title : Hafla ya Standard Chartered yabainisha viwanda 200 vya China kujengwa Tanzania
kiungo : Hafla ya Standard Chartered yabainisha viwanda 200 vya China kujengwa Tanzania
Hafla ya Standard Chartered yabainisha viwanda 200 vya China kujengwa Tanzania
Na Mwandishi wetu
CHINA katika kipindi cha miaka mitatu ijayo inatarajia kuwekeza katika viwanda 200 nchini Tanzania vitakavyokuwa na uwezo wa kuajiri moja kwa moja Watanzania laki mbili.
Kwa sasa uwekezaji wa China nchini Tanzania umetoa fursa za ajira za moja kwa moja 150,000 na zisizokuwa za moja kwa moja 350,000.
Taarifa hiyo imetolewa na Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Mh. Charles Mwijage katika hafla ya chakula cha jioni kwa wawekezaji kutoka China iliyoandaliwa na Benki ya Standard Chartered.
Aidha Waziri Mwijage alisema amefurahishwa na kauli iliyotolewa na Benki hiyo kwamba inawekeza dola za marekani bilioni 20 sawa na fedha za kitanzania trilioni 40 katika kampeni ya China ya uwezeshaji mitaji na biashara kutoka Asia kwenda nchi nyingine za dunia.
Kampeni hiyo inayoitwa One Belt One Road inagusa nchi 65, Tanzania ikiwamo.
Aliisifu Benki hiyo kwa kuandaa hafla hiyo kwa wateja wake wa China ikiwa ni sehemu moja ya kutangaza kampeni hiyo ya China na kuwafanya wananchi wengi kuelewa fursa zinazoambatana nazo.
Alisema kwa sasa Tanzania inapigana kuingia katika uchumi wa kati unaoendeshwa na viwanda na kampeni ya China inakwenda sawa na mpango wa maendeleo wa miaka mitano uliokazania uwekezaji katika viwanda.
Alisema kwa sasa Serikali inaweka vyema mazingira ya uwekezaji na ikiwa na uchumi unaokua kwa kasi wa asilimia 6 hadi 7 juhudi za Benki hiyo za kuonesha fursa za uwekezaji na uendeshaji wa uchumi zinakaribishwa na serikali ya Tanzania.
Aidha katika hotuba hiyo iliyosomwa na Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Uwekezaji wa Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Aristide Mbwasi alisema kwamba mpango huo wa China unaozungumzia uwezeshaji wa mitaji na biashara kutoka Asia kwenda nchi nyingine ni kichocheo cha kukua kwa chumi mbalimbali duniani na kutaka watanzania kushiriki kikamilifu.
Awali Ofisa Mtendaji Mkuu wa Benki hiyo nchini Tanzania, Sanjay Rughani alisema kwamba Benki ya Standard Chartered duniani inawekeza katika Belt and road Initiative kiasi cha dola bilioni 20 sawa na shilingi trilioni 44.8 za Kitanzania kuwezesha miradi mbalimbali kwenye kampeni hiyo ya China.
Alisema mwaka jana pekee benki hiyo iliingiliana mikataba katika miradi 40 kwenye nchi mbalimbali za mradi huo.
Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Uwekezaji wa Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Aristide Mbwasi akisoma hotuba kwa niaba ya Waziri wa wizara hiyo wakati wa hafla maalumu ya chakula cha jioni kwa wateja wa benki hiyo wa makampuni ya China nchini Tanzania iliyofanyika katika hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam.
Ofisa Mtendaji Mkuu wa Benki ya Standard Chartered, Sanjay Rughani akizungumza na wageni waalikwa wakati wa hafla maalumu ya chakula cha jioni kwa wateja wa benki hiyo wa makampuni ya China nchini Tanzania iliyoandaliwa na benki yake ambayo ilifanyika katika hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam.
Balozi wa China nchini, Mh. Wang Ke akitoa nasaha kwa wageni waalikwa wakati wa hafla wa maalumu ya chakula cha jioni kwa wateja wa benki hiyo wa makampuni ya China nchini Tanzania iliyofanyika katika hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam.
Pichani juu na chini ni baadhi ya wageni waalikwa waliohudhuria hafla maalumu ya chakula cha jioni kwa wateja wa benki hiyo wa makampuni ya China nchini Tanzania iliyofanyika katika hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam.
Picha ya pamoja ya meza kuu kutoka kulia ni Mjumbe wa Bodi ya Standard Chartered nchini, Ami Mpungwe, Ofisa Mtendaji Mkuu wa Benki ya Standard Chartered, Sanjay Rughani , Balozi wa China nchini, Mh. Wang Ke pamoja na Mwakilishi wa mgeni rasmi Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Uwekezaji wa Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Aristide Mbwasi.
Baadhi ya wafanyakazi wa benki ya Standard Chartered wakibadilishana mawazo wakati wa hafla maalumu ya chakula cha jioni kwa wateja wa benki hiyo wa makampuni ya China nchini Tanzania iliyofanyika katika hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam.
KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA
KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA
Hivyo makala Hafla ya Standard Chartered yabainisha viwanda 200 vya China kujengwa Tanzania
yaani makala yote Hafla ya Standard Chartered yabainisha viwanda 200 vya China kujengwa Tanzania Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala Hafla ya Standard Chartered yabainisha viwanda 200 vya China kujengwa Tanzania mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2018/04/hafla-ya-standard-chartered-yabainisha.html
0 Response to "Hafla ya Standard Chartered yabainisha viwanda 200 vya China kujengwa Tanzania"
Post a Comment