kuendelea kushikilia nafasi ya pili ambayo ina heshima katika ligi hii japo huwezi kuwakilisha nchi kimataifa,"amesema Jaffary.

Ameongeza kulingana na alama walizonazo huku wakiwa wamebakiza  michezo 3 ni ndoto kushika nafasi ya kwanza ambayo anaishikilia mnyama Simba kwa alama 65 huku Azam wakiwa nafasi ya Pili kwa alama 49 wakifatiwa na Mabingwa watetezi Yanga ambao wana alama 48.

Pia Jaffary amesema hatawaonea huruma Majimaji ambao wana wakati mgumu na wapo hatarini kushuka daraja msimu huu wa ligi.

"Hatuta angalia kuwa timu hiyo ina hati hati ya kushuka daraja, muda wa huruma haupo tena ikiwa kila mmoja alipewa mechi ya kwanza hadi ya mwisho na alitakiwa kujipanga mapema ili asifikie hatua hii mbaya,"amesema.

Baada ya kumalizana hiyo kesho na Majimaji, Azam FC watabakiza michezo yao miwili ambapo watawakaribisha Tanzania Prison baada ya hapo watakutana na watoto wa Jangwani akiwa wageni dhidi ha Yanga


Hivyo makala AZAM WAKATA TAMAA KUTWAA UBINGWA MSIMU HUU, WAAHIDI KULINDA HESHIMA

yaani makala yote AZAM WAKATA TAMAA KUTWAA UBINGWA MSIMU HUU, WAAHIDI KULINDA HESHIMA Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.

Wewe ni sasa kusoma makala AZAM WAKATA TAMAA KUTWAA UBINGWA MSIMU HUU, WAAHIDI KULINDA HESHIMA mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2018/05/azam-wakata-tamaa-kutwaa-ubingwa-msimu.html

Subscribe to receive free email updates:

0 Response to "AZAM WAKATA TAMAA KUTWAA UBINGWA MSIMU HUU, WAAHIDI KULINDA HESHIMA"

Post a Comment