title : NI MARUFUKU KURUKA NYUMBA WAKATI WA KUWAUNGANISHIA UMEME WA REA WANANCHI- DKT KALEMANI
kiungo : NI MARUFUKU KURUKA NYUMBA WAKATI WA KUWAUNGANISHIA UMEME WA REA WANANCHI- DKT KALEMANI
NI MARUFUKU KURUKA NYUMBA WAKATI WA KUWAUNGANISHIA UMEME WA REA WANANCHI- DKT KALEMANI
-Wekeni hata kwenye nyumba za nyasi
Na Tiganya Vincent
SERIKALI imesema ni marufuku kwa Wakandarasi na Wataalamu kuruka nyumba wakati wa uunganishaji wa umeme kwa wananchi kupitia Mradi kabambe wa kusambaza Umeme Vijijini Awamu ya Tatuunatekelezwa na Wakala wa Umeme Vijijini (REA).
Kauli hiyo ilitolewa jana wilayani Urambo na Kaliua na Waziri wa Dkt. Medard Kalemani wakati alipokuwa akigaua utekelezaji wa zoezi la usambazaji wa umeme wa REA katika maeneo hayo.
Alisema ni marufuku kuruka nyumba hata kama ni nyasi kama mwananchi anataka umeme na amelipa shilingi 27,000 za kuunganishiwa umeme.
Kalemani alisema kuwa mpango wa Serikali ni kuhakikisha umeme unafika katika vijiji na vitongoji vyote na kwa wananchi wote bila kubagua.
“Nawaagiza Wakandarasi na Wataalamu wote hakuna kuruka nyumba wala kubagua nyumba kwa sababu ya kuwa imeezekwa kwa nyasi…umeme ni nyumba kwa nyuma , kaya kwa kaya.., hata kama mtu hajakamisha nyumba yake kama kuna mti karibu na nyumba yake wekeeni hata hapo ili iwe rahisi kuingiza umeme atakapokuwa amekamisha nyumba yake” alisisitiza Waziri huyo.
Waziri wa Nishati Dkt Medard Kalemani(mwenye miwani) na Mbunge wa Urambo Magreth Sitta na viongozi wengine wakikata utepe wa uzinduzi wa uwashaji wa umeme wa REA katika Kijiji cha Jionee Mwenyewe kata ya Songambele jana.
Waziri wa Nishati Dkt Medard Kalemani akibonyesha kitufe kuwasha umeme katika Kijiji cha Jionee Mwenyewe Kata ya Songambele baada ya kukamilika kwa mradi wa uwekaji wa miundombinu katika eneo hilo.
Waziri wa Nishati Dkt Medard Kalemani(mwenye miwani) na Mbunge wa Urambo Magreth Sitta(kushoto) na wananchi wa kiijiji cha Jionee Mwenyewe kata ya Songambele wakishangilia mara baada ya uzinduzi wa uwashaji wa umeme katika eneo hilo jana.
Waziri wa Nishati Medard Kalemani akimpongeza Diwani wa Kata ya Vumilia kupitia ACT Wazalendo Kassim Shushu (kushoto) baada ya kumkabidhi eneo la shamba lake linalokadiriwa kuwa ekari moja kwa ajili ya ujenzi wa Kituo cha Kupozea umeme. Picha na Tiganya Vincent
KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA
KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA
Hivyo makala NI MARUFUKU KURUKA NYUMBA WAKATI WA KUWAUNGANISHIA UMEME WA REA WANANCHI- DKT KALEMANI
yaani makala yote NI MARUFUKU KURUKA NYUMBA WAKATI WA KUWAUNGANISHIA UMEME WA REA WANANCHI- DKT KALEMANI Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala NI MARUFUKU KURUKA NYUMBA WAKATI WA KUWAUNGANISHIA UMEME WA REA WANANCHI- DKT KALEMANI mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2018/04/ni-marufuku-kuruka-nyumba-wakati-wa.html
0 Response to "NI MARUFUKU KURUKA NYUMBA WAKATI WA KUWAUNGANISHIA UMEME WA REA WANANCHI- DKT KALEMANI"
Post a Comment