title : KAYA 6120 ZA WALENGWA WA TASAF ZALIMA PAMBA EKARI 8712 MSIMU WA MWAKA 2017/2018 MKOANI SIMIYU
kiungo : KAYA 6120 ZA WALENGWA WA TASAF ZALIMA PAMBA EKARI 8712 MSIMU WA MWAKA 2017/2018 MKOANI SIMIYU
KAYA 6120 ZA WALENGWA WA TASAF ZALIMA PAMBA EKARI 8712 MSIMU WA MWAKA 2017/2018 MKOANI SIMIYU
Na Stella Kalinga, Simiyu
Kaya 6120 sawa na asilimia 52 ya walengwa wa Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini kupitia Mfuko wa Maendeleo ya Jamii (TASAF) katika Halmashauri ya Wilaya ya Bariadi Mkoani Simiyu zimewezeshwa kulima pamba ekari 8712 katika Msimu wa mwaka 2017/2018 kwa kutumia fedha za uhawilishaji.
Hayo yalibainishwa na Mratibu wa TASAF Mkoa wa Simiyu Bw. Nyasilu Ndulu wakati wa kikao cha kujenga uelewa wa pamoja kwa viongozi juu ya mpango huo kilichofanyika katika ukumbi wa KKKT mjini Bariadi.
Nyasilu amesema pamoja na kulima pamba walengwa wa mpango huo katika Wilaya ya Bariadi na wilaya nyingine Mkoani Simiyu, kupitia fedha za uhawilishaji (wanazopewa) wamefanikiwa kujenga nyumba, kufuga, kuanzisha biashara ndogo ndogo na kujiunga na Mfuko wa Afya ya Jamii(CHF).
Ameongeza kuwa tangu kuanza kwa zoezi la uhawilishaji chini ya Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini awamu ya tatu mwaka 2015 hadi sasa, tayari awamu 17 za malipo zimekwisha fanyika kwa walengwa 37, 533 na jumla ya shilingi bilioni 28.9 zimelipwa kwa wahusika.
Amesema fedha hizo zimejumuisha ruzuku za aina mbili ikiwa ni ruzuku ya msingi na ile itokanayo na utimizaji wa mashati ya Afya na Elimu ambapo watoto 39,068 sawa na asilimia 90.3 wameweza kupata mahitaji muhimu ya shule na kukuhudhuria shuleni na watoto 51, 280 sawa na asilimia 93.1 wamepata mahitaji ya kliniki na kupelekwa kliniki.
“Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini umeweza kuwasaidia walengwa kujikwamua kutoka kwenye umaskini, wapo walioanzisha biashara, wanaolima, wanaofuga, waliojenga nyumba bora; kwa kutumia fedha hizi wanazopewa wapo ambao watoto walikuwa hawahudhurii shuleni na kliniki lakini sasa hivi mahudhurio mazuri” Alisema.
Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe.Anthony Mtaka akizungumza na viongozi wa mkoa huo wakati alipofungua kikao cha kujenga uelewa wa pamoja kwa viongozi wa Mkoa huo juu ya Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini kilichofanyika katika ukumbi wa KKKT mjini Bariadi.
Katibu Tawala wa Mkoa wa Simiyu, Ndg.Jumanne Sagini akizungumza na viongozi wa mkoa huo katika kikao cha kujenga uelewa wa pamoja kwa viongozi wa Mkoa huo juu ya Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini kilichofanyika katika ukumbi wa KKKT mjini Bariadi.
Baadhi ya Viongozi wa Mkoa wa Simiyu wakimsikiliza Mkuu wa Mkoa huo, Mhe.Anthony Mtaka katika cha kujenga uelewa wa pamoja kwa viongozi wa Mkoa huo juu ya Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini kilichofanyika katika ukumbi wa KKKT mjini Bariadi.
Katibu Tawala wa Mkoa wa Simiyu, Ndg.Jumanne Sagini akizungumza na viongozi wa mkoa huo katika kikao cha kujenga uelewa wa pamoja kwa viongozi wa Mkoa huo juu ya Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini kilichofanyika katika ukumbi wa KKKT mjini Bariadi.
Baadhi ya Viongozi wa Mkoa wa Simiyu wakimsikiliza Mkuu wa Mkoa huo, Mhe.Anthony Mtaka katika cha kujenga uelewa wa pamoja kwa viongozi wa Mkoa huo juu ya Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini kilichofanyika katika ukumbi wa KKKT mjini Bariadi.
Hivyo makala KAYA 6120 ZA WALENGWA WA TASAF ZALIMA PAMBA EKARI 8712 MSIMU WA MWAKA 2017/2018 MKOANI SIMIYU
yaani makala yote KAYA 6120 ZA WALENGWA WA TASAF ZALIMA PAMBA EKARI 8712 MSIMU WA MWAKA 2017/2018 MKOANI SIMIYU Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala KAYA 6120 ZA WALENGWA WA TASAF ZALIMA PAMBA EKARI 8712 MSIMU WA MWAKA 2017/2018 MKOANI SIMIYU mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2018/04/kaya-6120-za-walengwa-wa-tasaf-zalima.html
0 Response to "KAYA 6120 ZA WALENGWA WA TASAF ZALIMA PAMBA EKARI 8712 MSIMU WA MWAKA 2017/2018 MKOANI SIMIYU"
Post a Comment