title : WAZIRI WA NISHATI: TANESCO KUJENGA KITUO KIDOGO (SUB STATION) MPAKANI MWA URAMBO NA KALIUA NA NGURUKA
kiungo : WAZIRI WA NISHATI: TANESCO KUJENGA KITUO KIDOGO (SUB STATION) MPAKANI MWA URAMBO NA KALIUA NA NGURUKA
WAZIRI WA NISHATI: TANESCO KUJENGA KITUO KIDOGO (SUB STATION) MPAKANI MWA URAMBO NA KALIUA NA NGURUKA
NA TIGANYA VINCENT
RS TABORA
SERIKALI kupitia Shirika lake la la Ugavi wa Umeme Tanzania(TANESCO) itajenga Kituo kidogo(sub station) mpakani wa Urambo na Kaliua na kingine kitajengwa unapokaribia kuingia Nguruka kwa ajili ya kuboresha upatikanaji wa huduma ya umeme kwa wananchi wa Wilaya hizo na maeneo jirani.
Kauli hiyo ilitolewa jana na Waziri wa Dkt. Medard Kalemani wakati alipotembelea Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Tabora kwa ajili ya kusaini kitabu cha wageni kabla ya kuanza ziara yake ya siku moja mkoani humo kukagua miradi ya usambazaji umeme vijijini.
Alisema kuwa lengo la ujenzi wa vituo hivyo ni kurekebisha hali ya upatikanaji wa umememe na kuhakikisha umeme unakuwa wa uhakika ambao utawawezesha wananchi kufanya shughuli mbalimbali za uzalishaji bila wasiwasi.
Katika hatua nyinginye Waziri wa Nishati alisema Serikali itaendelea kuwatembelea Wakandarasi waliopewa jukumu la kujenga miundo mbinu ya kusambaza umeme vijiji chini ya Mradi Kabambe wa Kusambaza Umeme Vijijini Awamu ya Tatu ili kuhakikisha wanakamisha kazi kama walikubaliana katika mkataba.
Alisema wamewaagiza Wakandarasi wanaotekeleza Mradi Kabambe wa Kusambaza Umeme Vijijini Awamu ya Tatu kuhakikisha wanawasha walau vijiji vitatu kili wiki kwa ajili kuharakisha upelekaji wa umeme kwa wananchi waliopo maeneo ya vijijini.
Aidha alisema utafiti uliofanyika hivi karibuni umebaini kuwepo na vijiji 1541 ambavyo vilikuwa havizaingizwa katika Mradi Kabambe wa Kusambaza Umeme Vijijini Awamu ya Tatu na hivyo vitaingizwa mwakani ili navyo viweze kuangashiwa umeme.
Waziri huyo wa Nishati aliagiza wananchi wapatiwe umeme katika maeneo yote ya vijiji ambayo tayari kuna miundombinu ya umeme inapita bila kusubiri Mradi Kabambe wa Kusambaza Umeme Vijijini Awamu ya Tatu.
Akisoma taarifa ya Mkoa . Kaimu Katibu Tawala Mkoa wa Tabora Nathalis Linuma alisema kuwa katika REA III jumla ya vijiji 162 vitanufaika na huduma ya umeme kwa mzunguko wa kwanza.
Hivyo makala WAZIRI WA NISHATI: TANESCO KUJENGA KITUO KIDOGO (SUB STATION) MPAKANI MWA URAMBO NA KALIUA NA NGURUKA
yaani makala yote WAZIRI WA NISHATI: TANESCO KUJENGA KITUO KIDOGO (SUB STATION) MPAKANI MWA URAMBO NA KALIUA NA NGURUKA Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala WAZIRI WA NISHATI: TANESCO KUJENGA KITUO KIDOGO (SUB STATION) MPAKANI MWA URAMBO NA KALIUA NA NGURUKA mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2018/04/waziri-wa-nishati-tanesco-kujenga-kituo.html
0 Response to "WAZIRI WA NISHATI: TANESCO KUJENGA KITUO KIDOGO (SUB STATION) MPAKANI MWA URAMBO NA KALIUA NA NGURUKA"
Post a Comment