title : BIL.39 KULIPWA FIDIA WANANCHI KATIKA MRADI MWINGINE MKUBWA WA UMEME-MGALU
kiungo : BIL.39 KULIPWA FIDIA WANANCHI KATIKA MRADI MWINGINE MKUBWA WA UMEME-MGALU
BIL.39 KULIPWA FIDIA WANANCHI KATIKA MRADI MWINGINE MKUBWA WA UMEME-MGALU
SERIKALI imetenga kiasi cha sh.bilioni 39 kwa ajili ya kulipa fidia kwa wananchi ambao maeneo yao yatapitiwa na mradi wa umeme mkubwa unaotarajiwa kupitishwa kwenye maeneo yao.
Pamoja na hilo ,baadhi ya miradi ya awali ambayo fidia imechelewa kwa walengwa ,uhakiki tayari umekamilika na utaratibu ukikamilika malipo yatafanyika hivyo wananchi watoe shaka kwani serikali inataka ikabiliane na ubabaishaji.
Hayo yalisemwa na Naibu Waziri wa Nishati ,Subira Mgalu alipokuwa akizungumzia suala la fidia kwa baadhi ya wananchi watakaokuwa na haki ya kupatiwa.Alisema kuwa mradi huo ni mkubwa na utagharimu fedha nyingi.
Subira alielezea mradi unaanzia Rufiji, Kinyerezi,Kibaha na Chalinze na baadaye Dodoma ambapo wananchi watalipwa wakati utakapoanza.“Suala la fidia ni kubwa na kwa ile miradi ya awali ambayo haijalipwa ni kweli kwani baadhi bado hawajalipwa lakini wananchi wasiwe na wasi wasi kwani watalipwa fidia zao mara uhakiki utakapokamilika,” alisema Subira.
Alielezea ,kwa bajeti ambayo inaendelea kwa sasa zimetengwa kiasi cha sh.bilioni 21 kwa ajili ya fidia kwa laini inayoanzia Kinyerezi, Kibaha, Chalinze na Arusha ya umeme wa KV 400.Kwa mujibu wa Subira,mradi huo ulifanyiwa tathmini 2014/2015 na fidia imechelewa hivyo serikali inaomba radhi kwa hilo.
"Serikali ina majukumu na vipaombele mengi, haikusudii kuchelewesha bali mwaka unaoendelea wa bajeti zitalipwa tu,” alisema Subira.
Aidha alisema ,wakati Rais Dk. John Magufuli anaingia madarakani kulibainika kuwa kipindi cha nyuma kulikuwa na wizi mkubwa kwenye suala la fidia kwani walikuwa wakilipwa watu wasiostahili ambapo fedha inayopangwa na serikali inabadilishwa na kuwekwa viwango vingine hasa inapofika ngazi ya wilaya.
“Walikuwa wanabadili watu wanaopaswa kulipwa wanabadilisha majina na kila kitu hadi picha hata akilipwa anayestahili analipwa kiwango kisichotakiwa hali iliyosababisha hazina kufanya uhakiki,” alifafanua.Subira alisema, uhakiki tayari umefanyika na utaratibu ukikamilika malipo yatafanyika hivyo wananchi wasiwe na wasiwasi licha ya kucheleweshewa fidia zao bali serikali inataka iondokane na ubabaishaji
Hivyo makala BIL.39 KULIPWA FIDIA WANANCHI KATIKA MRADI MWINGINE MKUBWA WA UMEME-MGALU
yaani makala yote BIL.39 KULIPWA FIDIA WANANCHI KATIKA MRADI MWINGINE MKUBWA WA UMEME-MGALU Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala BIL.39 KULIPWA FIDIA WANANCHI KATIKA MRADI MWINGINE MKUBWA WA UMEME-MGALU mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2018/04/bil39-kulipwa-fidia-wananchi-katika.html
0 Response to "BIL.39 KULIPWA FIDIA WANANCHI KATIKA MRADI MWINGINE MKUBWA WA UMEME-MGALU"
Post a Comment