MVUA YAUA WATU NANE DAR , MAKONDA ATOA TAHADHARI

MVUA YAUA WATU NANE DAR , MAKONDA ATOA TAHADHARI - Hallo rafiki WORLD MAELEZO LATEST, Katika makala kusoma wakati huu na kichwa MVUA YAUA WATU NANE DAR , MAKONDA ATOA TAHADHARI, tumeandaa vizuri kwa makala hii kusoma na kupakua maelezo humo. pengine kujaza posts makala afya, makala biashara, makala general, makala hobby, makala karibuni info, makala michezo, makala siasa, makala utamaduni, sisi kuandika anaweza kuelewa. Naam, furaha ya kusoma.

title : MVUA YAUA WATU NANE DAR , MAKONDA ATOA TAHADHARI
kiungo : MVUA YAUA WATU NANE DAR , MAKONDA ATOA TAHADHARI

soma pia


MVUA YAUA WATU NANE DAR , MAKONDA ATOA TAHADHARI


*Ashauri wanafunzi wasiende shule kwa siku mbili, waliokuwa majumbani nao wakae huko huko

Na Said Mwishehe,Globu ya jamii

MVUA zinazoendelea kunyesha katika Jiji la Dar es Salaam imesababisha vifo vya watu nane katika Jiji hilo huku miundimbinu ya barabara nayo ikiharibiwa.

Akizungumza kuhusu athari za mvua ambazo zinaendelea kunyesha jijini Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam amesema taarifa ambazo anazo ni kwamba kuna watu 8 wamekufa kutokana na mvua hizo.Amefafanua taarifa rasmi itatolewa kwani kinachoendelea sasa ameagiza kata zote kufanya tathimini ya athari za mvua hizo.

Ameongeza vifo hivyo vimetokana na mafuriko katika baadhi ya maeneo ya Jiji la Dar es Salaam ambapo ameeleza ipo haja ya wakazi wa Jiji hilo kuhakikisha wanakuwa makini katika kipindi hiki ambacho mvua zinaendelea kunyesha.

"Mvua hizi zimesababisha maafa ambako taarifa ambazo ninazo kuna watu 8 wamefariki dunia kwasababu ya hizi mvua.Tutatoa taarifa rasmi baadae.Pia mvua zimesababisha kuharibika kwa miundombinu na barabara nyingi kutopitika,"amesema Makonda wakati anazungumzia athari za mvua akiwa eneo la Jangwani jijini Dar es Salam ambako eneo hilo maji yamejaa.

Pia Makonda amesema athari za mvua hizo zingeweza kuwa kubwa zaidi iwapo watu wangetoka majumbani kwao, na hivyo ameshauri ni vema Walimu wakuu wa mkoa wa Dar es Salaam wakatoa ruhusa kwa siku mbili ili wanafunzi wasiende shule ili kuepuka maafa kwani baadhi ya magari yamekuwa yakitumbukia mtoni.

"Nito rai kwa walimu wakuu na hasa kwa Ofisa Elimu Mkoa wa Dar es Salaam kuwapa taarifa walimu wa shule zote kuwa kwa siku mbili hizi yaani Jumanne na Jumatano wanafunzi wasiende shuleni.

"Hii itasaidia kupunguza maafa ambayo yanaweza kutokea kwa kuruhusu watoto waende shule huku tukijiua miundombini yetu haiko salama.Kwa wale ambao wako mabodeni nishauri waondoke huko kwani wanaweza kupata athari zaidi na kwamba hakuna sababu ya kupanda juu ya paa la nyumba kulinda bati,"amefafanua Makonda.

Makonda ameitumia siku ya leo kufanya ziara ya kuzunguka maeneo mbalimbali ya Jiji la Dar es Salaam ambako ameshuhudia namna ambavyo mvua hiyo imeleta madhara katika maeneo mbalimbali ambapo ametumia nafasi hiyo kuwataka wakazi wa mkoa huo kuhakikisha hawajengi kwenye njia za maji na kubwa zaidi kutunza mazingira.


Hivyo makala MVUA YAUA WATU NANE DAR , MAKONDA ATOA TAHADHARI

yaani makala yote MVUA YAUA WATU NANE DAR , MAKONDA ATOA TAHADHARI Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.

Wewe ni sasa kusoma makala MVUA YAUA WATU NANE DAR , MAKONDA ATOA TAHADHARI mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2018/04/mvua-yaua-watu-nane-dar-makonda-atoa.html

Subscribe to receive free email updates:

Related Posts :

0 Response to "MVUA YAUA WATU NANE DAR , MAKONDA ATOA TAHADHARI"

Post a Comment