QATAR AIRWAYS YATEMBEZA WAANDISHI MJINI DOHA.

QATAR AIRWAYS YATEMBEZA WAANDISHI MJINI DOHA. - Hallo rafiki WORLD MAELEZO LATEST, Katika makala kusoma wakati huu na kichwa QATAR AIRWAYS YATEMBEZA WAANDISHI MJINI DOHA., tumeandaa vizuri kwa makala hii kusoma na kupakua maelezo humo. pengine kujaza posts makala afya, makala biashara, makala general, makala hobby, makala karibuni info, makala michezo, makala siasa, makala utamaduni, sisi kuandika anaweza kuelewa. Naam, furaha ya kusoma.

title : QATAR AIRWAYS YATEMBEZA WAANDISHI MJINI DOHA.
kiungo : QATAR AIRWAYS YATEMBEZA WAANDISHI MJINI DOHA.

soma pia


QATAR AIRWAYS YATEMBEZA WAANDISHI MJINI DOHA.

Qatar Airways yapeleka waandishi kutoka vituo mbalimbali vya habari na utangazaji  vya Africa kwa ajili ya matembezi mjini Doha. Katika matembezi hayo wanahabari walipata fursa ya kutembelea maeneo mbalimbali kama Makumbusho ya Sanaa ya kiislamu (museum of Islamic art) haya ni makumbusho yaliyopo katika mji mkuu wa Qatar, Doha. Pia walitembelea Kijiji cha kitamaduni cha Katara, Katara ni kijiji kitamaduni huko Doha, Qatar. 

Iko katika pwani ya mashariki kati ya West Bay na Lulu ambayo Ilifunguliwa mnamo Oktoba 2010. Walitembelea The Grand Mosque, Msikiti wa Kitaifa Qatar. Huu ni mojawapo ya misikiti mikubwa ya kihistoria nchini Qatar, Msikiti huu uko katika wilaya ya Jubailat Doha. Wanahabari hao pia walipata nafasi ya kutembelea maeneo kama Souq waqif, Falcon souq, na Gold souq ambapo waliweza kujionea vitu vingi kama mapambo na vito vya thamani vilivyotengenezwa kwa dhahabu na madini ya aina mbalimbali.

Katika ziara yao mjini Doha waandishi wa habari walitembelea Qatar foundation, Al Shaqab sehemu ambayo hutumika kuwapa mafunzo farasi katika jamii za kiarabu, the Pearl na Khalifa International Stadium; ambayo inajulikana kama Uwanja wa Taifa, ni uwanja unaotumika kwa shughuli mbalimbali huko Qatar ambao pia ni kama sehemu ya eneo la Doha Sports City, ambalo linajumuisha Aspire Academy, Kituo cha Hamad Aquatic, na Aspire Tower park. Uwanja ulipewa jina hilo baada ya Khalifa bin Hamad Al Thani, ambaye zamani alikuwa kiongozi wa dini ya kiislamu (Emir) nchini Qatar. Mbali na maeneo hayo wanahabari walitembelea Regency sealine camp, Desert Safari, pia kituo cha utangazaji cha Al Jazeera.

Qatar Airways ina Zaidi ya miaka 20 katika kutoa huduma za anga, Ni shirika la ndege ambalo limejishindia tuzo mbalimbali ambapo kwa mwaka 2017 Qatar airways ilipata tuzo nyingi Zaidi ya tano na mwaka huu  imeshinda tuzo mbalimbali zikiwemo Crystal cabin award, Skytrax world airport award 2018, 2018 TripAdvisor travelers’ choice awards na Apex passenger choice award 2018. Qatar Airways imeshinda tuzo za Skytrax airline of the year mara nne (4) mfululizo katika miaka ya 2011, 2012, 2015 na 2017.

                                       “QATAR AIRWAYS, GOING PLACES TOGETHER.” 
    
 Wanahabari kutoka Tanzania wakiwa katika picha ya pamoja walipokwenda kutembelea Makumbusho ya sanaa ya kiislamu mjini Doha.
 Waandishi na wadau wa habari wakiwa wamepumzika baada ya kuwasili Hamad International Airport mjini Doha, Qatar.  
Waandishi na wadau wa habari kutoka nchi mbalimbali za Africa i.e Tanzania, Uganda wakiwa katika picha ya pamoja walipokuwa Doha.



Hivyo makala QATAR AIRWAYS YATEMBEZA WAANDISHI MJINI DOHA.

yaani makala yote QATAR AIRWAYS YATEMBEZA WAANDISHI MJINI DOHA. Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.

Wewe ni sasa kusoma makala QATAR AIRWAYS YATEMBEZA WAANDISHI MJINI DOHA. mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2018/04/qatar-airways-yatembeza-waandishi-mjini.html

Subscribe to receive free email updates:

Related Posts :

0 Response to "QATAR AIRWAYS YATEMBEZA WAANDISHI MJINI DOHA."

Post a Comment