WANANCHI WATAKIWA KUJIUNGA NA MIFUKO YA AFYA JAMII ILI KUKWEPA GHARAMA ZA MATIBABU

WANANCHI WATAKIWA KUJIUNGA NA MIFUKO YA AFYA JAMII ILI KUKWEPA GHARAMA ZA MATIBABU - Hallo rafiki WORLD MAELEZO LATEST, Katika makala kusoma wakati huu na kichwa WANANCHI WATAKIWA KUJIUNGA NA MIFUKO YA AFYA JAMII ILI KUKWEPA GHARAMA ZA MATIBABU, tumeandaa vizuri kwa makala hii kusoma na kupakua maelezo humo. pengine kujaza posts makala afya, makala biashara, makala general, makala hobby, makala karibuni info, makala michezo, makala siasa, makala utamaduni, sisi kuandika anaweza kuelewa. Naam, furaha ya kusoma.

title : WANANCHI WATAKIWA KUJIUNGA NA MIFUKO YA AFYA JAMII ILI KUKWEPA GHARAMA ZA MATIBABU
kiungo : WANANCHI WATAKIWA KUJIUNGA NA MIFUKO YA AFYA JAMII ILI KUKWEPA GHARAMA ZA MATIBABU

soma pia


WANANCHI WATAKIWA KUJIUNGA NA MIFUKO YA AFYA JAMII ILI KUKWEPA GHARAMA ZA MATIBABU


RS TABORA

SERIKALI imezitaka jamii kujiunga na mifuko ya huduma za bima za jamii ili waweze kupata huduma ya tiba kwa gharama nafuu badala ya kutumia mtindo wa kulipa fedha taslimu wanapokwenda kutibiwa.

Kauli hiyo ilitolewa jana Wilayani Nzega na Waziri wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu wakati akizungumza na wakazi wa Zogolo mara baada ya kukizindua.

Alisema kazi wananchi ambapo hajajiunga na Mifuko ya Afya ya Jamii(CHF) na mingine wanajikuta wakitumia fedha nyingi kwa ajili ya matibabu wakati wangekata Bima za viwango tofauti wangenufaika.

Waziri huyo alisema mtu akimkatia mtoto wake mdogo Bima ya Afya ya shilingi elfu 50 atapata huduma za matibabu mwaka mzima katika Hospitali yoyote hapa nchini zikiwemo za binafsi ambazo zina makataba na Serikali kupitia Mfuko wa Bima ya Afya ya Taifa. Aliwataka Madereva wa boda boda wilayani Nzega nao kujiunga na Bima kwa kulipia shilingi 76000 ili waweze kupata matatibu mwaka mzima popte pindi wanapopata ajali au wanapougua na kuongeza kuwa kwa kutegemea fedha taslimu ni gharama kubwa.

Waziri huyo aliwambia wakijunga pamoja na kutoa kiasi hicho atawaunganisha ili waweze kupata vitambulisho vya Bima ambavyo vitawaweze kupata matibabu kwa gharama nafuu na fedha nyingine kuzielekeza katika shughuli nyingine za maendeleo. “unapokwenda kufanyiwa upasuaji unaweza kutozwa shilingi 100,000/- lakini ukiwa umetoa shilingi elfu 30 kupitia kujiunga Mfuko wa Afya ya Jamii , utatumia kadi kupata huduma hiyo katika Hospitali yoyote bila kudaiwa chochote” alisisitiza Ummy

Kwa upande wa Mkuu wa Mkoa Aggrey Mwanri alisema kuwa mwitikio wa wananchi Mkoani humo kujiunga na Mfuko wa Afya ya Jamii (CHF) bado uko chini na kuongeza kuwa wameamua kuendesha elimu kupitia mikutano mbalimbali kwa lengo la kuongeza idadi inaongezeka.

Alisema kuwa sehemu kubwa ya wakazi ni wakulima ambao wanategemea mavuno ya msimu kujipatia kipato kwa ajili ya mahitaji mbalimbali ikiwemo matibabu na hivyo kupata shida wakati mwingine kwa kutokuwa na uwezo wa kulipia gharama kwa fedha tasilimu kwa kuwa fedha zinakuwa hazipo tena hadi mavuno mengine.

Mwanri alisema njia ya pekee ya kuwasaidia wakulima ni kuhakikisha wengi wao wamejiunga na Mfuko wa Jamii ambapo wakitoa shilingi 10,000 wanapata matibabu watu sita katika familia moja.


Hivyo makala WANANCHI WATAKIWA KUJIUNGA NA MIFUKO YA AFYA JAMII ILI KUKWEPA GHARAMA ZA MATIBABU

yaani makala yote WANANCHI WATAKIWA KUJIUNGA NA MIFUKO YA AFYA JAMII ILI KUKWEPA GHARAMA ZA MATIBABU Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.

Wewe ni sasa kusoma makala WANANCHI WATAKIWA KUJIUNGA NA MIFUKO YA AFYA JAMII ILI KUKWEPA GHARAMA ZA MATIBABU mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2018/04/wananchi-watakiwa-kujiunga-na-mifuko-ya.html

Subscribe to receive free email updates:

Related Posts :

0 Response to "WANANCHI WATAKIWA KUJIUNGA NA MIFUKO YA AFYA JAMII ILI KUKWEPA GHARAMA ZA MATIBABU"

Post a Comment