title : Wasanii watakiwa kuwa makini wanapo saini Mikataba.
kiungo : Wasanii watakiwa kuwa makini wanapo saini Mikataba.
Wasanii watakiwa kuwa makini wanapo saini Mikataba.
Na Agness Francis, Globu ya Jamii.
Wasanii wa nyanja zote wakumbushwa kuzingatia na kuwa makini kuzitambua aina 7 za sheria katika zoezi zima la kusaini mikataba mbalimbali katika kazi zao hapa Nchini.
Akizungumza na wasanii mbalimbali leo katika ukumbi wa Baraza la sanaa Tanzania (BASATA) Jijini Dar es Salaam Wakili wa kampuni ya Setla, Noeli Chikwindo amesema kuwa ni vema kwa wasanii kufahamu sheria 7 za usaini wa mikataba ili kupata haki zao zinazostahiki.
" Ni vema kabla hujatia saini ufahamu ni kitu gani unasaini pamoja na kuelewa vizuri lugha iliyotumika katika mkataba huo ili kuepuka matatizo ya baade yatakayojitokeza"amesema wakili Chikwito.
Vile vile amewataka wasanii kuwa makini na kazi zao pindi wanapoingia mkataba na kampuni yoyote kuzingatia zile sheria 7 katika makubaliano hayo.
"Msanii ni muhimu kufahamu masharti ya mkataba kabla ya makubaliano inasaidia kuepuka usumbufu wa kupata haki yako,na wakati mwinginine msanii hulalamika kumbe yeye ndo chanzo cha matatizo" amesema wakili Chikwindo.
Aidha msanii wa muziki wa dansi Franswaa Makasi amewataka wasanii wenzake wa nyanja mbalimbali wajitambue katika kuzingatia mikataba wanayosaini kuwa na vipengele vyote vya sheria ili kuondokana na usumbufu
"Wasanii wenzangu ifike mahari tujitambue ili haki zetu zipate kutendeka sawa,kazi zipo mikataba ipo lakini hatujitambui na sisi tutende haki upande wa pili maana wasanii wengine vile vile hawatendi haki" amesema makasi Junior.
Hivyo makala Wasanii watakiwa kuwa makini wanapo saini Mikataba.
yaani makala yote Wasanii watakiwa kuwa makini wanapo saini Mikataba. Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala Wasanii watakiwa kuwa makini wanapo saini Mikataba. mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2018/04/wasanii-watakiwa-kuwa-makini-wanapo.html
0 Response to "Wasanii watakiwa kuwa makini wanapo saini Mikataba."
Post a Comment