title : WANANCHI MKOANI GEITA WAJITOKEZA KWA WINGI KUPATA ELIMU YA MLIPAKODI
kiungo : WANANCHI MKOANI GEITA WAJITOKEZA KWA WINGI KUPATA ELIMU YA MLIPAKODI
WANANCHI MKOANI GEITA WAJITOKEZA KWA WINGI KUPATA ELIMU YA MLIPAKODI
Na Veronica Kazimoto
Wafanyabiashara na wananchi wa Mkoa wa Geita wamejitokeza kwa wingi kupata elimu ya mlipakodi inayoambatana na usajili wa Namba ya Utambulisho wa Mlipakodi (TIN) pamoja na kupatiwa makadirio ya kodi kwa wafanyabiashara mbalimbali.
Akizungumza baada ya kutoa elimu kwa wafanyabiashara na wananchi wa Wilaya ya Bukombe na Mbogwe wakati wa Kampeni Maalum ya Huduma na Elimu kwa Mlipakodi inayoendelea mkoani hapa, Afisa Kodi Mwandamizi wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Maternus Mallya amesema mwitikio wa wananchi ni mkubwa na unaridhisha.
"Nimefurahishwa sana na mwitikio wa wananchi wa Mkoa wa Geita kwasababu wengi wameonyesha kiu ya kupata elimu na Namba ya Utambulisho wa Mlipakodi na mpaka sasa takribani wafayabiashara 200 wamesajiliwa na kupatiwa namba hiyo pamoja na kufanyiwa makadirio ya kodi ya mapato," alisema Mallya.
Nae mfanyabiashara wa kuchomelea mageti wa Wilaya ya Bukombe, Mandela Alex amesema kuwa, amefurahishwa na ujio wa kampeni hii wilayani kwake kwani biashara yake imetambulika na kuingizwa kwenye mfumo rasmi wa kibiashara.
Afisa wa Huduma na Elimu kwa Mlipakodi wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) George Haule (kushoto) akitoa elimu ya kodi kwa wafanyabiashara wa Wilaya ya Bukombe mkoani Geita wakati wa Kampeni Maalum ya Huduma na Elimu kwa Mlipakodi inayoendelea mkoani hapa na inatarajia kumalizika tarehe 13 Aprili, 2018.
Afisa wa Kodi Mwandamizi wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Maternus Mallya (kulia) akitoa elimu ya kodi kwa wafanyabiashara wa Wilaya ya Mbogwe mkoani Geita wakati wa Kampeni Maalum ya Huduma na Elimu kwa Mlipakodi inayoendelea mkoani hapa na inatarajia kumalizika tarehe 13 Aprili, 2018.
Afisa wa Kodi wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Adela Kayella akimuhudumia mfanyabiashara aliefika kwenye Kampeni Maalum ya Huduma na Elimu kwa Mlipakodi inayoendelea mkoani Geita. Kampeni hiyo inatarajia kumalizika tarehe 13 Aprili, 2018.
Maafisa wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) wakipita katika maduka mbalimbali kutoa elimu ya masuala yanayohusu kodi wakati wa Kampeni Maalum ya Huduma na Elimu kwa Mlipakodi inayoendelea mkoani Geita. Kampeni hiyo inatarajia kumalizika tarehe 13 Aprili, 2018.
KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA
KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA
Hivyo makala WANANCHI MKOANI GEITA WAJITOKEZA KWA WINGI KUPATA ELIMU YA MLIPAKODI
yaani makala yote WANANCHI MKOANI GEITA WAJITOKEZA KWA WINGI KUPATA ELIMU YA MLIPAKODI Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala WANANCHI MKOANI GEITA WAJITOKEZA KWA WINGI KUPATA ELIMU YA MLIPAKODI mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2018/04/wananchi-mkoani-geita-wajitokeza-kwa.html
0 Response to "WANANCHI MKOANI GEITA WAJITOKEZA KWA WINGI KUPATA ELIMU YA MLIPAKODI"
Post a Comment