title : HESLB KUANZA KUPOKEA MAOMBI YA MIKOPO MWEZI UJAO
kiungo : HESLB KUANZA KUPOKEA MAOMBI YA MIKOPO MWEZI UJAO
HESLB KUANZA KUPOKEA MAOMBI YA MIKOPO MWEZI UJAO
- Yawakumbusha waombaji kuandaa nyaraka muhimu
- Mwongozo wa kina kutolewa mwanzoni mwa Mei, 2018
Jumanne, Aprili 17, 2018
Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu (HESLB) inapenda kuwataarifu wananchi kuwa inatarajia kuanza kupokea maombi ya mikopo ya elimu ya juu kwa mwaka wa masomo 2018/2019 kuanzia wiki ya kwanza ya mwezi ujao (Mei, 2018) baada ya kukamilishwa kwa maboresho makubwa ya mfumo wa uombaji kwa njia ya mtandao.
Maboresho ya mfumo wa maombi
Mkurugenzi Mtendaji wa HESLB Bw. Abdul-Razaq Badru (pichani) amesema katika taarifa yake leo (Jumanne, Aprili 17, 2018) kuwa maombi yote yatapokelewa kwa njia ya mtandao (www.olas.heslb.go.tz) ambao umefanyiwa maboresho na Kituo cha Kompyuta cha Chuo Kikuu cha Dar es salaam (UCC-UDSM).
Aidha, Bw. Badru amesema dirisha hilo la litafunguliwa sambamba na kutangazwa kwa mwongozo wa kina utakaotoa utaratibu wa kuwasilisha maombi, tarehe ya mwisho ya kuwasilisha maombi, sifa na vigezo vitakavyotumika katika kuchambua na kutoa mikopo kwa mwaka ujao wa masomo unaotarajiwa kuanza mwezi Oktoba, 2018.
“Tunawasihi wale wote wanaotarajia kuomba mkopo wa elimu ya juu kusoma kwa makini mwongozo tutakaoutoa kwa vyombo vya habari na tovuti mwanzoni mwa mwezi Mei, 2018 na kuuzingatia,” amesema Bw. Badru.
Bw. Badru amefafanua kuwa wito wa Bodi ya Mikopo umetolewa kutokana na uzoefu wa miaka iliyopita ambapo waombaji wa mikopo waliwasilisha maombi yao bila kuzingatia mwongozo uliotolewa na kusababisha baadhi ya wanafunzi kukosa mikopo.
“Mwaka jana, kwa mfano, zaidi ya waombaji 10,027 kati ya waombaji zaidi ya 61,000 hawakuambatisha nyaraka muhimu kama vyeti vya kuzaliwa au hata vile vya vifo vilivyothibitishwa na Wakala wa Usajili, Ufilisi na Udhamini (RITA) kama tulivyoelekeza,” amesema.
Hivyo makala HESLB KUANZA KUPOKEA MAOMBI YA MIKOPO MWEZI UJAO
yaani makala yote HESLB KUANZA KUPOKEA MAOMBI YA MIKOPO MWEZI UJAO Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala HESLB KUANZA KUPOKEA MAOMBI YA MIKOPO MWEZI UJAO mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2018/04/heslb-kuanza-kupokea-maombi-ya-mikopo.html
0 Response to "HESLB KUANZA KUPOKEA MAOMBI YA MIKOPO MWEZI UJAO"
Post a Comment