title : MAHAKAMA YAAGIZA HANS POPE , LAUWO WAKAMATWE, WAUNGANISHWE KESI UTAKATISHAJI FEDHA
kiungo : MAHAKAMA YAAGIZA HANS POPE , LAUWO WAKAMATWE, WAUNGANISHWE KESI UTAKATISHAJI FEDHA
MAHAKAMA YAAGIZA HANS POPE , LAUWO WAKAMATWE, WAUNGANISHWE KESI UTAKATISHAJI FEDHA
Na Karama Kenyunko, Globu ya jamii
MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi Kisutu imeamuru, aliyekuwa Mwenyekiti wa Kamati ya Usajili ya Simba Sports Club, Zacharias Hans Pope na Mkandarasi wa uwanja wa club hiyo, Frank Peter Lauwo waka matwe na kufikishwa mahakamani kujibu mashtaka yanayowakabili.
Washtakiwa hao wameongezwa katika kesi ya utakatishaji fedha na kugushi inayomkabili Rais wa Simba, Evans Aveva na Makamu wake, Geofrey Nyange maarufu Kaburu.

Amri hiyo imetolewa leo na Hakimu Mkazi Mkuu Thomas Simba wa mahakama hiyo baada ya Swai kudai amewatafuta washtakiwa hao toka Machi mwaka huu bila mafanikio na kuomba hati ya kuwakamata washtakiwa hao ambao hawakuepo mahakamani
Kutokana na mabadiliko hayo washtakiwa wamesomewa upya hati ya mashtaka na wanakabiliwa na jumla ya mashtaka 10 tofauti na hati ya mashtaka ya zamani iliyokuwa na mashtaka matano.
Wakili wa Serikali kutoka Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa Tanzania(Takukuru) Leornad Swai ameda kesi hiyo leo ilikuja kwa ajili ya kuwasomea washtakiwa hao maelezo ya awali lakini ameomba kufanyia madaliko hati ya mashtaka.Katika mashtaka hayo washtakiwa wanakabiliwa na shtaka la kula njama, kutoa nyaraka za uongo, matumizi mabaya ya madaraka, kughushi, utakatishaji, kuwasilisha nyaraka za kughushi na kuendesha biashara bila kufuata sheria.
Akisoma mashataka hayo, Swai amedai, kwenye shtaka la kwanza, Aveva na Nyange, walikula njama ya kutenda kosa la kutumia madaraka vibaya, pia wanadaiwa kati ya Machi 10 na 16 jijini Dar es Salaam, walitumia madaraka yao vibaya kwa kuandaa fomu ya maombi ya Machi 15/2016 na kuhamisha dola za Marekani 300,000 kutoka kwenye akaunti ya Simba iliyopo CRDB tawi la Azikiwe kwenda kwenye akaunti binafsi ya Barclays kwa madhumuni ya kujipatia faida.
Katika tarehe hizo hizo wakiwa Dar es Salaam kwa pamoja walighushi nyaraka iliyokuwa ikionyesha simba inalipa mkopo wa Dola za Marekani 300,000 kwa Aveva kitu ambacho si kweli.
Aidha wote kwa pamoja waliwasilisha nyaraka ya kughushi, inadaiwa kuwa Aveva Machi 15 mwaka 2016 katika benki ya CRDB aliwasilisha nyaraka ya uongo ikionesha Simba wanalipa mkopo wa dola 300,000.Katika shtaka la utakatishaji fedha linalomkabili Aveva, imedaiwa Machi 15 mwaka 2016 katika benki ya Baclays Mikocheni alijipatia Dola 187,817 wakati akijua zimetokana na zao la kosa la kughushi.
Pia katika shitaka la sita la imedaiwa Nyange alimsaidia Aveva kujipapatia dola 187,817 kotoka kwenye akaunti ya Simba wakiwa wanajua fedha hizo zimetokana na zao la kughushiKatika na shtaka la saba la kughushi, linaloqakabili mstakiwa wa Aveva, Nyange na Poppe.
Imedaiwa katika tarehe hizo hizo kwa pomoja walighushi hati ya malipo ya kibiashara ya Mei 28/ 2016 wakionesha nyasi bandia zilizonunuliwa na Simba zinathamani ya USD 40,577 huku wakijua kwamba sio kweli.Katika shtaka la nane imedaiwa, , Aveva aliwasilisha hati ya madai (commercial invoice), ya uongo kwa Levison Kasulwa ya Mei 28/ 2016 kwa madhumuni ya kuonyesha kwamba Simba wamenunua nyasi bandia zenye thamani ya dola 40,577
Katika Shtaka la tisa Aveva, Nyange na Zacharia Machi 10 mwaka 2016 na Septemba 30 mwaka 2016 waliwasilisha nyaraka za uongo kuonyesha Simba imenunua nyasi bandia zenye thamani ya USD 40,577.Katika shtaka la mwisho imedaiwa, kati ya Machi na Septemba 2016 Lauwo aliendesha biashara kama mkandarasi kwa kujenga uwanja wa Simba uliopo Bunju jijini Dar es Salaam wakati akiwa hajasajiliwa
Hata hivyo washtakiwa wamekana mashtaka hayo yote na wamepelekwa rumande kwa sababu shtaka la utakatishaji fedha linalowakabili halina dhamana.Kesi hiyo imahirishwa hadi Mei,14 mwaka 2018 kwa ajili ya kutajwa na kufuatilia kama washtakiwa hao wawili watakuwa wamekamatwa.

Hivyo makala MAHAKAMA YAAGIZA HANS POPE , LAUWO WAKAMATWE, WAUNGANISHWE KESI UTAKATISHAJI FEDHA
yaani makala yote MAHAKAMA YAAGIZA HANS POPE , LAUWO WAKAMATWE, WAUNGANISHWE KESI UTAKATISHAJI FEDHA Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala MAHAKAMA YAAGIZA HANS POPE , LAUWO WAKAMATWE, WAUNGANISHWE KESI UTAKATISHAJI FEDHA mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2018/04/mahakama-yaagiza-hans-pope-lauwo.html
0 Response to "MAHAKAMA YAAGIZA HANS POPE , LAUWO WAKAMATWE, WAUNGANISHWE KESI UTAKATISHAJI FEDHA"
Post a Comment