WAZIRI MKUU AKUTANA NA MABALOZI WA TANZANIA NCHINI RWANDA NA URUSI

WAZIRI MKUU AKUTANA NA MABALOZI WA TANZANIA NCHINI RWANDA NA URUSI - Hallo rafiki WORLD MAELEZO LATEST, Katika makala kusoma wakati huu na kichwa WAZIRI MKUU AKUTANA NA MABALOZI WA TANZANIA NCHINI RWANDA NA URUSI, tumeandaa vizuri kwa makala hii kusoma na kupakua maelezo humo. pengine kujaza posts makala afya, makala biashara, makala general, makala hobby, makala karibuni info, makala michezo, makala siasa, makala utamaduni, sisi kuandika anaweza kuelewa. Naam, furaha ya kusoma.

title : WAZIRI MKUU AKUTANA NA MABALOZI WA TANZANIA NCHINI RWANDA NA URUSI
kiungo : WAZIRI MKUU AKUTANA NA MABALOZI WA TANZANIA NCHINI RWANDA NA URUSI

soma pia


WAZIRI MKUU AKUTANA NA MABALOZI WA TANZANIA NCHINI RWANDA NA URUSI

WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amewataka mabalozi wanaoiwakilisha Tanzania nchini Urusi na Rwanda kutumia fursa hiyo kwa kutangaza vivutio vilivyopo nchini ili kuwavutia wawekezaji kuja kuwekeza kwenye sekta mbalimbali ikiwemo ya utalii.
Pia amewataka Mabalozi kila mwisho wa mwaka wajifanyie tathmini ya mafanikio waliyoyapata kutokana na uwakilishi wao katika Mataifa ambayo  ni kwa kiasi gani wamechangia kwenye uboreshaji wa maendeleo ya Taifa.
Ametoa maagizo hayo leo (Jumapili, Aprili 8, 2018) wakati akizungumza na Balozi Ernest Mangu anayewakilisha Tanzania nchini Rwanda na Balozi Simon Mumwi anayewakilisha Tazania nchini Urusi, katika ofisi ya Waziri Mkuu mjini Dodoma.
Waziri Mkuu amesema Tanzania ina vivutio vingi vya utalii ikiwa ni pamoja na uwepo wa mbunga za wanyama, hivyo ni vyema wanapoondoka wachukue nyaraka zote zitakazowasaidia katika kutangaza vivutio vya utalii ili kuongeza idadi ya watalii nchini.
Amesema mbali na kutangaza sekta ya utalii, pia watafute wawekezaji kwa ajili ya kuwekeza kwenye sekta nyingine kama vile madini, viwanda na kutafuta masoko ili wafanyabiashara na wakulima wa Tanzania waweze kuuza bidhaa zao nje ya nchi.
“Pia mkajifunze mbinu ambazo wenzetu wanazitumia katika kuboresha sekta mbalimbali ambazo na sisi tunazo hapa nchini kama za viwanda na kisha mje mtueleze namna ya kuziboresha. Kujifunza ni jambo zuri hivyo msisite kufanya hivyo huko muendako.”
Pia Waziri Mkuu amewataka mabalozi hao wakawatambue na kuwaunganisha Watanzania waishio kwenye nchi wanazoiwakilisha ili nao washiriki kwenye ujenzi wa uchumi wa viwanda na wawasisitize wafuate sheria za nchi wanazoishi na wakumbuke nyumbani.


Waziri Mkuu amewasisitiza mabalozi hao kwenda kupunguza gharama za uendeshaji wa Balozi kwa kuzuia matumizi katika mambo yasiyo ya lazima. “Pia maslahi ya nchi lazima mkayasimamie huko muendako hasa katika masuala ya kiuchumi.


Kwa upande wao mabalozi hao  wamesema watahakikisha wanayafanyia kazi maelekezo yote waliyopewa ikiwa ni pamoja na kuimarisha ushirikiano baina ya Tanzania na nchi wanazoziwakilisha.

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na Mkuu wa Jeshi la Polisi Mstaafu, Ernest  Mangu ambaye  ni Balozi wa Tanzania nchini Rwanda (kushoto) na Meja Jenerali  Mstaafu, Simon Marco Mumwi ambaye ni Balozi wa Tanzania nchini Urusi, kabla ya mazungumzo, ofisini kwa Waziri Mkuu mjini Dodoma, Aprili 8, 2018. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na Mkuu wa Jeshi la Polisi Mstaafu, Ernest Mangu ambaye ni Balozi wa Tanzania nchini Rwanda (kushoto) na Meja Jenerali Mstaafu, Simon Marco Mumwi ambaye ni Balozi wa  Tanzania nchini Urusi ofisini kwa Waziri Mkuu mjini Dodoma Aprili 8, 2018. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)



Hivyo makala WAZIRI MKUU AKUTANA NA MABALOZI WA TANZANIA NCHINI RWANDA NA URUSI

yaani makala yote WAZIRI MKUU AKUTANA NA MABALOZI WA TANZANIA NCHINI RWANDA NA URUSI Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.

Wewe ni sasa kusoma makala WAZIRI MKUU AKUTANA NA MABALOZI WA TANZANIA NCHINI RWANDA NA URUSI mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2018/04/waziri-mkuu-akutana-na-mabalozi-wa.html

Subscribe to receive free email updates:

0 Response to "WAZIRI MKUU AKUTANA NA MABALOZI WA TANZANIA NCHINI RWANDA NA URUSI"

Post a Comment