title : SERIKALI YAIPELEKA SERA YA TAIFA YA MASHIRIKA YASIYO YA KISERIKALI KWA WADAU KUPATA MAONI
kiungo : SERIKALI YAIPELEKA SERA YA TAIFA YA MASHIRIKA YASIYO YA KISERIKALI KWA WADAU KUPATA MAONI
SERIKALI YAIPELEKA SERA YA TAIFA YA MASHIRIKA YASIYO YA KISERIKALI KWA WADAU KUPATA MAONI
Na Mwandishi Wetu- Arusha
Serikali kupitia Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto imedhamiria kufanya mabadiliko katika Sera zake mbalimbali ili kuweza kuendana na wakati na kuwezesha kushirikiana na wadau wa maendeleo kutoa huduma kwa watanzania.
Katika kulifanikisha hilo Wizara imeamua kuipeleka Sera ya Taifa ya Mashirika Yasiyo ya Kiserikali ya mwaka 2001 kwa wadau ili iweze kutolewa maoni na baadae kufanyiwa marekebisho kuiwezesha kuendana na wakati.
Akifungua kikao kazi cha wadau wa Mashirika Yasiyo ya kiserikali kuijadili Sera ya Taifa ya Mashirika yasiyo ya Kiserikali Jijini Arusha, Katibu Mkuu Idara Kuu Maendeleo ya Jamii Bibi Sihaba Nkinga amesema kuwa maoni ya wadau ni muhimu sana katika mchakato wa maboresho wa Sera hiyo.
Bibi. Sihaba Nkinga ameleza kuwa Serikali imeamua kuwashirikisha wadau hao kwani kwa asilimia kubwa ndio watekelezaji wa Sera hiyo katika majukumu yao ya kila siku.
Ameongeza kuwa Serikali inatambua mchango wa kazi zinazofanywa na Mashirika Yasiyo ya Kiserikali nchini na zoezi hili la kuiboresha Sera hiyo litaleta mageuzi makubwa katika Sekta.
Katibu Mkuu Idara Kuu Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Sihaba Nkinga akizungumza na wadau wa Mashirika Yasiyo ya Kiserikali wakati akifungua kikao kazi kilichofanyika Jijini Arusha kilichowakutanisha wadau hao kujadili maboresho ya Sera ya Taifa ya Mashirika Yasiyo ya Kiserikali.
Msajili wa Mashirika Yasiyo ya Kiserikali, Marcel Katemba akitoa ufafanuzi kuhusu masuala mbalimbali ya kisera wakati wa ufunguzi wa kikao kazi kilichofanyika Jijini Arusha kilichowakutanisha wadau wa NGOs kujadili maboresho ya Sera ya Taifa ya Mashirika Yasiyo ya Kiserikali.
Mwenyekiti wa Baraza la Taifa la Mashirika Yasiyo ya Kiserikali, Nicholous Zakaria akieleza kuhusu umuhimu wa Baraza katika kuratibu utendaji kazi wa Mashirika yasiyo ya Kiserikali nchini wakati wa ufunguzi wa kikao kazi kilichofanyika Jijini Arusha kilichowakutanisha wadau hao kujadili maboresho ya Sera ya Taifa ya Mashirika Yasiyo ya Kiserikali.
Baadhi ya wadau wa Mashirika Yasiyo ya Kiserikali wakifuatilia mada mbalimbali katika kikao kazi kilichofanyika Jijini Arusha kilichowakutanisha wadau hao kujadili maboresho ya Sera ya Taifa ya Mashirika Yasiyo ya Kiserikali.
Katibu Mkuu Idara Kuu Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Bibi Sihaba Nkinga akiwa katika picha ya pamoja na wadau wa Mashirika Yasiyo ya Kiserikali nchini mara baada ya kufungua kikao kazi kilichofanyika Jijini Arusha kilichowakutanisha wadau hao kujadili maboresho ya Sera ya Taifa ya Mashirika Yasiyo ya Kiserikali watatu kulia waliokaa ni Mkurugenzi na Masajili wa Mashirika Yasiyo ya Kiserikali Bw. Marcel Katemba. Picha na Kitengo cha Mawasiliano WAMJW
KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA
KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA
Hivyo makala SERIKALI YAIPELEKA SERA YA TAIFA YA MASHIRIKA YASIYO YA KISERIKALI KWA WADAU KUPATA MAONI
yaani makala yote SERIKALI YAIPELEKA SERA YA TAIFA YA MASHIRIKA YASIYO YA KISERIKALI KWA WADAU KUPATA MAONI Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala SERIKALI YAIPELEKA SERA YA TAIFA YA MASHIRIKA YASIYO YA KISERIKALI KWA WADAU KUPATA MAONI mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2018/04/serikali-yaipeleka-sera-ya-taifa-ya.html
0 Response to "SERIKALI YAIPELEKA SERA YA TAIFA YA MASHIRIKA YASIYO YA KISERIKALI KWA WADAU KUPATA MAONI"
Post a Comment