TRA YASAJILI WAFANYABIASHARA WAPYA 600 MKOANI GEITA

TRA YASAJILI WAFANYABIASHARA WAPYA 600 MKOANI GEITA - Hallo rafiki WORLD MAELEZO LATEST, Katika makala kusoma wakati huu na kichwa TRA YASAJILI WAFANYABIASHARA WAPYA 600 MKOANI GEITA, tumeandaa vizuri kwa makala hii kusoma na kupakua maelezo humo. pengine kujaza posts makala afya, makala biashara, makala general, makala hobby, makala karibuni info, makala michezo, makala siasa, makala utamaduni, sisi kuandika anaweza kuelewa. Naam, furaha ya kusoma.

title : TRA YASAJILI WAFANYABIASHARA WAPYA 600 MKOANI GEITA
kiungo : TRA YASAJILI WAFANYABIASHARA WAPYA 600 MKOANI GEITA

soma pia


TRA YASAJILI WAFANYABIASHARA WAPYA 600 MKOANI GEITA

Na Veronica Kazimoto, Geita.

Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) imesajili jumla ya wafanyabiashara wapya 600 katika kampeni maalum ya utoaji huduma na elimu kwa mlipakodi iliyofanyika mkoani Geita ikiwa na lengo la kutoa elimu kuhusu masuala mbalimbali ya kodi pamoja na kusikiliza malalamiko, changamoto na maoni kutoka kwa wafanyabiashara hao.

Akizungumza mara baada ya kukamilika kwa kampeni hiyo mwishoni mwa wiki, Menenja wa TRA mkoani hapa James Jilala ameishukuru Idara ya Huduma na Elimu kwa Mlipakodi kwa kufika mkoani Geita hususani katika maeneo ambayo hakuna ofisi ya Mamlaka ya Mapato Tanzania na kufanikiwa kusajili wafanyabiashara wengi ndani ya wiki moja.

“Nianze kwa kuishukuru Idara ya Huduma na Elimu kwa Mlipakodi kwa hatua ambayo mmeifanya ya kufika katika Mkoa wetu wa Geita hasa maeneo ambayo hatuna ofisi ya TRA na kufanikiwa kusajili wafanyabiashara wengi kwa muda mfupi kitu ambacho kimekuwa historia kwetu,” alisema Jilala.

Jilala alisema kuwa, baadhi ya wafanyabiashara walishindwa kusajiliwa na kupatiwa Namba ya Utambulisho wa Mlipakodi (TIN) kwa wakati, kwasababu walitakiwa kusafiri zaidi ya kilomita 100 kwenda Geita mjini kwa ajili ya kupata huduma hiyo. Hivyo, zoezi hili limewarahisishia wafayabiashara kusajiliwa na kupatiwa TIN.

Naye Meneja wa Huduma na Elimu kwa Mlipakodi kutoka TRA Makao Makuu Gabriel Mwangosi alisema kuwa , pamoja na usajili wa wafanyabiashara hao, shughuli mbalimbali zimefanyika katika kampeni hiyo ikiwa ni pamoja na utoaji wa elimu kwa wafanyabiashara kuhusu masuala mbalimbali ya kodi kupitia semina na kuwatembelea katika sehemu zao za biashara.

“Katika zoezi hili tumefanya shughuli nyingi sana ikiwa ni pamoja na kuwatembelea wafanyabiashara mahali wanapofanyia biashara zao, tumesajili wafanyabiashara wapya na tumetoa semina mbalimbali ambazo tunaamini kabisa zitakuwa zimebadilisha mtizamo, utendaji na mwenendo mzima wa ulipaji kodi katika Mkoa huu wa Geita,” alieleza Mwangosi.

Kampeni ya huduma na elimu kwa mlipakodi ni moja ya mikakati ambayo Mamlaka ya Mapato Tanzania imejiwekea katika kuhakikisha kuwa inasajili wafanyabiashara 1,000,000 katika mwaka huu wa Fedha wa 2017/18.
Maafisa wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) wakiwasajili wafanyabiashara wapya Wilaya ya Bukombe mkoani Geita wakati wa kampeni maalum ya utoaji huduma na elimu kwa mlipakodi iliyomalizika mwishoni mwa wiki ikiwa na lengo la kutoa elimu kuhusu masuala mbalimbali ya kodi, kusajili wafanyabiashara wapya, pamoja na kusikiliza malalamiko, changamoto na maoni kutoka kwa wafanyabiashara hao.
Afisa wa Kodi wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Lameck Ndida akitoa elimu kuhusu masuala mbalimbali ya kodi kwa wafanyabiashara wakati wa kampeni maalum ya utoaji huduma na elimu kwa mlipakodi iliyomalizika mwishoni mwa wiki ikiwa na lengo la kutoa elimu kuhusu masuala mbalimbali ya kodi, kusajili wafanyabiashara wapya, pamoja na kusikiliza malalamiko, changamoto na maoni kutoka kwa wafanyabiashara hao.

Meneja wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Mkoa wa Geita James Jilala (kulia) akijadiliana jambo na Meneja wa Huduma na Elimu kwa Mlipakodi kutoka TRA Makao Makuu Gabriel Mwangosi wakati wa kampeni maalum ya utoaji huduma na elimu kwa mlipakodi iliyomalizika mwishoni mwa wiki mkoani Geita. Katikati ni Afisa wa Kodi Mwandamizi wa TRA Makao Makuu Maternus Mallya.


Hivyo makala TRA YASAJILI WAFANYABIASHARA WAPYA 600 MKOANI GEITA

yaani makala yote TRA YASAJILI WAFANYABIASHARA WAPYA 600 MKOANI GEITA Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.

Wewe ni sasa kusoma makala TRA YASAJILI WAFANYABIASHARA WAPYA 600 MKOANI GEITA mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2018/04/tra-yasajili-wafanyabiashara-wapya-600.html

Subscribe to receive free email updates:

Related Posts :

0 Response to "TRA YASAJILI WAFANYABIASHARA WAPYA 600 MKOANI GEITA"

Post a Comment