MWENYEKITI JUMUIYA YA WAZAZI CCM TAIFA AHIMIZA VIJANA KUWA NA NIDHAMU

MWENYEKITI JUMUIYA YA WAZAZI CCM TAIFA AHIMIZA VIJANA KUWA NA NIDHAMU - Hallo rafiki WORLD MAELEZO LATEST, Katika makala kusoma wakati huu na kichwa MWENYEKITI JUMUIYA YA WAZAZI CCM TAIFA AHIMIZA VIJANA KUWA NA NIDHAMU, tumeandaa vizuri kwa makala hii kusoma na kupakua maelezo humo. pengine kujaza posts makala afya, makala biashara, makala general, makala hobby, makala karibuni info, makala michezo, makala siasa, makala utamaduni, sisi kuandika anaweza kuelewa. Naam, furaha ya kusoma.

title : MWENYEKITI JUMUIYA YA WAZAZI CCM TAIFA AHIMIZA VIJANA KUWA NA NIDHAMU
kiungo : MWENYEKITI JUMUIYA YA WAZAZI CCM TAIFA AHIMIZA VIJANA KUWA NA NIDHAMU

soma pia


MWENYEKITI JUMUIYA YA WAZAZI CCM TAIFA AHIMIZA VIJANA KUWA NA NIDHAMU

Na Elissa Shunda
WAZAZI nchini wameombwa kudumisha nidhamu katika maisha wanayoishi ili vijana wao pia ambao ndiyo viongozi wajao katika ngazi mbalimbali waige mifano mizuri ya kitabia na kiuongozi kutoka kwao ili waje kuwa viongozi bora na si bora kiongozi.

Kauli hiyo imetolewa leo na Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Taifa,Dk.Edmund Mndolwa wakati akizungumza na wanachama wa Jumuiya hiyo na wananchi waliohudhuria  Maadhimisho ya wiki ya wazazi.

Ambayo kitaifa yalifanyika katika ofisi kuu ya wilaya ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) iliyopo wilayani Nzega mkoani Tabora na kuhudhuriwa na viongozi wengine wakuu wa jumuiya hiyo na viongozi wa ngazi mbalimbali wa Serikali.

Katika maadhimisho hayo Dk.Edmund Mndolwa amewaambia wazazi,viongozi,wanachama na wanajumuiya hiyo kuwa ili kijana awe na tabia nzuri katika ukuaji wake na katika utawala wake akichaguliwa kuwa kiongozi mzazi ni mtu wa kwanza katika kumlea mtoto huyo akue katika maadili mazuri.

"Mzazi au mlezi hakikisha katika ukuaji wa kijana wako unamsimamia bega kwa bega kuhakikisha anazingatia maadili na haigi mambo ambayo hayana tija.

“Ndugu zangu wazazi wenzangu katika ukuaji wa mtoto mzazi awe baba na mama ndiyo watu wa kwanza katika kuhakikisha watoto wake wanakua katika maadili mazuri kwa kuwafundisha kila lililo jema na kuwaonyesha lililo baya kuanza tabia na mavazi ambayo kijana aliye mtiifu anapaswa kuyavaa.

"Haiwezekani mzazi anamuona mwanae anatoka usiku anaenda kucheza disko hamkanyi au mzazi unamuona mtoto anatembea na makundi ya vijana wenzake ambao hawana tabia nzuri wewe humkanyi unamnyamazia kwa kuogopa kumkera hapo kaa ukijua mwanao anaharibikiwa utakapotaka kumrekebisha utakuwa umechelewa," anasema.

Mwenyekiti wa Umoja wa Wazazi Jumuiya ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) Taifa, Dk.Edmund Mndolwa akizungumza katika maadhimisho ya wiki ya Wazazi Taifa ambayo yalifanyika katika wilayani Nzega Mkoa wa Tabora leo. Picha zote na Elisa Shunda.
Mwenyekiti wa Umoja wa Wazazi Jumuiya ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) wa Mkoa wa Pwani, Jackson kituka, Katibu Mkuu wa jumuiya hiyo wa Mkoa huo, Gama J.Gama, Mjumbe wa Baraza Kuu Taifa kutoka Mkoa wa Pwani, Dk.Zainab Gama na Mwenyekiti wa Umoja wa Wazazi wa Wilaya ya Kibaha Mjini, Edwin Shunda na wajumbe wengine wakimsikilza kwa makini Mwenyekiti wa Jumuiya hiyo Taifa Dk.Edmund Mndolwa (hayupo pichani) alipokuwa akizungumza katika maadhimisho hayo.
 





Hivyo makala MWENYEKITI JUMUIYA YA WAZAZI CCM TAIFA AHIMIZA VIJANA KUWA NA NIDHAMU

yaani makala yote MWENYEKITI JUMUIYA YA WAZAZI CCM TAIFA AHIMIZA VIJANA KUWA NA NIDHAMU Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.

Wewe ni sasa kusoma makala MWENYEKITI JUMUIYA YA WAZAZI CCM TAIFA AHIMIZA VIJANA KUWA NA NIDHAMU mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2018/04/mwenyekiti-jumuiya-ya-wazazi-ccm-taifa.html

Subscribe to receive free email updates:

0 Response to "MWENYEKITI JUMUIYA YA WAZAZI CCM TAIFA AHIMIZA VIJANA KUWA NA NIDHAMU"

Post a Comment