title : MKAZI DAR AMLILIA RC MAKONDA AMSAIDIE KUPATA NYUMBA YAKE AMBAYO ANADAI AMEDHULUMIWA
kiungo : MKAZI DAR AMLILIA RC MAKONDA AMSAIDIE KUPATA NYUMBA YAKE AMBAYO ANADAI AMEDHULUMIWA
MKAZI DAR AMLILIA RC MAKONDA AMSAIDIE KUPATA NYUMBA YAKE AMBAYO ANADAI AMEDHULUMIWA
Na Emmanul Masaka ,Globu ya jamii
MKAZI wa Mnazi Mmoja barabara ya Sukuma na Mafya jijini Dar es Salaam Wechu Salumu Abdallah amempigia magoti Mkuu wa Mkoa huo Paul Makonda ili amsaidie nyumba yake kwani amedai amedhulumiwa na kupigwa mnada .
Akizungumza na waandishi wa habari Wechu Abdallah amesema anamwomba Mkuu wa Mkoa asikie kilio chake kwani amedhulumiwa nyumba ambayo ni ya urithi,waliyoaachiwa ambapo wapo ndugu wanne wanaimiliki nyumba hiyo.
Amesema nyumba hiyo ya urithi amedhulumiwa na mtu (amemtaja kwa jina)mbaye amemtaja jina(nayefahamika kwa jina)ambaye anaminayo kampuni na alikubaliana naye kujenga ghoropha 8 ambazo wangegawana.
Amesema lakini baadae amegeuka na kuchukua nyumba hiyo na kuipiga mnada ambapo ametakiwa kuweka zuio kwa siku 14 tu."Mkuu wa mkoa naomba unisaidie mimi mnyonge nimeachiwa watoto nawahudumia hakuna anayenisaidia, hivyo nakuomba mkuu wa mkoa wangu unisaidie nipate haki," amesema
Ameeleza yeye pamoja na ndugu zake hao walioachiwa nyumba hiyo walikubali kuwa mjenzi huyo ajenge ghorofa hizo 8 ambapo wangegawana 4 kwa 4 na kutokana na makubaliano hayo walifuata misingi yote ya sheria na wakaandikishana kwa makubaliano ya kujenga ghorofa.Amendelea kueleza mmoja wa mrithi wa mali hizo aliamua kuondoka kwenye mkataba na kutaka apewe gawio la fedha zake ambazo ni takribani ya Sh.milioni 7.6 ambapo walimweleza mjenzi wao na kukubali kumpatika kasi hicho cha fedha wakaandikishiana na wakampatia kiasi cha fedha hizo lakini dada yao huyo alitaka kuongezewa.
Amesema wamwambia kuwa anataka kuongezewa hivyo wakaenda mahakamani na kuhakikisha wakafanya makubaliano ambapo mjenzi huyo aliwapatia fedha hizo na kumpatia dada yao,na baada ya hapo walitakiwa kumwondoa katika makubaliano.Aidha mama huyu amemwomba Makonda kumsaidia kwani nyumba hiyo tayari imeuzwa na mnada ulifanyika bila ya matangazo yoyote na wakati kesi bado uko mahakamani.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa Mtaa Baragashi Azimio amesema ni kweli nyumba hiyo imepigwa mnada na watu waliofika kuleta tangazo ofisini kwake.Hata hivyo imepigwa mnada pasipokuwa na matangazo kwa wananchi wa mtaa huo kuwa nyumba inauzwa .
Nyumba hiyo iliyopo Mtaa wa Sukuma Kariakoo Ilala jijini Dar es Salaam ilipigwa mnada na kuuzwa kwa thamani ya Sh. milioni 350 ambapo walifanya mnada bila ya kumshirikishwa Msimamizi wa mirathi hiyo.

Mkazi wa Kariakoo jijini Dar as Salaam,Uwechu Salumu Abdallah akizungumza na waandishi wa habari juu ya kumuomba Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda amsaidie kutokana na kudhulumiwa nyumba ya urithi.
Hivyo makala MKAZI DAR AMLILIA RC MAKONDA AMSAIDIE KUPATA NYUMBA YAKE AMBAYO ANADAI AMEDHULUMIWA
yaani makala yote MKAZI DAR AMLILIA RC MAKONDA AMSAIDIE KUPATA NYUMBA YAKE AMBAYO ANADAI AMEDHULUMIWA Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala MKAZI DAR AMLILIA RC MAKONDA AMSAIDIE KUPATA NYUMBA YAKE AMBAYO ANADAI AMEDHULUMIWA mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2018/04/mkazi-dar-amlilia-rc-makonda-amsaidie.html
0 Response to "MKAZI DAR AMLILIA RC MAKONDA AMSAIDIE KUPATA NYUMBA YAKE AMBAYO ANADAI AMEDHULUMIWA"
Post a Comment