WATAFITI WA KODI AFRIKA WAJENGEWA UWEZO

WATAFITI WA KODI AFRIKA WAJENGEWA UWEZO - Hallo rafiki WORLD MAELEZO LATEST, Katika makala kusoma wakati huu na kichwa WATAFITI WA KODI AFRIKA WAJENGEWA UWEZO, tumeandaa vizuri kwa makala hii kusoma na kupakua maelezo humo. pengine kujaza posts makala afya, makala biashara, makala general, makala hobby, makala karibuni info, makala michezo, makala siasa, makala utamaduni, sisi kuandika anaweza kuelewa. Naam, furaha ya kusoma.

title : WATAFITI WA KODI AFRIKA WAJENGEWA UWEZO
kiungo : WATAFITI WA KODI AFRIKA WAJENGEWA UWEZO

soma pia


WATAFITI WA KODI AFRIKA WAJENGEWA UWEZO

Watafiti wa Kodi Barani Afrika wameshauriwa kuimarisha mtandao wao ili kuweza kusaidiana kutatua changamoto mbalimbali zinazowakabili katika jitihada zao za kufanya utafiti.

Ushauri huo umetolewa na Mkurugenzi wa Rasilimali Watu na Utawala wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Bw. Michael John wakati akifunga warsha ya mafunzo ya kuwajengea uwezo wajumbe wa Mtandao wa Watafiti wa Kodi Afrika (ATRN) ambayo imeandaliwa na Taasisi ya Usimamizi wa Kodi Barani Afrika (ATAF) kwa kushirikiana na Chuo cha Kodi (ITA).

Bw. Michael amesema kwamba watafiti hao wanategemewa sana na mamlaka za mapato wanazoziwakilisha hivyo kuwataka kutumia ujuzi wa utafiti walioupata wakati wa mafunzo hayo ya siku nne kutatua changamoto mbalimbali na kuziongezea uwezo mamlaka za mapato barani Afrika hivyo kupelekea kuongeza makusanyo.

“Nina imani kwamba baada ya mafunzo haya mtaendelea kushirikiana kupitia mtandao wenu ili kwa pamoja mtimize lengo lenu la kutatua changamoto katika utekelezaji wa taratibu, sheria na sera za kodi barani Afrika kupitia utafiti mtakaoufanya”.Aidha amewataka watafiti hao kuzitumia vyema nyenzo za ukusanyaji na uchambuzi wa taarifa ambazo wamepatiwa wakati wa mafunzo hayo ambayo yamefanyika Jijini Dar es Salaam.

Mkurugenzi huyo wa Rasilimali Watu na Utawala ameipongeza Taasisi ya Kodi Barani Afrika pamoja na Chuo cha Kodi kwa kuandaa na kufanikisha mafunzo hayo ambayo ni muhimu katika utendaji wa usimamizi wa Kodi barani Afrika.
Mkurugenzi wa Rasilimali Watu na Utawala wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Bw. Michael John akimkabidhi mshiriki kutoka Tunisia Bw. Jabali Belhanssen cheti cha ushiriki wa mafunzo ya utafiti ambayo yafanyika jijini Dar es Salaam kwa ushirikiano wa Taasisi ya Usimamizi wa Kodi Afrika (ATAF) na Chuo cha Kodi (IAT). Wengine kutoka kushoto ni Mkuu wa Chuo cha Kodi (ITA) Prof. Isaya Jairo, Naibu Mkuu wa Chuo Taaluma na Utafiti Dr. Lewis Ishemoi na Mwakilishi ATAF Bw. Eugenio Bras.
Mkurugenzi wa Rasilimali Watu na Utawala wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Bw. Michael John (katikati) akifuatilia matukio wakati wa kufunga na kukabidhi vyeti kwa washiriki wa warsha ya mafunzo kwa Mtandao wa Watafiti wa Kodi Afrika (ATRN) ambayo imefanyika jijini Dar es salaam. Wengina kutoka kushoto ni; Mkufunzi wa mafunzo hayo Prof. Nicaise Mede kutoka Benin, Mkuu wa Chuo cha Kodi (ITA) Prof. Isaya Jairo, Naibu Mkuu wa Chuo cha Kodi Taaluma na Utafiti Dr. Lewis Ishemoi na Mwakilishi wa Taasisi ya Utafiti Barani Afrika (ATAF) Bw. Eugenio Bras.
Baadhi ya washiriki wa Warsha ya Mafunzo kwa Mtandao wa Watafiti wa Kodi Afrika (ATRN) waliosimama wakiwa katika picha ya pamoja na Mkurugenzi wa Rasilimali Watu na Utawala wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Bw. Michael John (aliyekaa katikati) baada ya kufunga mafunzo hayo. Wengine kutoka kulia ni, Mwakilishi wa Taasisi ya Utafiti Barani Afrika (ATAF) Bw. Eugenio Bras, Naibu Mkuu wa Chuo cha Kodi Taaluma na Utafiti Dr. Lewis Ishemoi, Mkuu wa Chuo cha Kodi (ITA) Prof. Isaya Jairo na Mkufunzi wa mafunzo hayo Prof. Nicaise Mede kutoka Benin

HABARI ZAIDI BOFYA HAPA


Hivyo makala WATAFITI WA KODI AFRIKA WAJENGEWA UWEZO

yaani makala yote WATAFITI WA KODI AFRIKA WAJENGEWA UWEZO Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.

Wewe ni sasa kusoma makala WATAFITI WA KODI AFRIKA WAJENGEWA UWEZO mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2018/04/watafiti-wa-kodi-afrika-wajengewa-uwezo_14.html

Subscribe to receive free email updates:

Related Posts :

0 Response to "WATAFITI WA KODI AFRIKA WAJENGEWA UWEZO"

Post a Comment