MAADHIMISHO YA SIKU YA MTOTO YATIMA YAFANYIKA ZANZIBAR

MAADHIMISHO YA SIKU YA MTOTO YATIMA YAFANYIKA ZANZIBAR - Hallo rafiki WORLD MAELEZO LATEST, Katika makala kusoma wakati huu na kichwa MAADHIMISHO YA SIKU YA MTOTO YATIMA YAFANYIKA ZANZIBAR, tumeandaa vizuri kwa makala hii kusoma na kupakua maelezo humo. pengine kujaza posts makala afya, makala biashara, makala general, makala hobby, makala karibuni info, makala michezo, makala siasa, makala utamaduni, sisi kuandika anaweza kuelewa. Naam, furaha ya kusoma.

title : MAADHIMISHO YA SIKU YA MTOTO YATIMA YAFANYIKA ZANZIBAR
kiungo : MAADHIMISHO YA SIKU YA MTOTO YATIMA YAFANYIKA ZANZIBAR

soma pia


MAADHIMISHO YA SIKU YA MTOTO YATIMA YAFANYIKA ZANZIBAR

Na Salum Vuai, MAELEZO
MAKAMU wa Rais Samia Suluhu Hassan, amesema jamii ina wajibu wa kuwalea na kuwatunza watoto yatima badala ya kuwakwepa, kuwanyanyasa na kuwadhulumu.

Katika hutuba iliyosomwa kwa niaba yake na Waziri wa Kazi, Uwezeshaji, Wazee, Wanawake na Watoto Maudline Castico kwenye maadhimisho ya siku ya mtoto yatima duniani huko Fumba, Samia amesema kuwapuuza yatima ni kubeba dhima kwa Mwenyezi Mungu.

Alifahamisha kuwa, ni lazima ndugu na wanafamilia wa wazazi wanaotangulia mbele ya haki, wakubali  kuwa walezi wa watoto wanaoachiwa kwa kila hali na kuwapatia mahitaji ya msingi ikiwemo elimu na kuwafundisha maadili mazuri.

Makamu wa Rais, alieleza kuwa, haijuzu kwa mtu mzima kupuuza umuhimu wa kuwalea na kuwatunza watoto yatima, ikizingatiwa kwamba kila mmoja atakutana na kifo wakati wowote, hivyo naye pia kuacha watoto nyuma yake.

“Unapomnyanyasa yatima wa Mungu, ukamnyima matunzo, na mara nyengine ukamdhulumu mirathi na haki zake wakati nawe pia una watoto, na ni mgeni katika dunia hii, je, ukifariki utaridhika watoto wako wanyanyaswe?”, alihoji Makamu wa Rais. 

Alisisitiza kuwa, jukumu la kuwalea na kuwatunza  watoto waliopoteza wazazi wao ni la kila mtu na wanapaswa kuwapa upendo, matunzo pamoja na elimu ambayo ndio mkombozi wa maisha yao kwa sasa na hapo baadae.


 Mgeni rasmi Waziri wa  Kazi Uwezeshaji Wanawake Wazee na Watoto Maudline Cyrus  Castico akitoa Hotuba  katika maadhimisho ya Siku ya Mtoto yatima yaliofanyika katika Viwanja vya Bakhresa Fumba Wilaya ya Magharibi B Unguja.   

 Mufti Mkuu wa Zanzibar Sheikh Swaleh Omar Kabi akitoa hotuba yamakaribisho kwa mgeni rasmi  katika maadhimisho ya Siku ya Mtoto yatima yaliofanyika katika Viwanja vya Bakhresa Fumba Wilaya ya Magharibi B Unguja.  
 Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Kiislamu ya Muzdalifa Farouk Hamad  Khamis akizungumza machache kuhusu mtoto yatima katika maadhimisho ya Siku ya Mtoto yatima yaliofanyika katika Viwanja vya Bakhresa Fumba Wilaya ya Magharibi B Unguja.
 Baadhi ya Watoto mayatima waliohudhuria katika maadhimisho ya Siku ya Mtoto yatima yaliofanyika katika Viwanja vya Bakhresa Fumba Wilaya ya Magharibi B Unguja.
 Watoto mayatima kutoka Skuli ya Alfarouk Aktas Muslim wakisoma Kasda maalum yenye maudhui ya kumlinda mtoto yatima katika maadhimisho ya Siku ya Mtoto yatima yaliofanyika katika Viwanja vya Bakhresa Fumba Wilaya ya Magharibi B Unguja.

 KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA



Hivyo makala MAADHIMISHO YA SIKU YA MTOTO YATIMA YAFANYIKA ZANZIBAR

yaani makala yote MAADHIMISHO YA SIKU YA MTOTO YATIMA YAFANYIKA ZANZIBAR Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.

Wewe ni sasa kusoma makala MAADHIMISHO YA SIKU YA MTOTO YATIMA YAFANYIKA ZANZIBAR mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2018/04/maadhimisho-ya-siku-ya-mtoto-yatima.html

Subscribe to receive free email updates:

0 Response to "MAADHIMISHO YA SIKU YA MTOTO YATIMA YAFANYIKA ZANZIBAR"

Post a Comment