TCRA YATOA HUKUMU KWA RADIO TIMES FM, CLOUDS FM

TCRA YATOA HUKUMU KWA RADIO TIMES FM, CLOUDS FM - Hallo rafiki WORLD MAELEZO LATEST, Katika makala kusoma wakati huu na kichwa TCRA YATOA HUKUMU KWA RADIO TIMES FM, CLOUDS FM, tumeandaa vizuri kwa makala hii kusoma na kupakua maelezo humo. pengine kujaza posts makala afya, makala biashara, makala general, makala hobby, makala karibuni info, makala michezo, makala siasa, makala utamaduni, sisi kuandika anaweza kuelewa. Naam, furaha ya kusoma.

title : TCRA YATOA HUKUMU KWA RADIO TIMES FM, CLOUDS FM
kiungo : TCRA YATOA HUKUMU KWA RADIO TIMES FM, CLOUDS FM

soma pia


TCRA YATOA HUKUMU KWA RADIO TIMES FM, CLOUDS FM

Na Ropota Wetu,Globu ya jamii

KAMATI ya Maudhui ya Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA),imetoa hukumu kwa vituo viwili vya radio vya Times FM na Clouds FM kwa makosa ya ukiukwaji wa kanuni za utangazaji za mwaka 2018.

Taarifa iliyotolewa leo jijini Dar es Salaam imesema kuwa Radio ya Times FM walitangaza mahojiano na mwanamziki Nasib Abdul a.k.a Diamond Platinum.

Imeelezwa kwenye mahojiano hayo mwanamuziki huyo alitamka maneno yasiyofaa kimaudhui akimshambulia Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Juliana Shonza.
"Times FM wamepewa onyo na kutakiwa kumuomba radhi Naibu Waziri Shonza na jamii kwa ukiukwaji huo wa maadili ya utangazaji,"imesema sehemu ya taarifa hiyo.

Kuhusu Radio ya Clouds FM ni kwamba imepewa onyo kwa kutozingatia mizania ya utoaji wa habari uliohusu pande mbili ya mwanamuziki Ibrahim Musa a.k.a Roma mkatoliki na Naibu Waziri Shonza.


Hivyo makala TCRA YATOA HUKUMU KWA RADIO TIMES FM, CLOUDS FM

yaani makala yote TCRA YATOA HUKUMU KWA RADIO TIMES FM, CLOUDS FM Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.

Wewe ni sasa kusoma makala TCRA YATOA HUKUMU KWA RADIO TIMES FM, CLOUDS FM mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2018/04/tcra-yatoa-hukumu-kwa-radio-times-fm.html

Subscribe to receive free email updates:

Related Posts :

0 Response to "TCRA YATOA HUKUMU KWA RADIO TIMES FM, CLOUDS FM"

Post a Comment